CCM, CHADEMA, CUF na NCCRr-Mageuzi....someni hapa, ni dawa ni kinga pia. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM, CHADEMA, CUF na NCCRr-Mageuzi....someni hapa, ni dawa ni kinga pia.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyakarungu, Sep 15, 2012.

 1. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  CCM :-chadema wachochezi na wahamasishaji wa vurugu,wakabila na wadini.
  Chadema :- tumefika hapa kwenye hali ngumu ya maisha kwa sababu ya ccm.
  Cuf :- Chadema ndio ccm B kwa sababu wanapokea pesa za kada wa ccm sabodo kwa hiyo wanatunzwa na pesa chafu wanazozikemea kila siku.
  Nccr Mageuzi :- ccm, chadema na cuf wote hawafai tupeni nchi muone, hahaaaa

  QUENSEQ...
  TUMEJIKUTA TUNAPOKEA NA KUZOEA AINA HII YA HOTUBA, KILA TUSIMAMAPO TWAKOSOA BILA KUWEKA NJIA ZA SULUHU, WASIKILIZE WANASIASA MAJUKWANI UTAGUNDUA WANATAKA WACHAGULIWE KWA UMAHILI WAO WA KUKEMEA (UPINZANI) AU KULALAMIKA (CHAMA TAWALA)

  CRITICISM

  CHAMA TAWALA..wapinzani wanapotumia udhaifu wako kujiimarisha wewe shugghulika na utekelezaji wa sera zako na ujibu mapigo kwa utendaji na uwajibikaji sio kujitokeza kujibu hoja kinadharia tu.
  WAPINZANI.. CCM inapozorota kwenye utendaji wake wapinzani tumieni fursa hiyo kuikosoa na serikali yake, ukosoaji usiishie kutaja hasara tu zinazosababishwa na uongozi mbovu bali uendane na utoaji njia mbadala za utatuzi, Mfano, wewe kijana ukosoae sana kuhusu elimu taja njia mbadala za kuboresha mfumo huu wa elimu, namna gani utaendana na mahitaji ili ukidhi ushindani wa sasa, uwiano wa watumishi wa elimu na wingi wa shule, useme nini suluhu(r/l) na sio kuzikosoa shule za kata tu, ukumbuke kuna wazazi wanaoona zile shule ni mwokozi kwao, kwa hiyo ukikosoa tu bila kueleza njia mbadala utaambulia kupigiwa makofi ya shangwe kwa sauti yako kali na pengine ya hasira, lakini maneno yako hayatadumu mioyoni mwao (TUJIFUNZE),
  Wewe uwezae kukosoa kuhusu uchumi, hebu jikite kuelezea watu waelewe unaongelea kitu gani, ueleze njia sahihi na zinazowezekana kutatua tatizo la hali ngumu ya maisha, jikite japo kwenye ardhi useme namna gani ardhi pekee inaweza kuwa mkombzi, tena ijikite kwenye kilimo tu ukiachilia mbali madini na misitu, usemee kilimo tu hata nacho uchague mazao 5 tu na uayagawe katka makundi mawili, mazao matatu yakidhi kiwango cha kuuzwa kimataifa kwa ubora mkubwa na wamanufaana makubwa uelezee namna gani utamudu kushawishi dunia kuhusu ubora wa mazao yako na yauzike kwa bei ya kutosha, mazao mengime mawili yaboreshwe yakidhi soko la ndani na mipaka ya EA yawe kwenye demand ya hali juu sana, ifikie hatua wafanya biashara wafanye trade off ya mazao mengine na wafanye opportunit cost ya mazao haya, hebu eleza mbinu utakazotumia utaona utakavyowaingia watu mioyoni na ukadumu, kadhalika unaeweza kusemea miundombinu ueleze namna utakavyomudu kujenga reli eleza mbinu kwa kukosoa yaliyopo, NADHANI HUU NI MTIHANI AMABAO WENGI WETU MPAKA MSIMAMIZI ANASEMA PENS DOWN...HATA NUSU JIBU NI SHIDA, NILIDHANI TUJIFUNZE KUPITIA UWASILISHWAJI WA BADGET BUNGENI, TUNAONA NAMNA MAWAZIRI NA VIVULI VYAO WANAVYOFANYA ARGUMENTS..HATA KWENYE INTERPELLATION MARA NYINGI HUPENDEZA NAPOMUONA MTU AKIHOJI KWA KUTOA USHAURI, KUWA MH. SPIKA KWANINI SERIKALI ISITUMIE ......KUFANYA...., NA SIO KWANINI SERIKALI IMELALA TU NA MPAKA SASA SIONI MAJI NA UMEME JIMBONI KWANGU? TEH TEH...(TUJIFUNZE
  , NI DAWA KWA AFYA YA UPINZANI ILA NI KINGA KWA CHAMA TAWALA
   
Loading...