CCM ,Badilikeni tuungane tujenge Mifumo na Tasisi Imara baadala ya watu wa kuwaabudu.

Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Sep 8, 2010
1,017
256
Nawaomba wananchama wa CCM wabadilike na waache kujenga na kuwatukuza watu kama Miungu wanaoweza kufikiri na kuamua mambo ya nchi kwa naiba yetu wakati wote.
Imekuwa ni desturi ya wana CCM kila wanapoatoka ktk vikao vyao hasa NEC kutoka na maazio mbalimbali. Cha ajabu wajumbe wengi wa vikao hivyo wanakuwa wakwanza kumpongeza mwenyekiti kwa mazimio ya kikao.Mfano azimio la kujivua gamba. wajumbe wametoak wakimpongeza Mwenyekiti kwa uwamuzi wa kijivua gamba na si NEC.
Tabia hii inaendelea mpaka kwenye kamati na hata taarifa zao wanazi personalize, maoni ya kamati yanakuwa ya mwenyekiti(Mwakyembe au Pindi Chana ), maoni ya kambi ya upinzani yanakuwa ya msemaji (Lissu). Siamini kuwa maziamia ya vikao ni ya mwenyekiti au Msemaji wa kambi ya upinzani.

Tabia hii ya kujenga au kubomoa na kutukuza watu imetuletea fedhea, manung'uniko na mitafaruki kibao :
mfano.
1) Wabunge Kushindwa kumwajibisha Kurungezi wa TAKUKURU (Dr.HOSEA) kwa kuisafisha Richmond na badala yake wakageuziwa kibao cha wao wabunge vimbelembele kuchunguzwa kwa kupokea Posho mbili. Wote ni mashahidi wabunge wamenywea na Hosea kawafumba midomo hadi leo
2) Tumeshuhudia Jaji Kisanga akitukwanwa na Rais Mstaafu kwa kihelehele cha Kutoa maoni ya kutaka serikali tatu. Jaji kisanga alisema anamwachia Mungu! Kisa kateuliwa na rais hakuna wa kumwondoa
3) Mwaka jana tumeshuhudia Kampeni za BMW ( Baba Mama na Watoto) - Kisa urais huana ubia na hakuna ukomo wa madaraka ya rais ambaye pia ni mwenyekiti wa cahama.
4) Tumeshuhudia Rais akianza Ujasiriamali akiwa ikulu - kisa hakuna ukomo wa madaraka na speed gverner kwa Rais.
kwa mifano hii michache, CCM naomba mbadilike tuungane na wananchi wengine hata kama wako CDM, ni wanaharakati au wanasheria Wastaafu wote ni WATANZANIA
kuwa chadema, Mwanaharakati, mwanasheria mstaafu hakuondoi UTANZANIA WAO, Maoni yao yakichukuliwa kama ya Watanznia na kuyapinga au kuyanga mkono kwa hoja mtafaruku unapotea. Lakini tukizani Watanzania ni wale tu wanoa unga mkono hoja 100/100 tunapotoka.

Tusimame kama kitu kimoja tuunde taasisi na mfumo imara wa namna ya kuendesha nchi yetu badala ya kutegemea utashi wa mtu.
Kutuegemea utashi wa watu kunatufanya watumwa wa kila mara kumshuru kwa hisani, hebu fikiria namna wabunge wa CCM wanavyo poteza muda mrefu kupongeza na kushukuru utashi na hisani ya Rais kwa kila jambo.

CCM ikifikiri watanzania wataamini kuwa mawazo yote yaliyotafaouti na CCM ni upotoshaji, itakuwa imelala usingizi wa pono. kwa sababu kuna maeneo hata kionekana a umevaa kapero ua furana ya CCM unonekana kama ZUZU!!! kwa sababu ya propaganda na ahadi zisizo na kichwa wala miguu.
Ni maoni tu, mnaweza kuchukuwa ua kuyapiga chini kama kawaida
na kiniita mpotoshaji pia.

Stay Blessed Tanzania.
 
Back
Top Bottom