CCM Chagueni Vichwa Vya kuwawakilisha kwenye mijadala ya kitaifa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Chagueni Vichwa Vya kuwawakilisha kwenye mijadala ya kitaifa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbeu, Jan 23, 2011.

 1. Mbeu

  Mbeu Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ijumaa ya tarehe 21, msemo Chenua Achebe wa "In africa its not what you know but whom you" kwenye kipindi cha PIMA JOTO. kuna mwakilishi mmoja alikuwa anajikanyaga kanyaga ilivyo onekana alikuwa hajui au hatambui kuwa 'changes in tanzania is inevitable we need a new Katiba' Rais ameridhi na akaonyesha a way forward. likini yule jamaa alionyesha madhaifu makubwa ukweli ni kwamba hana KARAMA ya Kupambanua mambo. Next time tukiwa na vipindi kama hivi tafadhali CCM mtuletee watu wenye vipaji vya kupambanua mambo hatutaki watu wenye jazba, utazani alikuwa kwevye vita. naamini ndani ya CCM kuna watu wenye upeo mkubwa ndani ya chama hicho wenye uwezo mkubwa wa kupambanua mambo zaidi ya TAMBWE. Tunahitaji Men and women of substance, sio kwa sababu unamjua Bwana mkubwa ndo unapewa Post this is a wrong approach. ndo maana huyu jamaa Hana karama hiyo.
   
 2. s

  smz JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenena,

  haiwezekani tuna maswala nyeti kama Katiba unatuletea tambwe hiza, wa nini huyu?? Anasema ccm ilichaguliwa kwa sababu kwenye ilani yao swala la katiba mpya halimo, kwa hiyo watanzania hawataki katiba mpya- Tambwe Hiza leo asubuhu Star TV.

  tambwe hiza either ni mvivu wa kufikiri au hajui lolote, ila anaweza kuongea lolote
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mvivu wa kufikiri na hodari wa umbeya!
   
 4. F

  FENI Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtujuze elimu yake kwa anayefahamu
   
 5. M

  Mzalendoo Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kumbe wenzangu pia mlimuona! Huyu ccm kabla hawaja mtuma mtu wamuases kwanz manake TH alikuwa anabwabwaja tu ktk kpnd cha kipima joto.
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Huyu ni Bangusilo, watu makini wanaogopa kuharibu reputation zao kwani wanajua kuwa upepo unavumia wapi. Wanamtuma huyu STD VII ili hata kama akiharibu kina Makamba wamkosoe hadharani kuwa aliyoyasema si msimamo wa Chama na alitereza. Kinachowatafuna CCM ni utamaduni wa giza kuwa hutakiwi kusemea nje ya vikao vya chama, wanashindwa kujua kuwa katika Tanzania ya leo vyama is nothing mbele ya wananchi na kama wananchi hawajui serikali yao inawafanyia nini kwa sababu tu kuna genge la watu wanajinufaisha na mfumo wa Chama kushika hatamu basi chama hicho kijue kuwa hakina uhai endelevu.
   
 7. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Garbage in garbage out (GIGO). CCM wanatoa walichonacho.kama tunategemea mtu wa maana atoke CCM labda ni marehemu. Waliopo CCM sasa hivi ni Makamba na ndiyo akaonekana Tambwe ndiye nafuu.

  Mwenye akili hategemewi kuwepo CCM na kama yupo CCM basi ataona kuwa ni busara kukaa kimya kuliko kuongea upuuzi.
   
 8. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Swadakta, umenena mkuu. Jamaa ni kihiyo wa kutupa, yaani hajui lolote lile. Angekuwa mnyama ningemfananisha na nyumbu!
   
Loading...