CCM Chama Pekee Cha Siasa Chenye Dira na Mwelekeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Chama Pekee Cha Siasa Chenye Dira na Mwelekeo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Visible, Dec 10, 2009.

 1. Visible

  Visible Senior Member

  #1
  Dec 10, 2009
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heshima mbele wana JF:

  Kama kawaida najua wengi mtalipinga hili:

  CCM ni chama cha siasa ambacho kik madarakani tangu uhuru:

  Tulipotoka ni mbali na hadi tulipo lazima tukishukuru chama hiki kwa mambo yafuatayo:

  1.Amani na Utulivu nchini:Bila CCM na viongozi wake bora nadhani amani ya nchi hii isingefika hapa.

  -Tanzania ni taifa lenye amani duniani:
  -Naisifu CCM kwa hili; ukiangalia mataifa mbali mbali duniani vita na majanga mbali mabali unaweza gundua kuwa kweli Tanzania pamoja na umaskini wetu bado AMANI ni kitu muhimu sana na ni FAHARI YETU.
  -HONGERA CCM na tunashukuru kwa hili.

  2.Kukua kwa maendeleo:hapa tunazungumzia Elimu,Mawasiliano,Kilimo etc
  -Elimu hakuna ubishi toka kuwa na Chuo kikuu kimoja hadi sasa tunashukuru CCM na serikali yake bila wao nadhani tungechechemea kwa hili.
  -Mawasiliano:barabara na telecom kwa hili serikali imejitahidi sana na bado inaendelea kutengeneza barbara safi na za kisasa.
  -Kilimo kimeboreshwa na serikali bado inazidi kuhimiza kilimo kama njia ya kujikwamua kiuchumi.

  3.Kukua Kwa SIASA na democracy:CCM ingekuwa si chama kizuri nadhani sasa hivi TZ ingekuwa kama kwa kina castro Fidel CUBA:Yani kusingekkuwa na vyama vingi na tena vinajiexpress kama wapendavyo bial tabuu yoyote.
  -Katiba na utawala wa sheria pia ni kitu cha kujivunia.

  Kwa mlinganisho:Bado WAPINZANI hawawezi kuongoza nchii hii labda baada ya miaka mia hivi kwa wastani:

  sababu kubwa ikiwa ni :uchanga wa vyama na utitiri wake.
  -kukosekana kwa viongozi imara wenye msimamo na maamuzi mazito:
  -ulafi wa madaraka
  -wabunge waliochaguliwa kushindwa kabisa kusaidia wananchi ktk maendeleo na kuwakumbuka pindi za chaguzi.

  KWA MACHACHE HAYO NAOMBA MUONGEZE MENGINE MAZURI NA PIA MABAYA KAMA YAPO.

  HONGERA RAIS WETU HONGERA CCM:JK TUNAKUITAJI TENA MIAKA MITANO IJAYO:
   
 2. M

  Mvutakamba Member

  #2
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  You need to be ingored big time hakika Wadau huyu katumwa baada ya kumaliza kupima upepo kwa JK kuwa LIVE sasa wanakuja njia mpya . Hatuwezi kurudia kuridia mijadala okoa muda wetu wa kujadili mambo mengine bwana
   
 3. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Mkuu,wewe nio watakiwa uwe ignored hapa...Huu ni mtizamo wake(where we dare to talk openly).Cha msingi ni kumjibu kwa hoja(kwa nini hukubaliani na mtizamo wake) badala ya kuanza kumtuhumu kwamba KATUMWA na nani sijui...Wakati mwingine ni vizuri watu tukatofautiana kimtizamo aisee...Hoja hujibiwa kwa hoja na si blah blah kama hizo zako hapo juu...Pamo jah!!
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Dec 10, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Haya kweli sio matatizo ya wapinzani??

  -kukosekana kwa viongozi imara wenye msimamo na maamuzi mazito:
  -ulafi wa madaraka


  Unataka vithibitisho?
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Dec 10, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Hongera kwa lipi mkuu?

  dira ya CCM unayoisema ni ipi hiyo?

  Una hakika Tanzania kuna Amani?? hali ya mahospitalini, vibaka, kukosa ajira, elimu, umaskini , hivi navyo ni amani? au kwako definition ya amani ni nini?

  Huoni unaonekana mbinafsi sana kwa sababu unabonyabonya kwenye keyboard ya kwenye hiyo PC ya serikali basi haujui kuna watu wanalala na njaa nchi hii?
   
 6. Visible

  Visible Senior Member

  #6
  Dec 10, 2009
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu nimekugongea senksi hapo.
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,357
  Likes Received: 3,116
  Trophy Points: 280
  FIKRA MGANDO!!!!!
  We unajua kabisa unaongea pumba ndio maana umetahadharisha kuwa inawezekanna ukawakera wengi na ndivyo ilivyo.....
  Amani haiwezi kuletwa na ccm hata siku moja.......
  watz sio ccm........ndio maana kutokana na mfumo mbivu asilimia 90 hawapigi kura kwani hawaoni umuhimu kwa chama cha mafisadi.

  mbona US kila muhula kuna mabadiliko ya chama na kuna amani?
  mbona uingereza kuna mabadiliko ya vyama lakini kuna amanni
  hali kadhalika ujerumani na mataifa mengine
  Wanachojali wao ni sera.....
  watz tutakapogeuka na kuwa binadamu wa ukweli tutafaidi sana matunda ya nchi ...lakini tukiwa bei chee kiasi hiki kama akina zitto kununulika kwa bei ndogo kiasi hiki kamwe hatutafiak................
   
 8. Visible

  Visible Senior Member

  #8
  Dec 10, 2009
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  unauhakika ka nunuliwa?na nani?

  jenga hoja:

  na kama kanunuliwa utakubaliana nami kuwa ni udahifu wa upinzani au?
   
 9. I

  Inviolata Member

  #9
  Dec 10, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Are u sure kweli Tanzania kuna Amani?? Hivi wale watu wanaokufa kwa sababu ya kukosa hela ya matibabu (hata hela ya kununua panadol ya kutuliza maumivu hana, utasema wana amani, Je yule ambaye hata mlo mmoja kwa siku unamshinda utasema ana amani? Je na yule anayeshindwa kumpeleka mtoto wake shule kwa sababu hana hata hela ya kunua kiatu cha shule, uniform, au hata kalamu utasema ana amani? Au utasema hakuna watu wenye maisha duni kama hayo?????? Hiyo amani unayoiimba wewe naomba baada ya miaka 10 kama mtindo wa maisha utakuwa bado upo hivi wa viongozi kujilimbikizia mapesa na tabaka la wenye nacho na wasionacho kuongezeka njoo uniambie kama amani hiyo itakuwepo.
   
 10. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #10
  Dec 10, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Duh mzee hongera sana, manake kukifagilia chama kama hiki lazima uwe na roho ngumu zaidi ya ile ya kumchinja mwanao wa pekee kwa nia ya kumtoa kafara.
   
 11. Nostradamus

  Nostradamus JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina hakika hujatumwa,ila sina uhakika na uwezo wako wa kuchanaganua mambo..
  yooote uliyoyaorodhesha hayana point wala hayahitaji mtu mwenye busara zake ku-fall into dialogue na wewe.ila lazima nikubaliane na wewe jambo moja ''hakuna kiongozi ndani ya upinzani anayefaa kuongoza nchi'' kwani wengi wamezidiwa na ubinafsi,ukabila,uroho na ushirikina.
  Ila hilo halihalalishi uwepo w ccm madarakani.

  ''kutojitambua kumetufanya tushindwe kutambua mapungufu katika utambuzi wetu''
   
 12. A

  Amanikwenu Senior Member

  #12
  Dec 10, 2009
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ELNINO,

  Ni kweli. Kuisifia CCM lazima uwe na moyo wa kipekee na ushujaa kwa kifisadi.
   
 13. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #13
  Dec 10, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna methali moja ya kabila fulani inasema hivi. "Mtoto asiyetembea kwa majirani siku zote atamsifia mama yake kwamba ni mpishi mzuri". Nadhani hilo ndilo tatizo la mtoa hoja.

  Unaposema CCM wamefanya mazuri kulinganisha na nani? Na majirani? Mimi nadhani tunapaswa kujilinganisha na nchi ambazo zina amani kama Tanzania kuliko kujilinganisha na nchi ambazo muda mrefu zimekumbwa na ghasia. Ebu tujilinganishe na Zambia, Botswana, Malawi, na hata jirani yetu Kenya (hadi 2007). Ni dhahiri kwamba nchi hizi karibu zote zinatuzidi katika nyanza zote alizozitaja. Tanzania katika hali ya amani aliyoitaja mtoa hoja ingepaswa kuwa mbali zaidi kwa vile ni nchi tajiri sana kuliko nchi hizi nilizozitaja ambazo ni land locked! Utaniambia nini wakati hata bandari tuliyopewa na muumba wetu tumeshindwa kuitumia vizuri kulinganisha na Kenya! Alafu watu wanasema CCM imefanya vizuri?

  Ndio CCM imefanya vizuri ukilinganisha wa vyama vingine vilivyofanya vibaya sana katika nchi zao. Ni sawa na kusema mtoto wangu amekuwa wa kwanza katika kundi la wanafunzi walio feli mtihani! What a shame.
   
 14. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #14
  Dec 10, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Wewe Visible,
  Yule demu wako asharejea au ndio ametokomea kimoja na huyo jamaa mwenye Landcruiser?

  Kwa njia hii unafanya vyema kujipunguzia stress. Unajua tena maisha ya kuachwa!
   
 15. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #15
  Dec 10, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo la chama tawala ni utekelezaji wa kile viongozi wake wanachohubiri kila uchao. Itatuchukua zaidi ya nusu karne kutoka hapa tulipo kwa mwendo huu.
   
 16. Visible

  Visible Senior Member

  #16
  Dec 10, 2009
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  POINTLESS hivi umejiunga lini hapa JF?
   
 17. Visible

  Visible Senior Member

  #17
  Dec 10, 2009
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashangaaa.!
   
 18. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #18
  Dec 10, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Nahisi kama kichefuchefu!!
   
 19. Visible

  Visible Senior Member

  #19
  Dec 10, 2009
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 20. Einstein

  Einstein Senior Member

  #20
  Dec 10, 2009
  Joined: Dec 5, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi napinga kwenye point ya Kwanza, kusema kuna AMANI.. Amani si kutokuwepo na vita.. Huwezi ukasema kuna amani wakati watu wanalala njaa...

  There is NO peace in Tanzania... Kuna utulivu tu.
   
Loading...