CCM, CHADEMA, CUF Na Udhaifu Wa Itikadi

Kwa hoja hii, sielewi kwanini haukubali hoja kwamba ACT ametibua Safari Ya UKAWA Ya matumaini Kwa kuamua kuitikia ccm.
Mkuu nimesema the main problem ni NEC, TISS na POLISI kwa UKAWA hivyo ujio wa ACT haupunguzi nguvu yoyote ya UKAWA maana hakuna safari hiyo. maadam wanagawana majimbo kusimamisha mgombea mmoja wa chama sio UKAWA, kila chama kusimamisha mgpombe wake upande wa pili sio UKAWA bali Upinzani kwa CCM.

Matokeo ya kura hazitahesabika za UKAWA bali za Chadema, CUF au NNCR hivyo ACT akichukua kura zozote zinakwenda upinzani ulogawanyika tu bado..Jambo ambalo kalisema Zitto ili muunganishe nguvu, mkasema haiwezekani wala hatakiwi kwa sababu ni msaliti kumbe wanataka kusimamisha vyama vyenu kama mwaka 2010 kwa kutumia karata ya UKAWA kugawana majimbo wakati ukweli ni kwamba vyama hivi hawakuungana.

Vyama vinavyounganisha nguvu kupanmbana na chama tawala hujisajili kama chama kimoja, wakagawa majimbo kwa jina la UKAWA japo ndani wakijua huyu Chadema, huyu CUF, huyu NCCR na kama kugawana ruzuku zitatokana na maridhiano ya pamoja kugawanya hizo ruzuku. Unashinda huku unapoteza huku, maadam lengo ni kukiondoa chama tawala nyote mnakuwa washindi. Wanachofanya UKAWA ni kiini macho tu kuwapumbaza wananchi na wamepumbazika na siasa za katiba Mpya ilihali kila chama ktasimama peke yake..Chadema itasiimama kama Chadema, CUF na NCCR ila wamegawana majimbo kwa jina la UKAWA.
 
Pamoja na ukweli kwamba vyama vingi vya siasa Tanzania vinaendeshwa kwa mujibu wa Katiba, Kanuni, na Taratibu, pia kuna ukweli kwamba vyama vyote vikubwa – CCM, Chadema na CUF, vina udhaifu mkubwa katika itikadi zao. Kama tutakavyobaini katika mjadala huu, itikadi ndio moyo wa chama ambao unasukuma damu katika viungo vingine vya chama kama vile katiba, kanuni, taratibu, mwongozo, sera na ilani. Mjadala huu utalenga zaidi kwenye vyama vikubwa vitatu vya siasa Tanzania: CCM, Chadema na CUF.
Ina maana gani kusema Idara za Itikadi, Siasa na Uenezi za CCM, Chadema na CUF zinapwaya?

1. Tanzania, tuna vyama visivyokuwa na itikadi inayoeleweka na ya vitendo. Mfano, CCM; CCM ilifanikiwa ki-itikadi chini ya mfumo wa chama kimoja kutokana, iliyolenga ukombozi wa nchi na Utaifa (chini ya TANU); baadae siasa ya Ujamaa na kujitegemea ililenga kumwinua mtanzania/mtanganyika. Lakini tangia kifo cha azimio la Arusha mwaka 1992, CCM imekuwa inahubiri itikadi ya Ujamaa, lakini upande mwingine, inatekeleza itikadi ya soko huru, tena bila ya mchujo. Ukosefu wa msimamo kiitikadi ndio tiketi ya Kifo kwa CCM, na wala sio Ufisadi. Tutalijadili hili kwa undani baadae.

2. Pia tuna vyama vilivyo jizolea umaarufu kutokana na sababu ambazo hazihusiani na UMMA kubaini ubora wa itikadi ya chama baada ya kufananisha na itikadi za chama/vyama vingine vilivyopo. Badala yake, umaarufu wa vyama hivi unatokana na UMMA kuvikubali kwa sababu nyingine nje kabisa ya ubora wa itikadi zao. Mfano mzuri ni umaarufu wa NCCR miaka ya 1990, na ule wa Chadema miaka ya 2000 – hadi sasa. Nimetumia neno ‘jizolea umaarufu’ badala ya ‘jipatia mafanikio’, Kwa sababu, tofauti na ‘mafanikio’ ambayo hutokana na itikadi, mara nyingi ‘umaarufu’ hutokana na vitu vya mpito, na huwa haudumu kwa muda mrefu. Wengi tunakumbuka umaarufu NCCR miaka ya 1990; umaarufu wa Chadema hauna tofauti kubwa sana kwa sababu mafanikio tunayoyaona hayatokani na ubora wake wa itikadi, bali kwa vitu vya msimu tu, ambavyo vinaweza meguka kirahisi. Hili pia tutalijadili zaidi baadae.

3. Lakini pia, Tanzania tuna vyama vilivyopata mafanikio kisiasa (sio umaarufu) kutokana na itikadi zao. Lakini vyama hivi vina udhaifu mmoja mkubwa juu ya itikadi zao: Itikadi hizi zinaendana na hali halisi ya upande mmoja tu wa jamii badala ya jamii nzima. Mfano, CUF na mafanikio yake visiwani ambayo imekuwa vigumu kuyarudia Bara. Tutalitazama hili pia baadae lakini kwa sasa ni muhimu tu kusema kwamba - mafanikio ya sasa ya CUF visiwani hayana tofauti kubwa na mafanikio ya TANU bara miaka 1960. Kama ilivyokuwa TANU miaka ya 1960, mafanikio ya CUF yanatokana na itikadi inayolenga Utaifa /Ukombozi dhidi ya Utawala wa Bara. Pamoja na mafanikio yake visiwani, itikadi ya CUF haina mashiko upande wa bara, na pia haitachukua miaka mingi kabla ya itikadi hii kuishiwa makali hata Zanzibar. Kama ilivyokuwa kwa CCM, CUF nayo itapitia hatua tatu za maisha: (1) Itikadi ya uhuru na Utaifa iliyozaa matunda hadi sasa (2) baada ya utaifa kupatikana, CUF itakumbwa na changamoto za kutekeleza ahadi ilizozitoa wakati wa mapambano ya kudai utaifa kutoka Bara. Hali itazidi kuwa ngumu zaidi iwapo patatokea vyama vingine vya upinzani upande wa Zanzibar (3) Iwapo vitajitokeza vyama vipya vyenye nguvu Zanzibar, itikadi ya CUF itazidi kuishiwa makali kwa kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi za ukombozi (kama ilivyotokea kwa CCM), na vyama vitabaki kukosoana huku CUF ikionekana sio lolote/dhaifu, huku vyama vya upinzani Zanzibar vikisahau kabisa kwamba adui yao ni mmoja – wawakilishi wa mataifa tajiri yani - WorldBank na IMF.Hili pia tutalijadili baadae.
Udhaifu huu wa ki-itikadi ndani ya vyama vya siasa unawakosesha wananchi fursa ya kuunda muono na mtazamo wa kisiasa unaofuatana na imani (za kiitikadi) zinazotambulika, na nyepesi kueleweka au kutofautisha. Hii ndio sababu kubwa kwanini inakuwa rahisi kwa wananchi kuunga mkono vyama kishabiki zaidi kuliko kutokana na kushiba imani za vyama. Ndio maana, tofauti na nchi zilizokomaa kisiasa, kwa Tanzania, suala la wanachama kuhama hama vyama ni suala la kawaida. Vilevile kwa upande wa viongozi wa vyama, ni jambo la kawaida kuwasikia wanasiasa wa chama kimoja wakitetea wanasiasa wa vyama vingine hata kama wamepewa adhabu kwa kwenda kinyume na katiba na kanuni za vyama vyao (mfano Zitto kuwatetea kafulila na Hamad). Kama Chadema ingekuwa inaendesha siasa za ki-itikadi, jambo hili lisingetokea kwani itikadi ya Chadema na ile ya CUF ni tofauti kabisa. Katika demokrasia iliyokomaa na yenye kuendeshwa ki-itikadi, kitendo cha wanasiasa kuteteana kwa sababu binafsi, au wanasiasa kuhama hama vyama, ni kitendo cha kujimaliza kisiasa. Ni katika nchi kama Tanzania pekee ambapo leo mwanasiasa anaweza jitoa CHADEMA, CCM, au NCCR na kwenda chama kingine bila ya hofu yoyote. Hiki ni moja ya vielelezo vikubwa juu ya udhaifu wa vyama vyetu ki- itikadi. Katika mazingira ya kawaida, kitendo cha kiongozi kuhama chama ni sawa na kukana imani (itikadi) yake na kukumbatia imani (itikadi) nyingine. Kwa mwanachama kufanya hivi sio jambo la hatari sana, lakini ni la hatari sana kwa viongozi.

