CCM Arusha wasali Nyerere afufuke kuokoa jahazi la Chama ambalo limezama na JK siyo.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Arusha wasali Nyerere afufuke kuokoa jahazi la Chama ambalo limezama na JK siyo..

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 15, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Kwa mara ya kwanza, makada wa ngazi za juu wa CCM hapa Arusha wameanza kukiri ya kuwa tofauti na ngebe za Katibu Mkuu wao, Yusufu Makamba, JK siyo mtaji mkuu wa chama hicho kikongwe nchini bali Nyerere ndiyo uliokuwa mtaji tegemezi na sasa wajutia Dr. Slaa kuwanyang'anya huo urithi.

  Wamesema tabia ya JK kuwakumbatia mafisadi na kula nao sahani moja ndiyo imemwondoa baba wa taifa kutoka katika Chama hicho na akiwa kaburini unajimu wake sasa utatimia aliousema mwaka 1995 kule Dodoma ya kuwa "Kama watanzania watakosa kiongozi wa kutumainiwa ndani ya CCM watamtafuta nje ya CCM" Dr. Slaa aonekana kurejesha matumaini ya watanzania badala ya mtu wao JK.......................

  Mjadala mzito niliouhudhuria leo hapa mchana Arusha kwenye kijiwe cha wakereketwa wa CCM wamenitobolea kwa uwazi kuwa Dr. Slaa sasa hashikiki na hakuna anayeweza kuokoa jahazi hilo labda Nyerere afufuke.

  Wanasema mikakati ya Makamba na JK wake kumnadi JK kama ndiyo mtaji mkuu wa CCM sasa ni shubiri ya kutupwa na kuongeza ya kuwa JK siyo Nyerere na bila ya Nyerere kufufuka basi wanajiandaa kujifunza siasa za serikali kivuli upinzani.
   
Loading...