CCM Arusha yawageukia waendesha Bodaboda ,yawanyakuwa wapinzani

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
704
1,000
Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Themi ,jijini hapa kimewawezesha Kofia Ngumu Madereva pikipiki( bodaboda) wapatao 100 kwa lengo la kuwanusuru na ajali zisizozalazima ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na kupunguza nguvukazi ya taifa.

Akiongea kwenye Mkutano wa hadhara wa chama hicho,Mwenyekiti wa CCM kata ta Themi,Thomas Munisi amesema mpango huo umelenga kuondoa changamoto ya kutokuwa na kofia ngumu na kusababisha baadhi ya waendesha pikipiki kukamatwa na askari wa usalama barabarani.

Hatua hiyo iliibuka katika zoezi la kufungua mashina katika kata hiyo, ambapo baadhi ya vijana walionyesha kuwa na changamoto ya ukosefu wa kofia ngumu jambo ambalo chama hicho kililazimika kuwafadhili kupitia mpango wake wa kuwezesha vijana na kuwapatia kofia hizo.

Baadhi ya waendesha pikipiki, Elisha Mbise na simon Swai wamekishukuru chama cha mapinduzi kata ya Themi kwa hatua ya kuwawezesha kupata kofia ngumu wakidai kwamba zitawasaidia sana katika kujikinga na ajali wakati wakitekeleza mahukumu yao.

Katika hatua nyingine Munisi amewaonya wanachama wa chama hicho kuacha kuwabeba baadhi ya wagombea wa CCM kwa maslahi yao kwa kuwa chama hicho kinamfumo mpya wa kupata viongozi wake.

" ule uongozi wa zamani wa kila mwanachama kuwa na viongozi wake mfukoni kwa sasa hilo halipo na tukigundua kuna mgombea yoyote anatumua wanachama wetu kutaka uongozi tutamfyekelea mbali"Amesema Munisi.

Aidha aliwataka wanachama kuacha tabia ya kutembea na majina ya wagombea mfukoni kwa kuwa kila mwanachama anayetaka kugombea anapaswa kuja ofisini kuchukua fomu.

Wakati huo huo Munisi alisema CCM imefanikiwa kuwanyakua baadhi ya wafuasi wa chadema wanaokihama chama hicho akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema katika kata hiyo,ambao wamejiunga na ccm wakidai wameridhishwa na utendaji Kazi wa CCM chini ya mwenyekiti wake Taifa,Dkt John Magufuli.

Ends....

IMG_20190707_174400.jpeg
IMG_20190707_175113.jpeg
 

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
4,484
2,000
Wawape na bodaboda kabisa,kofia ngumu ni hadi elfu ishirini vijana hawawezi kushindwa kununua.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom