Ccm arusha - damu zetu na watoto wetu zitakuwa mikononi mwenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm arusha - damu zetu na watoto wetu zitakuwa mikononi mwenu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by chachana, Nov 10, 2011.

 1. c

  chachana Member

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimesikitishwa sana na tukio la juzi la wakazi wa Arusha kuamua kwenda kukesha uwanja wa NMC unga ltd.
  Nilikuwepo uwanjani mpaka saa TANO nikiwatazama watu hawa na nikawaona wanaelewa wanachokitaka na kile walichokichoka.
  Bila ya mimi kujua kumbe na mtoto wangu alikuwepo hapo uwanjani na amekesha mpaka asubuhi walipofikuzwa na polisi.
  Suala la UMEYA arusha toka mwaka jana hawa CHADEMA wanalalamika na hakuna anayewasikiliza. Waziri Mkuu ameahidi na kutoa maagizo vikao vifanyike lakini mambo yanapuuzwa, Polisi nao wanapiga watu ambao kimsingi wanadai haki kabisa tena haki ya kweli. Usiku ule wananchi hawakuwa na sime wala mapanga kisa cha kuwapiga na mabomu na kuwafukuza kwa risasi za moto hakionekani. Haki ya Mungu niliapa mwanangu angerudi nyumbani na alama ningetoka na mtu.

  ENYI CCM NYINYI, JUZI MAMBO YALINIFIKA SHINGONI, NATAMANI MFE ILA MAPENZI YA MUNGU YATIMIZWE. Arusha damu itamwagika, tena damu itamwagika. Dalili zinaonekana, watu wana hasira na CCM, mnapokonya haki ya CHADEMA wazi wazi hivi??

  Juzi kwenye hotuba ya mkesha nimemulewa sana Freeman Mbowe na Dr Slaa. Nilikuwa sijalielewa vema suala hili la Arusha kuhusu umeya na huyu OCD Zuberi Mombweji. Nilikuwa kila siku namlaumu Mbunge LEMA kuwa ni mtu wa fujo kumbe LEMA ANAZO HOJA ZA MSINGI, UKWELI NA HAKI YA WATU WA ARUSHA IMEPOKONYWA.

  Najisikia kuwa siiwezi kuvumilia ushenzi huu tena. CHADEMA PAMBANENI, HAMUWEZI KUFA, NA HAFI MTU KIPUMBAVU MAANA MNAPIGANIA HAKI. Huu ni wakati wenu kwa ajili yetu Watanzania.

  Mpaka mbunge anakubali kwenda jela ili kutoa ujumbe na watu wamefunga masikio hawasikii?? Mungu wangu naogopa maana hii ni dalili nzuri ya watu kuchukua Mapanga na sime. damu yetu na watoto wetu itakuwa mikononi mwenu CCM.

  Ole wako diwani wa CCM uliyekubali kubeba uovu huu na kuukubali UMEYA wa ubatili maana siku imefika ya ufalme wa CCM kufa kwa AIBU.

  Eeeh Mungu unirehemu mimi na nchi yangu Tanzania.
   
 2. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  dah! tanzania zaidi ya uijuavyo!
   
 3. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #3
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimeipenda. Tutapigania haki yetu kwa gharama yoyote. Kama wao wana risasi na mabomu sisi tuna nguvu ya umma. Aluta Continua CDM mpaka kieleweke. Tunataka nchi yetu
   
 4. s

  seniorita JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Poleni wana Arusha ambao mmekesha NMC; sisi tuko mbali tungekesha nanyi but tuko pamoja katika mapambano ya haki....
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Tunaitaka Tanganyika irudi mikononi mwa watanganyika
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 7. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Ni vema umepata nafasi ya ku-express feelings zako...inaonekana uko na uchungu sana

  But let me share with you these two best quotes from MLK Jr

  [FONT=&amp]"Man must evolve for all human conflict a method which rejects revenge, aggression and retaliation. The foundation of such a method is love"

  [/FONT]
  [FONT=&amp]"Nonviolence is a powerful and just weapon. which cuts without wounding and ennobles the man who wields it. It is a sword that heals.[/FONT][FONT=&amp]"[/FONT]

  [FONT=&amp]

  [/FONT]
   
 8. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Inapendeza,tusikubali kuwa madhalimu kwa kukaa kimya,uoga ni silaha ya maangamizi kwa wananchi na nchi yao.Hakuna wakuwasemea wananchi ispokuwa wananchi wenyewe wasimame for their rights.Unafiki umepigiwa kelele mpaka kwenye vitabu vitakatifu.suala la mh.Lema si la kutafuta umaarufu.watu wananshindwa kuelewa kuwa naye ni mwananchi wa Arusha,ni raia wa Tanzania ana haki kama walivyo Watanzania wengine,ubunge ni dhamana tu,amethubutu anaweza kuwatetea wanyonge kwa maneno na vitendo.Tunaamini kukaa kwake gerezani ni ishara ya ushindi dhidi ya madhalimu waliokubuhu katika nchi yetu,kama umaarufu tayari alikwisha kuwa maarufu alipokataa kuwa mnafiki na kuwapigania wananchi kwa hali na mali bila ubaguzi wala itikadi za uvyama.Tatizo wanashindwa kuelewa hawa CDM ni kuwa ni raia na wana haki kama raia wengine.Nawasihi wana wa Arusha kuwa ninyi si kichaka cha kuhifadhi uonevu,ukandamizaji na udhalimu katka nchi hii,mna historia katika mapambano ya kupigania utu wa Mtanzania.Kumbukeni Azimio la Arusha lilitangazwa Arusha lilijali misingi bora ya utu,hii in nafasi adimu kupata tena fursa hii kupinga udhalimu unaofanywa wazi bila kificho kwa kupora haki za wana wa Arusha,msikubali kupora haki ya kujichagulia viongozi wenu muwatakao,haki ya kujiamulia mambo yenu na kupanga mipanago yenu ya kimaendeleo bila kuingiliwa na walevi wa madaraka.Mungu amewapa nafasi hii tena kuhakikisha haki na batili hazishikamani kamwe.Aluta Continua MAPAMBANO NDO KWANZA YANASHIKA KASI,hakuna kulala mpk kionekane kimeeleweka,tutasema kweli daima fitina kwetu mwiko
   
Loading...