Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,666
- 729,790
Hii inatokana na ukweli kwamba magufuli sio mwanasiasa na hajui kuremba maneno
Wasiwasi na mashaka si kwasababu ya uhai wa chama la hasha! Chama kipo na kitaendelea kuwepo japo katika sura mpya kabisa...wasiwasi na mashaka ni kuhusu maslahi ya wachache, hapa ndio penye kimuhemuhe
Zile slogans ambazo mwanzoni ziliishia tu kwenye makaratasi sasa zitafufuka kwa vitendo
Slogans za Kusafisha chama, Kujivua gamba, Kurejea kwenye misingi, Kufukuza mafisadi nk....Sasa dalili ziko wazi kuwa zinakuja kwa vitendo
Lipo daraja la watu ambao maisha yao yote waliishi kupitia CCM wao na familia zao na marafiki zao..hizi zama zinafikia kikomo na hili hawapendi kuona linatokea
Hofu nyingine kubwa ni ule udhaifu mkubwa wa kibinadamu alionao Magu, udhaifu wa kuteua kwa ajili ya kukomoa kundi fulani, udhaifu wa kuteua watu hasa vijana wasiojua kingine zaidi ya ndio mzee, uteuzi wa watu wasiojua kuhoji na wanaotumia nguvu zaidi kuliko akili
Kuweza kuweka uwiano kwenye safu ya uongozi ndani ya CCM, uongozi utakaobadilisha sura ya chama na kukipa ustawi mpya bila kuathiri mahusiano ya nyuma yaweza kuwa changamoto kubwa kwake
Akiliweza hili atakuwa ameshinda vita kubwa lakini akitetereka akafanya kama alivyofanya kwenye teuzi za serikalini tutarajie CCM mpya isiyo na simile tafakuri wala uvumilivu...! Na mtifuano utaanzia hapo