Ni mapungufu haya ya ki-itikadi ndiyo hupelekea vyama vyetu kunadi ilani na sera zinazofanana, badala ya kuwa na ushindani mkali wa mtazamo unaotokana na itikadi. Katika siasa za sasa, vyama vyote vinashindana kwenda Ikulu, sio kuleta jambo jipya linalotokana na itikadi zao, bali kutekeleza sera zile zile za soko huria zilizojaa uholela, za WorldBank na IMF, kwa kasi na ufanisi zaidi. Vyama pia vinapoteza muda mwingi sana kushindania yasiyo na umuhimu sana yakiwa yametapakaa (not coherent), kama vile haki za raia, utawala wa sheria, na vita dhidi ya ufisadi. Siasa juu ya masuala haya zimekosa uthabiti (consistency) na kuungamana (coherence) kutokana na udhaifu wa ki-itikadi. Vile vile, kutokana na udhaifu wa ki-itikadi, umaarufu wa vyama mara nyingi (kama sio mara zote), unatokana zaidi na hulka (personalities) za viongozi waliopo katika vyama hivyo, hasa nguvu zao katika jamii wanazotoka, bila ya kujali vyama wanavyotoka au itikadi wanazoziamini.

Mapungufu ya ki-itikadi yanapelekea vyama kushiriki katika ushindani wa siasa kama vile ni soko la kushindana ubora wa bidhaa. Vyama vinajikita zaidi katika ushindani wa nani ana bidhaa bora zaidi (sera na ilani), kuliko mwenzake, bila ya uwiano na itikadi zao. Vyama vinajali zaidi kuja na bidhaa zinazoendana na mahitaji ya soko kwa wakati huo. Idara za uenezi, siasa na itikadi hazijishughulishi kuzunguka nchi nzima kujenga chama na kusambaza imani (itikadi) zao ili kushawishi wananchi kuwa wafuasi wa kudumu, na pia wawe wapiganaji wa kutetea na kulinda itikadi zao katika maeneo wanayoishi. Nguvu ya chama cha siasa ipo kwenye matawi na mashina, huko ndiko watu wengi wanaishi. Lakini cha ajabu ni kwamba, Idara za itikadi, siasa na uenezi, zinatumia muda mwingi kwenye Redio, TV na magazeti kama vile nguvu ya chama ndio zipo huko. Huwa wanakumbuka umuhimu wa matawi na mashina wakati wa uchaguzi tu. Nia ya Mwalimu Nyerere miaka ya 1960, ya kumwachia Kawawa uongozi wa nchi kwa muda na yeye kwenda vijijini ilikuwa ni kujenga chama akisaidiwa na idara ya itikadi na uenezi ya TANU. Aliporudia zoezi hili wakati anawaaga watanzania miaka ya mwisho ya 1990, alielezea kushtushwa kwake na jinsi gani imani ya chama ilivyokuwa ikishuka, kutokana na chama kuzembea kusambaza itikadi kwenye maeneo yanayostahili.

Kwa Tanzania ya leo, udhaifu huu ndio unaozaa UMMA usiokuwa na msimamo wa kudumu wa kisiasa, na wengine wengi kutoona umuhimu wa kushiriki katika siasa. Wananchi wengi wamechoka na vyama vya siasa, kwani havitekelezi yanayohubiriwa. Isitoshe, mara nyingi, kauli na vitendo vya vyama vilivyopo hupishana, mfano suala la posho za wabunge n.k. Idara za uenezi, siasa na itikadi zimeshindwa kufanya kazi zake kwa ukamilifu, idara hizi mara nyingi uendesha siasa za leo kupinga hili, kesho kuunga mkono lile, ili mradi tu “kujiepusha wasipitwe na masuala ya kupita”. Suala la idara hizi kuja na pre – emptive strategies halipo, na badala yake ni pro-active strategies. Hiki ni kikwazo kikubwa sana kwa ustawi endelevu wa vyama vyetu vya siasa, na demokrasia kwa ujumla.

Umuhimu wa Itikadi ya Chama
Kama moyo ulivyokuwa na umuhimu kwa uhai wa binadamu, itikadi ni moyo wa chama cha siasa. Moyo wa chama (itikadi) ndio husukuma damu ili kuviwezesha viungo vingine vya chama (katiba, kanuni, taratibu, mwongozo, ilani na sera), vifanye kazi zake kwa uhakika na ukamilifu. Itikadi utengeneza mtazamo, msimamo, malengo na matarajio kuhusu masuala mbali mbali yanayozunguka maisha ya jamii. Na mitazamo, misimamo, malengo na matarajio haya uhathiri matendo na shughuli za kisiasa ndani ya jamii husika. Wananchi hutegema sana itikadi kama moja ya njia zao kuu za kuwasaidia kuelewa masuala mbalimbali ya kiulimwengu, kwani iItikadi hutoa mwongozo na kusaidia uwepo wa misingi ya kuratibu jinsi gani jamii iendeshe masuala yake ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, katika hali ya ufanisi, nidhamu na utulivu.

Katika dunia ya leo, Itikadi zimegawanyika katika makundi makubwa sita kama ifuatavyo:

1. Ukomunisti
2. Ujamaa
3. Ujamaa wa kidemokrasia/Deocratic Socialism/Social Democrats
4. Uliberali/Liberal
5. Conservative Liberals/mchanganyiko wa uhafidhiana na uliberali
6. Uhafidhiana/Conservative

Mpangilio huu wa itikadi hutokea kushoto kuelekea kulia (as a continuum) kama ifuatavyo:

Communism=>Socialism=>Ujamaa wa Kidemokrasia=>Liberals=>Conservative Liberals=>Conservative

Kwahiyo kwa mfano, itikadi ya kikomunist, na kijamaa zinatambulika kama itikadi za mrengo wa kushoto (leftist), wakati itikadi ya uhafidhiana (conservatism) inatambulika kama itikadi ya mrengo wa kulia (rightists). Katika miaka ya hivi karibuni, itikadi hizi kuu zimezaa itikadi nyingine tatu kubwa ambazo ni: (1) Centre/kati; (2) kati-kulia (centre-right); na (3) kati-kushoto (centre-left); Nitazijadili kwa undani baadae. Vinginevyo, kwa ujumla wake, ukomunisti, Ujamaa na Ujamaa wa kidemokrasia/democratic socialism zinazotambulika kama itikadi za mrengo wa kushoto, wakati uliberali, conservative liberals na conservative hujulikana kama itikadi za mrengo ya kulia.
Tuzitazame itikadi hizi sita kubwa kwa undani, ili tuzidi elewa itikadi za vyama vya CCM, Chadema na CUF kwa undani zaidi. Ili kurahisisha zoezi hili, nitazigawanya itikadi hizi sita katika makundi makubwa mawili - kundi la kwanza ni lile la itikadi zote za mrengo wa kushoto yani ukomunisti, Ujamaa na Ujamaa wa kidemokrasia/social democrats; Na kundi la pili ni itikadi zote za mrengo wa kulia, yani uliberali, conservative liberals na conservatives. Tuanze na itikadi za mrengo wa kushoto – Ukomunisti, Ujamaa, na Ujamaa wa Kidemokrasia, kwa kufuatana na mpangilio tuliokwisha uona ambao ni:

Ukomunisti>Ujamaa=>Ujamaa-wa-Kidemokrasia=>Uliberali=>Conservative Liberals=>Uhafidhiana

Itikadi za mrengo wa kushoto (Ukomunisti, Ujamaa na Ujamaa wa kidemokrasia), asili yake ni Karl Max ambae alidai kwamba Ubepari muundo wa kinyonyaji na kikandamizaji. Wengi wetu tayari tunalielew vizuri suala hili.


UKOMUNISTI
UJAMAA
UJAMAA WA KIDEMOKRSIA
UTAWALA
Mamlaka yote ipo chini ya umma; kuna mwafaka katika jamii kuhusu michakato wa maamuzi mbalimbali.
Masuala ya umma yanaendeshwa kwa “power structure” iliyopo chini ya muundo wa halmashauri, kuanzia ngazi ya chini mpaka taifa.
Masuala ya umma yanaendeshwa na viongozi waliochaguliwa kupitia muundo wa kidemokrasia.
CHAGUZI
Hakuna chaguzi kwani serikali ya kikomunisti inakubalika na wote.
Ingawa mara nyingi huwa na chama kimoja cha siasa, huwa kunakuwepo na chaguzi za mara kwa mara, hivyo viongozi kuanzia ngazi ya halmashauri mpaka juu hutokana na watu.
Viongozi wa umma hutokana na chaguzi za mara kwa mara zenye uwazi na uhuru kwa wapiga kura;
SERIKALI
Maisha yote ya jamii, kuanzia utawala, uchumi na maisha binafsi, yapo chini ya serikali.
Kuna za makusudi za kuunganisha serikali na jamii nzima.
Serikali thabiti huitajika ili kuendesha mipango na sera za kugawanya keki ya taifa.
UCHUMI
Hakuna soko wala ubadilishanaji (exchange) wa aina yoyote; hakuna umiliki binafsi wa mali; bidhaa na huduma zote zinagawanywa sawa katika jamii bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Uwepo wa mishahara isiyotofautiana sana; Pia huduma na bidhaa nyingi kwa umma hutolewa na serikali.
Ubepari unakubalika, na unashamiri kupitia muundo thabiti wa kugawana keki ya taifa na upatikanaji wa huduma bora za kijamii.
KAZI/AJIRA
Hakuna matabaka ya aina yoyote miongozi mwa wafanyakazi.
Kuna muungano wa tabaka la wafanyakazi; uwepo wa fursa sawa kwa watu wote bila kujali matabaka.
Kuna umoja wa kitabaka miongozi mwa wafanyakazi kupitia taasisi zinazounganisha tabaka hili.
MAPINDUZI
Kuna mapinduzi yanayolenga kufuta uhaba (scarcity) na pia umiliki binafsi wa mali.
Kuna mapinduzi ya kuangamiza ubwanyenye.
Mapinduzi hayahitajiki kwani ubepari unakubalika hivyo kuendelea kushamiri.
PROGRAMU ZA KIJAMII
Wananchi hupatiwa huduma zote za msingi na serikali bure, kwa mfano elimu, afya, n.k.
Umiliki wa umma wa njia kuu za uchumi, na matumizi ya rasilimali ya taifa kwa manufaa ya umma pamoja na upatikanaji wa huduma zote za msingi kwa watu wote.
Msisitizo mkubwa ni uwepo wa a “Welfare State”, yenye Social security programs zinazolenga kutoa msaada kwa wote wanaostahili - kama vile huduma ya afya, elimu, makazi, n.k; Pia serikali hugawanya mapato (redistribute income) kwa kutoza kodi za aina mbali mbali kwa lengo la kupunguza tofauti za kiuchumi baina ya matabaka mbalimbali, huku pia ikiweka kinga thabiti kwa watu wasio na ajira, wagonjwa, na wastaafu.


Na sasa tuziangalie itikadi za mrengo wa kulia –Uliberali, Liberal Conservatives, na Conservativesm/uhafidhiana.

