CCM, CHADEMA, TLP, CUF kufanya mkutano wa hadhara wa pamoja wa Maridhiano Arusha

Kamanda Lema awepo maanake Magamba wenzangu nawafaham, lazima Watapotosha, ila Kuweni Makini sana na hawa CUF hasa MBATIA na huyo Mbunge wa Mkanyageni HABIBU MNYAA

Viongozi wote wa arusha mkoa na wilaya watahudhuria sanjari na.viongozi wote wa ccm mkoa na wilaya ya arusha mjini
 
Sijui kama ni rahisi kiasi hicho jambo kama hilo kutokea kwa Arusha hasa hao wauaji ccm wapande jukwaa moja na Chadema? Sijui... Lakini kwa cuf na tlp sioni ukakasi wowote kwakuwa tayari wanashirikiana katika maeneo mengine.

Mkuu mwita
Msajili wa vyama amethibitisha mkutano huu na ndie mwandaaji mkuu.
Anasema arusha sasa ni amani na watalii wengi wameukacha mkoa huu kwahiyo lengo la kuandaa mkutano huo ni pamoja na kurejesha imani kwa watalii kiwa sasa arusha ni salama na hakuna tena uhasama wa kisiasa.
Yule ----- mugesa mulongo nae amesema hata yeye amemaliza uhasama na lema na ni washkaji wanaweza hata kunywa pamoja na wote watahudhuria mkutano huo wa hadhara
 
Huu utakuwa ni upuuzi wa mwisho kutokea Arusha kwa chadema! Haijawahi kutokea nchi yoyote yenye demokrasia ya vyama vingi! Kama Mtungi anataka kuondoa tension iliyoko Arusha ni kuhakikisha haki inatendeka tu basi nothing else will help!

Hii ni mbinu ya maccm kutaka kuichafua chadema! Wanataka baada ya mkutano huo wazushe kuwa hata chadema nao wako kundi moja na ccm hivyo ni walewale! Chadema wasithubutu kuingia huu mkenge watajuta huko mbele! Wanapashwa kuwa wajanja kama nyoka ila wapole kama huwa maana zama hizi ni za uovu wa maccm at its peak!

Mtungi kazi yake kati hili ni kuhakikisha kuna level ground kwa vyama vyote lakini si kuviunganisha kuwa kitu kimoja hii ni kutumwa na ccm! Awaambie ccm warudishe umeya wa Arusha ili haki itendeke kwa uchaguzi halali! Na afanye hivyo na kule ilemela pia!

Chadema tafadhari kuweni makini kuliko kipindi kingine chochote!

Mkuu hofu na hoja yako ni ya msingi sana na inahitaji tafakuri ya kina
 
Maridhiano gani? Tunahitaji kusikia uchaguzi wa Meya umefanyika na vyama byote vimeshiriki kama ulivyo kuwa wa naubu meya na si vinginevyo,

Nadhani GODbles Lema anatakiwa aje huku kutupa ufafanuzi zaidi wa mkutano wao huu
 
Last edited by a moderator:
maana kuna mbili siku hizi kuna ya bwana Zitto na ya Mbowe .......msajili anapaswa kusema pia chadema zote zitakuwepo
 
Hii ni kwa mujibu wa Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Mutungi ambaye ametangaza kuwa vyama vyote vya siasa vitafanya mkutano wa hadhara mjini Arusha kwa ajili ya kuzika rasmi uhasama wa kisiasa mkoani humo.

Mkutano utafanyika katika uwanja wa sheigh Amri Abeid ambapo viongozi wa vyama wa mikoa ndio pekee watakaoruhusiwa kuvaa sare za vyama vyao.

source
 
Hii haikubaliki na meya feki akiwa bado anatanua madarakani. Huyo kiongozi wa CHADEMA Arusha atakayesimama jukwaani na Magamba itabidi atueleze hiyo damu ya wanawaarusha iliyomwagwa na hao CCM imelipwa vipi ilihali haki iliyokuwa inatafutwa haijapatikana.

Nimejiuliza maswali kidogo,1)Msajili huyu naye ashakua na bei ugambani?2)Suala la meya ni jambo dogo kiasi cha kulimaliza kwa kulifukia chini ya zulia??3)Bomu la Soweto nalo ni jambo dogo kiasi hiki cha kupata muafaka bila majibu ya kina yenye vina???"TANZANIA NI ZAIDI YA TUIJUAVYO".
 
Kwa mawazo yangu nadhani wale waliohusika na bomu la Arusha wakamatwe kwanza na kufunguliwa mashitaka ndio maridhiano yaendelee. Tofauti ya hapo ni uendawazimu na mazingaombwe ya mchana kweupe!
 
Upatanisho gani tena, na kwa nini ARUSHA tu..?
Au watu wanasaka umaarufu na cha kuzungumza (kwa wenzetu SERA)..??
 
Kwa mawazo yangu nadhani wale waliohusika na bomu la Arusha wakamatwe kwanza na kufunguliwa mashitaka ndio maridhiano yaendelee. Tofauti ya hapo ni uendawazimu na mazingaombwe ya mchana kweupe!
nakubaliana nawe mkuu
 
Back
Top Bottom