CCM, CCM, CCM, Shika Hatamu! Why Not?

Mdau

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,789
470
Mabadiliko huletwa na kikundi cha watu wachache wenye mtizamo tofauti na wenye uwezo wa kubadilisha fikra za jamii.....I salute JF members (ingawa sio wote) kwamba wana mawazo`bora sana kwa jamii ya Watanzania........LAKINI, mbona tumejazana humu tukibadilishana mawazo kama kikao cha walevi bar?? Hivi ni watanzania wangapi wanafahamu mchakato wa yanayojadiliwa humu? MwanaHalisi wakiacha kuchapisha maoni kadhaa ya Mzee Mwanakijiji, hivi ni watanzania wangapi watapata japo kidogo toka humu??? Hebu tujaribu kubadilisha approach wajameni, JF ipo kwa wachache wenye huduma za internet, especially za bure maofisini, sasa basi,tuchekeche bongo zetu, tujue namna pana zaidi ya` kusaidia Wadanganyika......otherwise, CCM itaendelea kushika hatamu, wenyewe mmeona WALIOKUWA wanajiita WAPIGANAJI WA UFISADI>>>kwishneri habari yao!!! Ni maoni tu wadau.......
 
Kulikuwa na kile kijarida cha Cheche za fikra....Siku hizi hakitoki tena!Haya mapambano ni magumu mno.Haya magazeti yanaishia kusomwa sehemu za mijini tu,huko bush ni ngumu kulipata gazeti.Radio na mikutano ya hadhara inasaidia sana kuamsha wananchi wa maeneo mengi.No wonder viongozi wa upinzani wanapigana vikumbo pale maelezo ili kuongea na waandishi wa habari.
 
CCM sasa inashika hatamu,na hakuna sababu yoyote kwa nini isiendelee kushika hatamu. Mimi nawapinga wale wanaosema kwamba tatizo la Tanzania ni kwamba hakuna Chama cha upinzani chenye nguvu. Tanzania HAIHITAJI uwepo Upinzani.
Lakini kama wapo Wapinzani ambao wanaweza kuunda Serikali nzuri kuliko hii ya CCM,yaani Wapinzani wanaoweza kuja na Ajenda nzuri,platform nzuri ya Uchaguzi,msingi mzuri wa sera zao,hakuna sababu yoyote kwa nini wasichaguliwe kuiongoza Nchi.. Tanzania HAIHITAJI CCM..
 
Paomja na mabo mengine mijadala ni muhimu hivyo JF lazima iwepo.Mpaka leo hujajua tu mbinu mbadala?pole yako.
 
Huwezi badirisha watu kwa maneno tu. Unatakiwa kufanya matendo.
Mtu akikuita weye ni kichaa hutakiwi kujibizana ama kupoteza mda mwingi kujieleza jinsi gani we si kichaa. Bali unatakiwa kuonyesha jamii kwa matendo kwamba weye si kichaa.
 
Back
Top Bottom