1. Uliberali
Asili ya itikadi hii ilikuwa ni kupigania haki za watu katika jamii za mataifa ya magharibi yaliyokuwa chini ya tawala za kifalme; tawala hizi hazikutoa haki na fursa sawa za kiuchumi kisiasa na kijamii kwa wananchi. John Locke ndiye (mwanzilishi), na wenzake walidai kwamba – binadamu huru ndio msingi wa jamii imara yenye amani na utulivu; pia walihimiza umuhimu wa kuwepo kwa serikali yenye wajibu wa kulinda haki za msingi za wananchi; harakati hizi ndiyo zilizokuja kuzaa dhana nzima ya demokrasia ya uwakilishi (representative democracy); Baadae harakati hizi ziilichochea kuzaliwa kwa uliberali katika eneo la uchumi, muasisi wake akiwa Adam Smith, ambae alihimiza umuhimu wa serikali kutoingilia shughuli za kiuchumi, kwa mtazamo kwamba, serikali ikiachia shughuli za uchumi zijiendeshe na kujisahisha zenyewe itapelekea ufanisi zaidi katika uchumi. Katika dunia ya leo, Itikadi hii bado ina nguvu kubwa. Kuna jamii nyingi duniani zinazo himiza umuhimu wa serikali kutojiingiza katika shughuli za kiuchumi na kijamii, kwa mfano, serikali kukaa mbali na na utoaji wa huduma za kijamii – afya, elimu n.k; na pia serikali kutoshiriki katika uchumi kupitia mashirika ya umma, na badala yake, mashirika binafsi pekee ndiyo yatawale shughuli za kiuchumi.

2. Conservative Liberals
Itikadi hii ni mchanganyiko wa mawazo, sera na imani za uliberali (liberalism) na uhafidhiana (conservatism). Itikadi hii inaunga mkono ulegezaji wa masharti mbalimbali ya kiuchumi na utandawazi (globalization), Pia inaunga mkono sera kali zinazozuia uhamiaji (strict immigration policies). Kiuchumi – itikadi hii inaunga mkono uwepo wa uhuru wa kiuchumi miongoni mwa wananchi, hasa kuwapatia wananchi uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe. Itikadi hii haijihusishi sana na masuala ya kijamii lakini kila inapobidi kufanya hivyo, huwa na msimamo wa kijamii ulio sawa na ule wa kiliberali (rejea mjadala wa uliberali hapo juu).

3. Conservatives/wahafidhiana
Asili ya itikadi hii ni harakati za kupinga mapinduzi ya kumwondoa mfalme wa Ufaransa katika karne ya kumi na nane. To conserve maana yake ni ‘kuhifadhi’, hivyo conservatives hawaamini katika mabadiliko au uharibifu wa desturi/utamaduni. Edward Burke ni muasisi wa itikadi hii; yeye alipinga mapinduzi ya kumwondoa mfalme wa ufaransa kwa mtazamo kwamba kitendo hicho kitaharibu desturi, imani na taasisi zilizojengwa kwenye jamii kwa muda mrefu ambazo ni muhimu katika maisha ya watu. Katika siasa za leo, wahafidhiana wanapinga ushiriki wa serikali katika uchumi kwa madai kwamba, umaskini ndani ya jamii ni matokeo ya serikali kuingilia maisha ya wananchi kwani kitendo hiki hulea watu wavivu, na kuua dhana ya uchapa kazi na uwajibikaji katika jamii. Badala yake, wahafidhiana wanahimiza kila mtu kujipatia riziki yake kwa jasho lake, na sio kusubiri serikali kupitia huduma za kijamii, social security, n.k. wahafidhiana pia wanapinga uwepo wa mashirika ya umma katika uchumi, na badala yake wanahimiza uchumi uendeshwe na mashirika binafsi.

Kama tulivyoona awali, itikadi hizi sita zkubwa baadae zilizaa itikadi nyingine tatu: Centre/kati; kati-kulia (centre-right); na kati-kushoto (centre-left). Tuzitazame na hizi:

Ukomunisti>Ujamaa=>Ujamaa-wa-Kidemokrasia=>Uliberali=>Conservative Liberals=>Uhafidhiana

1. Itikadi ya Mrengo wa Kati (Centre) – Huu ni mrengo kati ya Uliberali na Ujamaa wa kidemokrasia. Chadema inatamka hii kama itikadi yake kama chama. Kwa kawaida, Itikadi ya mrengo wa kati (centre) inaamini na kuunga mkono mambo makuu yafuatayo:
· Ongezeko la kodi linaloenda sambamba na ongezeko la vipato vitokanavyo na shughuli za uchumi (progressive taxation); Umiliki binafsi wa mali; Uhuru na haki ya wananchi mbele ya sheria; Uliberali wa kiuchumi na uliberali wa kijamii.

Uliberali wa kiuchumi kwa maana ipi:
· Kuwapatia wananchi uhuru wa kujiendeshea shughuli zao bila ya kuingiliwa na serikali; Umiliki wa mali binafsi; Serikali kuratibu/rekebisha (regulate) uchumi, lakini wanapinga serikali kukwaza uhuru wa biashara na ushindani katika soko; wanaunga mkono sera za serikali za kuondoa ukiritimba binafsi (private competition) kwa imani kwamba ukiritimba huu unaumiza wananchi maskini;

Uliberali wa jamii kwa maana ipi?
· Haki ya kijamii na uhuru kwa watu wote; Wajibu wa serikali kuinua hali za maisha ya wananchi kwa njia kama vile – ajira, afya, elimu, huku haki za wananchi zikizidi kuimarishwa.

2. Mrengo wa Kati - Kulia (centre-right) – huu ni mrengo uliopo katikati ya Uliberali na Conservative Liberals.
· Kwa ujumla, itikadi hii inaunga mkono kanuni nyingi za soko huru; lakini vilevile inapinga serikali kujiingiza kupita kiasi kwenye shughuli za kiuchumi (kupitia mashirika ya umma); inapinga serikali kujingiza kupita kiasi kwenye utoaji wa huduma za kijamii (kama vile afya na elimu); na inaunga mkono umiliki wa mali binafsi;

3. Mrengo wa Kati – Kushoto – huu ni mrengo uliopo kati ya Ujamaa wa Kidemokrasia na Ujamaa.

Mrengo huu unaamini katika yafuatayo:

· Jamii endelevu na serikali endelevu; Uliberali wa kijamii (rejea hapo juu), na siasa za kijani (green politics); pia ina amini katika mchanganyiko wa sekta ya umma na sekta binafsi kuendesha huduma za kijamii kama vile elimu, afya n.k; Uwepo wa social security ya kutosha kwa wananchi wanaostahili tu (sio katika kiwango cha Ujamaa na Ukomunisti) ili kupunguza kasi ya umaskini na kulinda ‘vipato’ vya wananchi wanaioshi katika mazingira ya uzee (wastaafu), wagonjwa, walemavu na wasio na ajira; mrengo huu pia una amini katika haki na fursa sawa kwa wote; inaunga mkono uwepo na umuhimu wa taasisi za serikali zinazoratibu sekta binafsi kwa nia ya kutetea wafanyakazi na walaji (consumers), kwa kuhakikisha uwepo wa vyama vya imara vya wafanyakazi, na pia ushindani wa haki (fair competition) katika soko; pia wanaunga mkono ongezeko la kodi linaloenda sambamba na ongezeko la vipato katika uchumi, lengo kuu likiwa kukusanya kodi ya kutosha ili isaidie kutoa huduma muhimu za kijamii kwa wale wanaostahili.

Kwa leo naomba niishie hapa ili kupunguza urefu wa uzi huu ambao tayari umepitiliza. Ila ningependa kumalizia kwa kusema kwamba - ni muhimu kwa vyama vyetu vya siasa kuamka na kuchagua itikadi zilizokuwa ‘relevant’ na mazingira ya nchi na kuondokana na siasa za kubahatisha. Siaza za ki-itikadi zitavipatia vyama vyetu vya siasa mafanikio ya kudumu, na maisha marefu, badala ya umaarufu wa muda mfupi kama ule uliotokea kwenye chama cha NCCR, mzimu ambao pia unaviwinda vyama vya Chadema na CUF hivi sasa, huku CCM ikiwa imeshafikia katika hatua ya mwisho kabisa ya maisha yake. Ni muhimu wananchi kushiba itikadi za vyama. Ni muhimu kuanza kuwavutia wananchi kwa sababu nje ya personalities za viongozi wa vyama, au kelele za ufisadi ambazo hazina mashiko ya ki-tikadi. Pa ni muhimu nitamke kwamba kwa hali ya sasa ya udhaifu ki-itikadi ndani ya vyama vyetu vikubwa, sio CCM, CHADEMA, CUF, au NCCR, ambavyo vina majibu ya kumnyanyua mtanzania kutoka katika umaskini. Kinachoendelea sana sana ni mbio za vyama hivi kukimbilia Ikulu ili kuwa watekelezaji wazuri zaidi kuliko wenzao, wa sera za soko holela zinazolazimishwa kwetu na WorldBank na IMF.

Lakini vyama vya siasa Tanzania bado vina nafasi nzuri ya kurekebisha mapungufu yote haya. Kwa CCM ambayo ndio chama tawala, ni lazima sasa itambue kwamba Ujamaa wa Marxist – Lenin ulishaanguka zaidi ya miaka 20 iliyopita, lakini haina maana kwamba Ujamaa umefeli. Ujamaa wa Kidemokrasia kama ule uliopo katika nchi za Sweden na nyinginezo ndio njia sahihi ya CCM kuifuata ki-itikadi. Nje ya kufanya haya, CCM haina mbadala mwingine zaidi ya KUFA, kwani kitaendelea kushindana na vyama kama Chadema katika sera zile zile, tofauti kubwa ikiwa, mmoja yupo madarakani, mwingine ni mpinzania. Kwa Chadema na CUF, ingawa wana declare itikadi zao kuwa ni mrengo wa kati (Chadema) na Uliberali (CUF), vyama hivi bado vina mapungufu makubwa ki-itikadi, ambazo nitazijadili siku ningine. Poleni na pia samahanini kwa uzi mdefu.

Mungu akubariki sana, asante kwa uchambuzi mzuri. ......
 
Nimeona nililete hili varangati hapa kwa sababu watu wengi wanashabikia vyama vya kisiasa bila kujua vinasimamia nini.

Naomba kwa wale wanaojua POLITICAL ECONOMY waanze kuchangia hapa. Kama wewe hujui maana ya political economy naomba usubiri kuelimishwa kabla hujatupia matusi na mihemuko yako.

Ninaileta hii mada kwa sababu Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CDM, walikuwa wamepanda chati kabla ya 2015 kupita ajenda yao ya kutokomeza UFISADI. Leo, kwa sababu CCM inafanya kazi nzuri kukabili ufisadi, inaonekana wanafulia na hawana kete nyingine za kuikabili CCM. Hii si kweli. Kuna tofauti kubwa za kiitikadi kati ya CCM na vyama pinzani.

Nitazieleza kwa kifupi tofauti hizi ili kuanzisha mjadala.

Sasa tuanze.

Itikadi ya CCM.
Hiki chama kimejieleza kuwa kitafuata itikadi za KIJAMAA (social democratic). Hii ina maana gani?

Ina maana kuwa uzalishaji utaendelea katika misingi ya ushindani (capitalistic mode of production) lakini uchumi wa nchi utapangwa na serikali, na mafao yatakayotokana na mapato ya nchi yatagawiwa kulingana na mahitaji ya nchi (equitable distribution of national wealth to all citizens)

Hii kwa ufupi ndio itikadi ya CCM. Ninaweza kuwa nimekosea mengi. Naomba masahihisho.

Itikadi ya CDM
CDM wanajinadi kuwa ni chama cha KIBEPARI.

Hii ina maana uchumi utaendeshwa kufuatia uzalishaji wa kibepari (capitalistic mode of production), na mgao wa mapato kufuatia misingi ya kibepari (capitalistic distribution of national resources).

Mfano mdogo, ardhi yote itabidi iuzwe kwa anaeweza kuinunua. Serikali haitakuwa mmiliki wa ardhi tena, mabepari wenye uwezo watanunua ardhi yote na masikini watabaki vibarua katika ardhi ya nchi yao.

Kama nimekosea naomba masahihisho.

Itikadi ya ACT-Wazalendo
Katika zama hizi za nchi kama CHINA kuipiku MAREKANI kiuchumi, naona itikadi ya ACT kuwa sio tofauti sana na ya CCM.

Itikadi ya CUF
Niseme ukweli tu wandugu. Siijui.

*******************************
Naomba tujadili kwa nini CCM watolewe madarakani na kuwaweka CDM?

Au CUF.
Au ACT-Wazalendo.

Karibuni.
 
wote walewale tunataka tubadilishe tu mwingine naye ale sio toka uhuru yuleyule
 
Ccm inahubiri ujamaa ila matendo yake nafikiri hayapo kijamaa.

Serekali inabebwa na huu mfumo wa welfare economy ila ccm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom