CCM Bingwa wa Mikakati na Ufanisi

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
CCM kwa kiasi kikubwa ni chama kilichobobea katika mikakati ovu na chenye ufanisi uliopitiliza katika utekelezaji.

Chama hiki kwa kadiri ya miaka inavyozidi, na aina ya viongozi inaowapata kinazidi kujiimarisha katika uharamia, uovu, ulaghai na mbinu chafu, na katika utekelezaji wa hayo, hufanya kwa ufanisi wa kiwango kilichopitiliza. Kinapotekeleza uharamia wake kinakuwa kimesoma kwa umakini mazingira na aina ya watu kinaowafanyia uharamia, na kutambua wazi matokeo, na madhara yake na jinsi kitakavyokabiliana nayo:

1. Mwaka 2020, kwa namna ya kiwango cha hali ya juu kabisa, kiliweza kujitangazia ushindi wa pekee kwa kuwatumia makada wake waaminifu, Tume ya uchaguzi, wakurugenzi wa Wilaya na jeshi la polisi. Na katika kutekeleza uharamia uliopangwa, hakikuwa na swalia Mtume, aliyeonekana kisiki alikamatwa, aliteswa, wengine wakapoteza hata maisha, na wengine bado wapo ndani. Kwa kutumia Tume ya Uchaguzi na wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi, kuna maeneno kilizuia mawakala wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi kutoingia vyumba vya kupigia kura, kuwachelewesha na hata kuwazuia kushuhudia ujumlishaji wa kura. Kwa kutumia Tume ya uchaguzi, kilijitengenezea kura fake, zilizobebwa kwenye mifuko, nyingine zilikamatwa, lakini nyingine zilifanikiwa kuingizwa na kuhesabiwa. Kikajitangazia ushindi ulipitiliza zaidi hata ilivyopangwa.

Siyo kwamba CCM ilikuwa haijui kuwa wapiga kura watachukia, lakini kilikwishaujua uwoga wa wapiga kura na kuutumia uwoga huo kukamilisha uovu bila ya hofu yoyote. Walipojifanya kutaka kuandamana, kwa kuutambua uoga wa wapiga kura, kiliitumia vyema hiyo karata. Ikayazima kwa urahisi kabisa.

2) Kutumia mali za Serikali. CCM wakati wote imekuwa ikizitumia rasilimali za serikali kwa manufaa yake bila hofu yoyote. Imeyafanya hayo kwa kuwatambua Watanzania walivyo waoga, wasomi walivyo wanafiki, na wengi wa Watanzania wanavyopenda kusimamia zaidi manufaa ya tumbo kuliko mstakabali wa Taifa lao. Safari wamevuka mipaka, kuna taarifa za uhakika zisizothibitishwa kuwa pesa ya covid 19 na vitambulisho vya mchinga, nayo ilipelekwa kwenye chama kitukufu

3) Mwaka 2015, CCM kwa kumtumia mwenyekiti wake, kinyume kabisa na katiba, ilipiga kabisa marufuku ya mikutano ya vyama vya upinzani, huku Polepole na Bashiru wakipuyanga nchi nzima kufanya mikutano ya CCM kwa kadiri wapendavyo. Kwa msaada wa Jeshi lake la Polisi, hakuna mwananchi wala chama kilichonyanyua pua kupinga kwa namna yoyote ile ya kuitikisa CCM na vyombo vyake

4) Kwa kutumia Polisi waie, iliwakamata na kuwasweka ndani viongozi na wapenzi wa upinzani waliojifanya kukosa sifa ya uoga, nchi nzima. Wote wakaufyata. Iliwatoa ndani kwa namna ilivyotaka.

5) Kwa kutumia wasiojulikana, baadhi walipotezwa, akina Lisu walimimininiwa risasi, wengine kucharangwa mapanga na kupoteza maisha. Hakuna mtuhumiwa wala mshtakiwa. Wote kwa uwoga na unafiki, tukaufyata

6) Kiliamua kuwanyima huduma muhimu wananchi waliochagua upinzani, tena kwa kumtumia mwenyekiti wake, kikatamba waziwazi na kuwaambia wananchi kuwa waliochagua upinzani watakula jeuri yao. Wote kimya. Nani atanyanyuka asiye na sifa ya uoga wa kupoteza maisha au kyozea jela au kufilisiwa kama alivyofanyiwa Mbowe?

7) Sahizi kinaamua kujinyofolea yeyote na kumpa ubunge, na kumbatiza kuwa ni mbunge wa upinzani. CHADEMA wamewafuta uwanachama wale waliotii maelekezo ya CCM ya kutengeneza upinzani bandia bungeni. Lakini mnadhani kutabafilisha chochote? Halima na wenzake wataendelea kuwa wabunge, CCM ikitaka inaweza kuwapa hata uwaziri wa mambo ya ndani ili wakawadhibiti waliowafukuza uwanachama. Nani atanyanyuka na kusema hapana?

8) CCM kwa kutumia serikali na bunge lake, imetengeneza sheria nyingi za kidikteta zinazozuia uhuru wa maoni, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kupata habari. Kwa kutumia serikali yake, inazisimamia hasa. Wote wanajua ni sheria za hovyo, lakini nani wa kunyanyuka. Wanaonyanyuka kidogo, wananlachwa pekee yao waozee mahabusu kama nyumbu wanavyofanya mmojawapo akikamatwa na simba. Yaani wanasema aheri amekamatwa mwenzangu, labda akimla yule atashiba, hatanila tena mimi. Asichojua ni kuwa njaa haiishii kwa kumla nyumbu mmoja leo.

Duniani kuna wanadamu magaidi, kuna vyama magaidi, kuna Serikali magaidi, kuna Polisi magaidi, n.k. Ugaidi msingi wake mkuu ni kumtendea uovu wa kutisha kila anayeenda kinyume nawe ili kumjengea uwoga anayetendewa au kundi linalotendewa.

Leo Tanzania imekuwa nchi ya wananchi waoga, vyama vioga, viongozi wa dini waoga, vyombo vya habari vioga, viongozi wastaafu waoga. CCM sasa imefanikiwa kuwatisha watu na taasisi zote kwa kutumia vyombo vyake.

Kimsingi, CCM ni terrorist party.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni aibu sana sarakasi za kijinga kama hizi mnapoona ni ufanisi.
Nitaona ni ufanisi iwapo tu wazungu watawapeni hiyo trillion mbili ya UTAWALA BORA
 
HILI DUBWANA CCM LINA MWISHO WAKE NA KARIBUNI SANA KUFA

Wanachama/ wananchi wamepokwa chama chao, CCM kikekuwa chama Dola.

polisi, Jwtz, Tiss,NEC wakuerugenzi nk.
 
Kweli ni chama nguli Africa hakijawahi tokea CCM ni number one. hata ukiipeleka kwa Trump marekani ni chama Bora na nakuhakikishia ushindi wa kishindo ni lazima upatikane.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Wao kama mabingwa wa mikakati wafanye kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Mitano tena ata pale dodoma yeye mwenyewe haelewi anaimaliza vipi
 
Yote hayo Yana mwisho wake. Hofu yangu Ni kua Kuna nyakati ccm itashindwa kusimama yenyewe bila msaada wa Dola.
 
Kweli ni chama nguli Africa hakijawahi tokea CCM ni number one. hata ukiipeleka kwa Trump marekani ni chama Bora na nakuhakikishia ushindi wa kishindo ni lazima upatikane.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Kule kitakuwa ni chama dhaifu kwa sababu kule vyama vya siasa na serikali vinavyoziunda hujitahidi kuwatendea wema wananchi. CCM ni mbobezi katika mbinu chafu na za kiharamia. Hakiwezi kufit kwenye jamii yoyote iliyostaarabika au jamii ya watu wasio waoga.

Katika definition ya terrorism, CCM ni terrorist party.
 
Ni aibu sana sarakasi za kijinga kama hizi mnapoona ni ufanisi.
Nitaona ni ufanisi iwapo tu wazungu watawapeni hiyo trillion mbili ya UTAWALA BORA

Bujibuji, unachotakiwa kujua ni kuwa hata jambazi kila linapotaka kuoliba likafanikiwa, huo nao ni ufanisi. Ni ufanisi katika uharamia.

CCM ni chama kilichobobea katika mipango ovu na chenye ufanisi katika mipango hiyo haramu. Na kinazidi kujiimarisha zaidi katika uharamia. Ni genge la maharamia linalojitahidi kudumu katika uharamia na kujiimarisha zaidi katika huo uovu.

Uharamia wa 2010 ulikuwa na unafuu kuliko wa 2015, uharamia wa 2020 umefunga kazi kuliko uharamia wote uliotangulia.

Kama hakutakuwa na jitihada zozote za wananchi, 2025 itafanya uharamia mbaya zaidi kuuzidi huu wa 2020.
 
Wao kama mabingwa wa mikakati wafanye kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Mitano tena ata pale dodoma yeye mwenyewe haelewi anaimaliza vipi
Tajiri kichwa, unawapa kazi ambayo hawana ujuzi nayo. CCM haijawahi kuwa thabiti katika mipango ya maendeleo.

Yenyewe ubingwa wake na ufanisi upo kwenye uovu siyo kwenye maendeleo.

Mafanikio mengine:

Wakati wa Mkapa mauaji ya wapemba, wananchi kimya!

Mauaji ya Arusha, wananchi kimya!

Mauaji ya Mawazo, wananchi kimya!

Mauaji/upotezwaji wa Ben, Azory, wananchi kimya.

Mauaji na upotezwaji wa wananchi wa Rufiji, wananchi kimya!

Risasi kwa Lisu, zaidi ya ngiri anavyodlshambuliwa, wananchi kimya!

Uswekaji ndani wa viongozi mbalimbali wa upinzani, Mbowe, Msigwa, Zito, n.k, wananchi kimya!

Safari hii, mauaji tena ya wapemba na kule Tarime, wananchi kimya!

Kama CCM siyo mabingwa wa utekelezaji wa uharamia, basi wananchi wa Tanzania ni nusu binadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tajiri kichwa, unawapa kazi ambayo hawana ujuzi nayo. CCM haijawahi kuwa thabiti katika mipango ya maendeleo.

Yenyewe ubingwa wake na ufanisi upo kwenye uovu siyo kwenye maendeleo.

Mafanikio mengine:

Wakati wa Mkapa mauaji ya wapemba, wananchi kimya!

Mauaji ya Arusha, wananchi kimya!

Mauaji ya Mawazo, wananchi kimya!

Mauaji/upotezwaji wa Ben, Azory, wananchi kimya.

Mauaji na upotezwaji wa wananchi wa Rufiji, wananchi kimya!

Risasi kwa Lisu, zaidi ya ngiri anavyodlshambuliwa, wananchi kimya!

Uswekaji ndani wa viongozi mbalimbali wa upinzani, Mbowe, Msigwa, Zito, n.k, wananchi kimya!

Safari hii, mauaji tena ya wapemba na kule Tarime, wananchi kimya!

Kama CCM siyo mabingwa wa utekelezaji wa uharamia, basi wananchi wa Tanzania ni nusu binadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Umesahau mkakati wa kukuza wajinga na vijana wachumia tumbo
 
Back
Top Bottom