Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
HALI ya kisiasa katika jimbo la Bunda kwa upande wa Chama Cha Mapiduzi (CCM) inazidi kuchafuka, ikiwa ni matokeo ya kushindwa kwa Steven Wassira katika nafasi ya ubunge, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.
Jimbo hilo lilichukuliwa na Esther Bulaya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hivyo kumgalagaza mwanasiasa huyo mkongwe, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM.
Wapiga kura watatu walifunga kesi Mahakama Kuu kupinga ushindi wa Bulaya lakini hata hivyo walishindwa kuthibitisha udanganyifu wowote.
Kutokana na kushindwa huko kwenye sanduku la kura, wanachama wa CCM ‘wanakabana koo’ kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, na miongoni mwa wanaotajwa ni baadhi ya viongozi wake.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa kamati ya siasa ya CCM katika kata ya Nyasura na viongozi wa matawi yake wanakamilisha taratibu za kuwavua uanachama vigogo wanne wa wilaya. Mbali na vigogo hao, CCM pia inataraji kuwafukuza wanachama wanne maarufu.
Katibu Mwenezi wa CCM katika kata hiyo, Frank Mamba alisema wanachama hao wameitwa kuhudhuria kikao kitakachowajadili na kwamba endapo watakaidi wito huo, hatua zitachukuliwa na wao kufikishiwa taarifa rasmi.
"Tumeisha waandikia barua za kuja katika kikao kwa ajili ya kufanya mahojiano ya tuhuma zinazodaiwa na wanachama kupitia vikao vilivyokaa kwa wakati tofauti katika kutathmini matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Octoba 25 mwaka jana,” alisema.
“Kikao cha tawi la Nyasura B kilikaa Desemba 11 mwaka jana na kuazimia viongozi walioshiriki kukihujumu chama waitwe na kamati ya siasa. "Tawi la Nyasura A lilikaa Machi 21 mwaka huu na kupendekeza wafukuzwe uanachama.”
Source: Nipashe