CCM Bukoba yapasuka vipande vipande,viongozi wajiudhuru!

DJ Baraka

Senior Member
May 15, 2013
177
82
Leo kulikuwa na kikao cha kamati kuu ya mkoa kilicholenga maandalizi ya kuandaa hoja za kutoa maoni katika rasimu mpya,kilikuwa chini ya mwenyekiti wa CCM mkoa Contacia buhiye.

Katika kikao hicho kumetopea vurugu za hapa hapa na pale baada ya kuwepo uteuzi wa baadhi ya wajumbe kupewa nyadhifa mbalimbali ngazi ya wilaya katika kujipanga kimkakati hasa suala la siasa za hapo.

Nikiwa naingiza taarifa hii ni kwamba viongozi kadhaa wamekabidhi barua ya kujiudhuru nyadhifa zao wakituhumiwana kuhujumiana.

Tayari MNEC Abdu kagasheki amekabidhi barua rasmi.

kwa ufupi,kwa Bukoba mjini CCM inaweza kuwa imezikwa leo!

Narejea na habari kem kem

Updates:

Tifutifu la huu mzozo limeanza kufuatia Mwenyekiti wa CCM mkoa Bi constancia Buhiye kumteua Bw Philber Katabazi a.k.a Nyerere ambaye hivi karibuni alishikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kagera kwa tuhuma za kuandaa vipeperushi vya kueneza udini katika jimbo la Bukoba mjini.Bado polisi wanachunguza tuhuma zake na hawajamfikisha mahakamani.

Aidha Katabazi(Nyerere) alihojiwa na tume inayochunguza mgogoro wa Meya wa Bukoba na Mbunge hivyo kisiasa wana CCM bukoba mjini wanamuona kama mtu ambaye si msafi ambaye hapaswi kushirikishwa katika maamuzi ya chama.

Taarifa zinasema kwa mantiki hiyo Bw Abdu Kagasheki ambaye ni MNEC ameamua kujiudhuru kwa sababu ya kuteuliwa kwa 'mtuhumiwa' huyo.

Aidha Katabazi ndiye MENEJA wa siasa chafu dhidi ya Mbunge wa bukoba mjini akihadhiliwa na Meya wa Bukoba anatory aman.Hivyo kuteuliwa kwa huyo bwana ni kama ule mzozo wa Kagasheki na Meya umeanza upya na kumbuka Mwenyekiti wa CCM Mkoa yuko upande wa Meya katika mzozo huo.

Nina mengi nitarejea
 
Updates

Nyerere gani?
yule jamaa muuza simu zilizotumika (used) karibu na duka la ben bazar? au mwingine

mbona huyo ni mchanga katika siasa za Bukoba
 
Hizo ni laana za kuchakachua kura za RWAKATARE mwaka 2005, eti HAMIS alishinda kwa tofauti y kura 100 kutoka KATA YA BUHEMBE. Sasa watusaidie hata kumtaja aliyechakachua hizo kura za CUF na kuipa NYINYIEMU ushindi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom