CCM, chama kimoja karne ya 21 ni ndoto za mchana

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
CCM wanafanya juhudi kubwa kupita kiasi za kuhakikisha kuwa wanaendelea kuifisadi nchi katika mfumo wa chama kimoja. Kazi yao kubwa ni kuhakikisha kuwa wanadhoofisha vyama vya upinzani. Waliua TLP, wakaua NCCR mageuzi, wameua CUF, sasa wanainyemelea Chadema. Lakini wamechelewa sana, hakuna mtanzania wa karne ya 21 atakayekubali zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM. Ndio maana wabunge wa Chadema mwaka huu wameongezeka mara dufu, na wataendelea kuongozeka. Kizazi cha sasa kinataka Uhuru wa kufikiri na kuamua. Hivi, kuna watanzania ambao bado wanataka kuwekeza ubongo wao kwa CCM ili wawasaidie kufikiri na kuamua? CCM hawawezi kutawala fikra za kizazi cha sasa, chama kimoja karne ya 21 ni ndoto za mchana.
 
Back
Top Bottom