CCM bahati ya mtende

ZeMarcopolo

Platinum Member
May 11, 2008
14,017
7,220
Vyama vya upinzani Tanzania havijajenga uhuru wa mawazo unaoruhusu ushindani wa kisiasa ndani ya vyama hivyo, ndio maana mashabiki wa vyama vya upinzani wanapata shida kuelewa kinachoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye kumtafuta mgombea wake wa urais.

CCM imefanya kazi nzuri kuliongoza taifa letu na imeweka misingi ya fursa kwa kila mwenye bidii. Tanzania ni taifa la kutolewa mfano barani Afrika kutokana na kazi nzuri ya CCM.

Lakini ni wajibu wa wanaCCM kukiri kuwa kwa kiwango fulani chama kimetoka nje ya misingi iliyokiasisi.

Vipo viashiria vingi lakini kimoja ni Lowassa kufikiriwa kuwa atapitishwa kugombea urais. Iwapo chama kingekuwa imara kwenye misingi ya uadilifu, mtu kama Lowassa hata asingefikiria kuchukua fomu.

Lowassa anamwaga mapesa kwa wajumbe na makada kwa vile anajua ndani ya chama cha mapinduzi siku hizi pesa ndiyo inayoamua nani awe kiongozi.

Hii ni hatari na vijana lazima wawe mstari wa mbele kulisema hili kwa sauti kuu.

Rushwa ikishamiri kwenye chama itaingia serikalini. Itafikia wakati ukuu wa shule utakuwa unauzwa, ukuu wa idara utapangiwa bei, na huo ndio utakuwa mwisho wa ufanisi. Nchi itaporomoka na hakutakuwa na jinsi ya kuzuia kuporomoka huko.

Lowassa kawaahidi watu wengi vyeo serikalini iwapo atakuwa Rais. Je, nani atasimamia na kukagua ufanisi wa watu walioingizwa kisiasa na mkuu wa nchi? Hawa hawatagusika. Mtu wa namna hii anapofikiriwa kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM basi ni ishara tosha kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaonyesha dalili za kukinzana na malengo ya kuasisiwa kwake.

CCM imekataa kubadilika kwenye rushwa, hasahasa rushwa za uchaguzi. Rushwa za uchaguzi huzaa viongozi wasiowajibika kwa watu. Kwanini CCM inachagua kutoa viongozi wanaowajibika kwa pesa za uchuuzi?

Viongozi wasiowajibika kwa watu hufanya watu hao wakichoke chama.

Ndio maana kundi la vijana ambao wanaisema vibaya CCM linaongezeka kila baada ya uchaguzi. Ugomvi wao na CCM sio kwa sababu ina sera mbaya na sio sababu haijajenga nchi, ila kwa sababu viongozi wanaotokana na CCM hawaonyeshi udhati wao kwenye kushughulikia masuala yanayoikera jamii kama hili la ufisadi.

Agenda kuu katika uchaguzi wa mwaka huu ni UFISADI. Je, vigezo vya kumpata mgombea wa CCM vinazingatia hili? Kutokuzingatia hili ni kujitenga na jamii na kuifanya wasiipende CCM.

Bahati ya mtende kuota jangwani ndio inayofanya CCM iendelee kubaki madarakani. Hakuna Chama cha upinzani chenye infrastructure ya kuongoza nchi. Ndio maana watanzania wataendelea kuichagua CCM. Wanaichagua CCM kwa shingo upande huku wakijua they deserve better, but better is not available.

Good news kwa CCM ni kwamba watanzania wanaipa nafasi ya kujirekebisha. Now it's up to CCM kama itajirekebisha au itaendelea kutegemea udhaifu wa wapinzani. Wakati huohuo wapinzani pia wamekuwa wakitegemea udhaifu wa CCM kujitwalia majimbo na kata lakini kwenye Urais ni tofauti.

Vijana wanaokumbatia rushwa za uchaguzi ni vipofu wa fikra, kwa sababu wanachofanya ni kuharakisha tu process ya CCM kuwa chama cha upinzani. Wanajiharibia wenyewe future yao kwa tamaa za muda mfupi.

Mabadiliko ya kweli ni si lele mama...
 
Safi sana. Kati ya watakaomkosesha urais Lowassa ni Hamis Mngeja M/kiti CCM Shinyanga amekuwa kimbelembele mno kumpigia debe Lowassa hadi kumtukana Nape hadharani.
 
Safi sana. Kati ya watakaomkosesha urais Lowassa ni Hamis Mngeja M/kiti CCM Shinyanga amekuwa kimbelembele mno kumpigia debe Lowassa hadi kumtukana Nape hadharani.
Sikio la kufa halisikii dawa, hivi kweli mtu ambaye Kampeni meneja wake ni ROSTAM atakuwaje raiis?
 
Unaposema UKAWA haujajipanga kuchukua nchi unamaanisha nini? Masual yote muhimu yameshawekwa mezani iwe ni protokali, mambo ya nje sekta ya madini na nishati nk vyote vimesharatibiwa. Na ukumbuke UKAWA hautegemewi kuvunja vyombo vya dola bali ni kuviratibu tu. Muungano utadumishwa kwa gharama yoyote ile. Kwa hiyo wananchi msiogope kuchagua UKAWA eti kwa sababu hawajajipanga!
 
Unaposema UKAWA haujajipanga kuchukua nchi unamaanisha nini? Masual yote muhimu yameshawekwa mezani iwe ni protokali, mambo ya nje sekta ya madini na nishati nk vyote vimesharatibiwa. Na ukumbuke UKAWA hautegemewi kuvunja vyombo vya dola bali ni kuviratibu tu. Muungano utadumishwa kwa gharama yoyote ile. Kwa hiyo wananchi msiogope kuchagua UKAWA eti kwa sababu hawajajipanga!

UKAWA hawana political infrastructure ya kuongoza nchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom