CCM asili kwafuka Moshi, mwenye pesa ndio mshindi. Polepole ahusishwa na Rushwa

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
MWAMBIE POLEPOLE KAMATI KUU CCM IMECHEMKA NA IMEKOSA MENO

Na Thadei Ole Mushi

Jana nilisema mwenye fedha ana asilimia 90 za kushinda uchaguzi huu wa kura maoni ndani ya CCM kutokana na mfumo ulivyo ndani ya chama. Niliwaambia Jana hakuna mahali ambapo Mjumbe wa kwenye Shina anaweza kukataa shilingi elfu 20 hadi elfu 40.

Jambo la Pili ambalo ni kutokuwa makini ni mchakato wenyewe. Hapo mwanzo chama kilisema kingefanya vetting kwa watakao chukua form wote halafu wangerudisha majina matatu. Yaani kati ya majina hayo matatu yeyote ambaye angelishinda angefaa kuwa Mbunge. Niseme tu wazi wazi hili lilikuwa la maana sana.

Kwanza lilipunguza Rushwa kwa wajumbe maana hakuna aliyekuwa anajua kama jina litarudi hivyo waliogopa kupoteza fedha.

Pili, waliogopa vyombo vya Usalama vingewachuja na kuondoa majina yao kwa maana ya kwamba yasingerudi kutokana na utoaji wa Rushwa ya aina yoyote.

Tatu ndio mfumo unaotumika sehemu nyingi katika kupata Viongozi Bora. Hii ndio tunayoiita vetting kuangalia uwezo wa mtu, na uadilifu wake kabla hatujampa Majukumu ya kuwatumikia wananchi.

Kilichotokea
Baada ya kuondoa utaratibu huu tumeruhusu hadi majambazi kuchukua Form na wataenda kujinadi kwa Wapiga kura. Hapa ndipo mwenye fedha atakaposhindia na kuacha vijana wenye uwezo kiongozi lakini walikosa tu fedha za Kununua Kura.

CCM wanasema baada ya Kura wagombea watajadiliwa na kutolewa mapendekezo. Kuna ugumu mkubwa sana kumuengua mtu aliyeshinda kwa kura na kumpa mtu mwingine hiyo nafasi. Hapo ndipo makundi yanapoanzia na kuwanufaisha Wapinzani. Bora huyu mtu asingelipigiwa Kura mngemkata mwanzoni angelitulia kuliko kashashinda ndio mnakata jina. Hizi ni akili za kinyume nyume na zitagugarimu.

Lakini kingine ni kwamba WATIA nia ni wengi sana kuna majimbo yana watia nia kuanzia 15 Hadi 60. Hivi kusikiliza watu Hawa wote na kuamua nani anayefaa kunawezekanaje? Akianza wa kwanza akifika wa 10 tu walishasahau wa kwanza alisema nini. Pale Rorya nasikia wapo 60 hiki ni kichekesho.

Mfumo wa kurudisha majina matatu yalikuwa yanawapa fursa CCM kupata vichwa haswa pale Bungeni, ulikuwa unawafanya CCM kuondoa makapi ya Awamu zilizopita, Ulikuwa unawafanya CCM kutokuja kumtesa Rais kwenye kuteua Nani awe wizara flan na Nani awe pale, tunakumbuka alivyoteseka kwenye kuunda Serikali Hadi akawakopa kina Mpango na Kabudi, Ungemfanya Rais asitumbue kila siku kutokana na watu kukosa uwezo, tungewatendea haki wananchi kwa kuwapa watu sahihi wa kuwasemea na kutatua shida zao.

Nimwambie tu Mh Polepole Hakuna Demokrasia isiyokuwa na gharama, kiongozi kuogopa kulaumiwa wewe hufai, najiuliza mbona kwenye Urais tumechuja hadi kubaki na watatu wa kupigiwa Kura? Kwanini hatukuwaleta wale wa Zanzibar wote 31 kuomba kura kwa wajumbe wa mkutano? Tulikimbia nini? Kwanini huku chini tumewaachia holela? Hata mkiwa na Rais mzuri kiasi gani bila kumpa wabunge mahiri ni kitu gani mmefanya?

Mfumo unashawishi rushwa,
Mfumo utatufanya tuuze nafasi za uongozi Kama nyanya za kwenye mnada mwenye fedha nyingi ndiye anayechukua tenga,
Mfumo utatupatia watu wabovu na wasio waadilifu,
Mfumo unawanufaisha wenye fedha,
Mfumo unakatisha tamaa,
Mfumo ni mbovu kabisa.

Msikilize Mwenezi akielezea mfumo Mbovu. Waliohonga vizuri Leo Ni siku yao ya kuchukua Form wanajiamini haswa.

Ole Mushi
0712702602.
 
Huyu Mushi si angeenda kwenye vikao vyao akayasema haya? CCM inefundisha vijana wao kukosa adabu?
 
Back
Top Bottom