CCM Arusha yamsafisha mtia nia wa Ubunge na kashfa ya TAKUKURU

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha kupitia jumuiya ya wazazi Mkoani hapa kimelalamikia taarifa za upotoshaji kwa makada wake akiwemo mtia nia wa nafasi ya ubunge wa viti maalumu , Lilian Ntiro waliohusishwa na rushwa wilayani Longido na kudai kwamba taarifa hizo zinapotoshwa na Vyombo Vya Habari.

Akiongea ofisini kwake,mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Arusha, Ezron Mbise alisema tuhuma zinazowakabili Makada wake sita hazina ukweli wowote na zimelenga kukipaka matope chama chao na kuitaka TAKUKURU kufanya uchunguzi wa kina kwa sababu zinatokana na fitina za uchaguzi.

Alisema miongozi mwa waliokamatwa na takukuru pia yumo mjumbe wa baraza la Jumuiya ya Wazazi wa CCM mkoa, Sifael Pallangyo anayedaiwa kukutwa na fedha tasilim shilingi 14,000 huku taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti moja la kila siku zikipotosha na kuonyesha alikutwa na kiasi cha Shilingi milioni 14, jambo ambalo alidai si kweli.

Alisema pamoja na kwamba jambo hilo lipo ndani ya vyombo vya uchunguzi haizuii chama hicho kulalamikia makosa ya upotoshaji yaliyotolewa na vyombo vya habari na mitandao na kueleza kwamba taarifa hizo zina mlengo wa kuwachonganisha wananchi na chama chao.

Alisema Liliani hahusiki kuwatuma viongozi wa jumuiya hiyo ya wazazi kwenda kugawa fedha kwa wajumbe ila makada hao walienda Longido kwa shughuli zao za kurina asali na kukamatwa hata hivyo aliongeza kwa kutaka jambo hilo liachiwe takukuru.
 
(Alisema liliani hahusiki kuwatuma viongozi wa jumuiya hiyo ya wazazi kwenda kugawa fedha kwa wajumbe ila makada hao walienda Longido kwa shughuli zao za kurina asali na kukamatwa.) Hii nchi sasa, kumbe unaweza waambia hivi takukuru wakafuta kesi? au wananchi wakakuelewa? Labda hii chama chetu pekeeeeeeee
 
Back
Top Bottom