VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Katika hali iliyotarajiwa, CCM imewaagiza Wabunge wake wafanye kila wawezalo kuhakikisha kuwa Bajeti za Wizara zote zinapita na Misimamo na Hoja za Serikali zinapita bila rabsha yoyote. Hayo yameagizwa hivi punde wakati wa kikao cha Wabunge wote wa CCM kilichomalizika muda mchache uliopita. Mtoa taarifa ambaye pia ni Mbunge kutoka mkoani Tabora,aliyekuwepo katika Mkutano huo, amesema kuwa kila Mbunge ameagizwa kuzingatia mambo hayo kwa ukamilifu.
"Mzee,mle ndani kulikuwa na Mjadala mkali sana. Wabunge wengi walionesha kutoridhishwa kwao na Bajeti za Wizara mbalimbali zinazowwasilishwa Bungeni ikiwemo ya leo ya Mh. Anna Tibaijuka. Walisema kuwa Kambi ya Upinzani imekuwa ikisumbua na hoja zao kukosa majibu" alisema mtoa taarifa.
Aliongea kwa kusema kuwa Mwenyekiti wa Caucus aliruhusu mijadala mikali ya Wabunge lakini mwishoni msimamo wa kichama ukatolewa. Wabunge wote walitakiwa kuhakikisha kuwa Bajeti,Hoja na Misimamo ya Serikali inapita na kutetewa ipasavyo. " Wabunge waliambiwa wana ruhusa ya kukosoa kwa maneno ya staha na katika hali ya kujadili kama wengine.Lakini, mwishoni wahakikishe kila jambo linafanikiwa" aliongeza Mbunge huyo
Haya tena,Wabunge wetu wameruhusiwa kuendelea na kujadili na kupitisha kwa sauti za 'ndiyoooooooooooooooooo'
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam