CCM chama kinachopelekwa machinjioni na watu wake wenyewe!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM chama kinachopelekwa machinjioni na watu wake wenyewe!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anold, Nov 24, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Chama cha mapinduzi ni chama kikongwe ambacho kinaudhoefu mkubwa wa ndani na nje juu ya maswala ya siasa. Ni chama ambacho kina raslimali watu (wanachama) ambao wanaudhoefu mkubwa katika mambo ya kisiasa. Nimekuwa nikishangazwa na namna wanavyoshindwa kutambua matatizo muhimu ambayo pengine mtu yeyote mwenye akili timamu angefikiria kuwa ndiyo chanzo cha kufanya chama hiki kishuke hadhi yake kulinganisha na miaka iliyopita ambapo watanzania wengi walikiamini kipindukia!

  Chama cha Mapinduzi kama hakitaondoa uvivu na kufanya tathmini ya kina ya hali halisi ya kisiasa ndani ya chama na nje ya chama na kubaini matatizo ya msingi na kuachana na siasa za kuchafuana na kuharibiana sioni sababu za msingi za kufanya chama hiki kiepuke kufuata njia aliyokwenda KANU.

  Chama cha mapinduzi ninahakika bado hakijapata Daktari wa kugundua tatizo linalokisumbua, ndiyo maana sasa hivi hata kauli ya mpinzani mmoja tu inaweza kukinya chama kizima kiweweseke kiasi cha kuchanganyikiwa. Chama cha Mapinduzi huenda ni chama kizuri ila kina mlolongo wa viongozi na washauri ambao huenda sio wazuri, maana kama kingekuwa na washauri wazuri huenda wangeshabaini tatizo linalowasumbua kiasi cha kupingwa kila wanachokifanya. sasa hivi kinachoendelea ndani ya chama hivyo hakina tofauti na mtu "anayembembeleza ngombe wake anayempenda ili afike kwa urahisi machinjioni"
   
Loading...