CCM Arusha wadaiwa kutumia mlemavu wa akili kuombea kura

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
549
Kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani jijini Arusha zimezidi kupamba moto, huku CCM kupitia kwa naibu Katibu mkuu wake Mwigulu Nchemba akija na mtindo mpya wa kumtumia kijana mmoja anayedaiwa kuwa na ulemavu wa kudumu wa Akili(Taahira) kama sanamu la kuombea kura majukwaani na kisha kumlipa ajira kwa kazi hiyo.

Kijana huyo anayejulikana kama Tesha, ameharibika sura yake kufuatia kumwagiwa tindikali usoni wakati wa uchaguzi wa Igunga mwaka juzi.

Baadhi ya wakazi wa Arusha walishangazwa na kitendo cha kijana huyo kukubali kupandishwa majukwaani ili aonyeshe ulemavu wake wa ngozi usoni na hapo ndipo CCM wapate nafasi ya kuomba kura kwa kigezo cha huruma lakini pia kwa njia ya kukipaka matope chama cha CHADEMA.

Lakini watu kadhaa waliokaa karibu naye na kufuatilia nyendo zake kimatendo na maneno wamegundua hana Akili sawa sawa(Low IQ).

Hapo kabla ilishawahi kuelezwa kuwa huyu kijana kutokana na kuwa na Matatizo ya kiakili amekuwa akikubali kutumiwa kufanya vitu vya hatari tena kwa ujira mdogo sana.
Hata tukio la kumwagiwa Tindikali usoni inadaiwa ni kutokana na wenzake wawili kumgeuka baada ya kuwadhurumu pesa walizopewa na Mwigulu kule Igunga ili waende wakachane picha na mabango ya mgombea ubunge wa CHADEMA.
 
mkuu hizi ni dalili za kufa taratibu (silent killer) na bado wanatamani ata wasimamishe dr ulimboka,kibanda na mjane wa mwangosi rip ili waweze kujisafisha though wanajua hawawezi ata siku moja (rip magamba)
 
Last time alipokuja Lipumba na viongozi wengine wa CUF walimsimamisha Jukwaani mama mmoja mjane ambaye mumewe aliyeuwawa na polisi katika maandamano ya CHADEMA 2011 na kudai CHADEMA wamemtelekeza bila kumlipa chochote.
Watu wengi walijua ni njaa inamsumbua ndio maana akakubali kujidharirisha kwa kutumia ujane wake kusimama majukwaani. Baada ya CUF kuondoka tu, amerudi kwenye njaa yake ile ile!!!
 
Mwigulu Nchemba Oscar nimekupata. Aliyemwagiwa tindikali anafanya kwa hiari na anashuhudia. Sio kulazimishwa plz. Najua unamhurumia ila yeye ndiye anapenda aseme

17 hours ago via mobile · Like

Haya ni majibu yake toka fb........ni upuuuzi, hata kama anataka mwenyewe, you have to think twice
 
Ninachojua ni kwamba, Tesha alimwagiwa tindikali na CCM wenyewe ili kucover kwamba ni CHADEMA. Kwakuwa Tesha aliumizwa nao, amekubali kutumiwa kwa posho tu. Haina impact zaidi ya kutishia watoto wadogo
 
Mwigulu Nchemba Oscar nimekupata. Aliyemwagiwa tindikali anafanya kwa hiari na anashuhudia. Sio kulazimishwa plz. Najua unamhurumia ila yeye ndiye anapenda aseme

17 hours ago via mobile · Like

Haya ni majibu yake toka fb........ni upuuuzi, hata kama anataka mwenyewe, you have to think twice
Asante mkuu kwa kutupa taarifa rasmi ya Mwigulu.

Jambo baya ni kwamba huyo kijana Tesha anasafirishwa kwa ruzuku ya CCM na analipwa ujira kwa kazi hiyo anayoifanya but katika hali ya isiyo ya kawaida ana matatizo ya kiakili pia.
 
Mwigulu Nchemba Oscar nimekupata. Aliyemwagiwa tindikali anafanya kwa hiari na anashuhudia. Sio kulazimishwa plz. Najua unamhurumia ila yeye ndiye anapenda aseme

17 hours ago via mobile · Like
Vp na cdm wamsimamishe dr ulimboka,kibanda?ambao mmewang'oa meno na kucha bila hata huruma?achilia mbali hao je ni haki kumsimamisha mjane wa mwandishi Daud?,wewe cdm tutapochukua nchi mimi nitakutafuta hata kama kukufungulia mashitaka the hague -unastahili kabisa,kumbuka braza wewe ni kijana na utarajie kuishi sana tena muda huo cdm iko kwenye dola,jiandae braza

Haya ni majibu yake toka fb........ni upuuuzi, hata kama anataka mwenyewe, you have to think twice

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Huu ni udhalilishaji.
Kama sera imeisha basi Mwigulu asiishie hapo..Namshauri akusanye walemavu wa kila aina mfano..
Albino
Walemavu wa miguu na mikono
Vichaa
N.k
Aseme ni chadema ndo wamesababisha.
Lakini wako wapi watu wa haki za binadamu?
Kumtumia mlemavu kama mtaji wa kura ni utu?
 
Angekuwa na akili angejitolea kumsaidia kwa tiba ili arudi ktk hali ya kawaida na siyo kumdhalilisha majukwaani!Wana ushahidi gani kuwa Chadema ndio wahusika waliomsababishia ulemavu na kwa nini kama serikali hawakuchukua hatua kwa wahusika?CCM isitafute huruma kwa wananchi kwa makosa yao wenyewe
 
Asante mkuu kwa kutupa taarifa rasmi ya Mwigulu.

Jambo baya ni kwamba huyo kijana Tesha anasafirishwa kwa ruzuku ya CCM na analipwa ujira kwa kazi hiyo anayoifanya but katika hali ya isiyo ya kawaida ana matatizo ya kiakili pia.

Huu ni udhalilishaji ulio kithiri. Ifike mahali Jumuiya ya Walemavu ilikatae hili. Hata Taasisi za Haki za Binadamu waingilie kati.

Haiwezekani muathirika wa aina ile ageuzwe KINYAGO wa kunadi Kampeni kisa wanasingiziwa watu wengine kumfanyia jambo baya.

Inajulikana wazi kwamba, walio fanya jambo lile ni MAGAMBA wenyewe. Roho zinawasuta ndio maana wanahangaika nae kwa kumfanya ndio Mtaji wa Kuombea kura.

Nijuavyo mimi, Mtaji wa kuombea kura ni kuwa na SERA ZA MAENDELEO NA ZINAZO TEKELEZEKA. Sio kutembeza mtu mwenye madhara ya namna ile. Hapa ni dhahiri MAGAMBA wameishiwa SERA.
 
Jaman huyo si mlemavu. Watanzania tuache ushabiki
Hakuna ushabiki hapa.
Yeye mwenyewe anakiri kuwa tindikali aliyomwagiwa usoni umempa ulemavu wa Ngozi na Macho(Hata ukimtazama anaonekana hivyo) lakini pia watu waliokuwa naye karibu wanadai ukimsikiliza maneno na kutazama vitendo vyake ni dhahiri kabisa ana ulemavu wa Akili(Taahira).

Mwigulu yeye anajitetea na kudai hajamtuma wala kumlazimisha kijana huyo kupanda jukwaani na kujianika kama sanamu huku akionyesha ulemavu wake wa mwili alionao bali kijana huyo anafanya hivyo kwa hiari yake mwenyewe!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom