CCM badilikeni, wenyeviti wa CCM Mikoa na Wilaya wawe wasomi wenye vyeti vya taaluma

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Wakati Umefika sio kwa CCM TU bali kwa VYAMA VYOTE vya SIASA kuwa na VIONGOZI WASOMI na Wenye VYETI vya TAALUMU badala ya sasa Mtu anachaguliwa ili Mradi Kaomba hiyo Nafasi na ana FEDHA za KUWAHONGA wajumbe.

NCHI hii ina WASOMI WENGI SANA wasio na AJIRA na Wana TAALUMA nzuri ambazo WAKIPEWA UONGOZI watatumia ELIMU na TAALUMA zao KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI.

CCM imejenga CHUO KIKUU cha UONGOZI KIBAHA ni Rahisi Kumpeleka MSOMI mwenye TAALUMA ili kumpiga MSASA kuliko hao Viongozi wasio na ELIMU au TAALUMA yoyote na Wamepata UENYEKITI wa Mkoa au Wilaya kwa KUHONGA WAJUMBE kwenye CHAGUZI.

Nakishauri Chama cha Mapinduzi CCM na VYAMA VINGINE Kifanye MABADILIKO haya kwenye UCHAGUZI wa VIONGOZI wake Unaotarajiwa kufanyika MWAKA huu 2022

bd9fadcfec3a952bb7beefef291bd5f6.jpg
 
Ni wazo zuri ,itasaidia tutakuwa tunaibiwa na hili liCHAMA kisomi zaidi .
 
1.Nitajielimisha kadri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.

2. Injili takatifu inasema "Mshike sana elimu usimuache aende zake"

3. Mafundisho ya uislamu yanasema "Kutafuta elimu ni jambo la lazima kwa Kila muislamu wa kiume na WA kike"

Elimu elimu elimu

Asanteni
 
Wasomi wetu wengi wana vyeti lakini kichwani ni weupe mfano mzuri ni viongozi wetu ni maprofesa lakini masuala madogo wanaleta janja janja
 
Wasomi walishaisaidia nini Tanzania? Nchi hii hakuna tofauti ya aliyesoma na ambaye hajasoma maana wote wamekuwa mizigo kwa serikali. Wasomi wajiajiri vinginevyo wataua taaluma zao wakijiingiza kwenye siasa.
 
Back
Top Bottom