ccm acheni kuwatisha wananchi


H

HIMO

Member
Joined
Aug 31, 2012
Messages
76
Likes
4
Points
0
H

HIMO

Member
Joined Aug 31, 2012
76 4 0
Ndugu wanabodi!
Nikiwa kama mtanzania na mwananchi mpenda maendeleo kamwe sitopenda kuona hiki chama kinachoitwa ccm kinatumia udhaifu wa uelewa mdogo na upembuzi wa kauli mbalimbali za viongozi hawa wa ccm kwa watanzania waliowengi hasa walioko vijijini,
ndugu wanabodi!
Miongoni mwa kauli ambazo zinatumika ama kwa makusudi waliojiwekea au kama nilivyoandika hapo mwanzo kuwa ni uelewa mdogo wa watanzania ni hii isemayo kuwa watanzania wasipoichagua ccm NCHI ITAINGIA VITANI,kauli imekuwa ikitumika vibaya na hata jana mwenyekiti wa uvccm amelitamka akiwa kisarawe na hata alipokuwa mwenge alitoa matamshi kama hayo.Nape na wenzake ndiyo usiseme,
Sasa hebu tuone mantiki ya kauli hii na nyinginezo ambazo zimekuwa zikitolewa,
Yawezekana ikawa ni propaganda ili kuwatisha wananchi lakini ukiingia kwa undani zaidi utaona kuwa ccm ndiyo watakaoanzisha vita dhidi ya wale wote wanaoonekana kuwapinga,kwa mfano ccm wamekuwa wakilitumia jeshi la polisi kuvuruga matokeo ya chaguzi na pia matokeo,sasa katika mazingira hayo watu wanaweza kujibu mapigo kwa kuanzisha mapambano na polisi hivyo kupelekea vita kutokea,

Ukifuatilia maeneo ambayo wananchi wamepata uelewa mkubwa(political conscious)ccm wamekuwa wanatumia nguvu kubwa hasa jeshi la polisi kwa mfano,nyamagana na shinyanga mjini 2010 ambapo msimamizi wa uchaguzi alitoa matokeo baada ya siku tatu ambapo ccm walikuwa wanataka wao watangazwe wameshinda wananchi waliposiposimama kidete na kufanya maandamano makubwa matokeo yakatoka,hii maana yake ni kuwa ccm wapo tayari watu wafe lakini waongoze,kwa hiyo viongozi wanapozunguka nchi nzima kuwatangazia watanzania kuwa wakichagua vyama vingine nchi itaingia vitani maana yake hawako tayari kuachia nchi hata watu wakifa.
Nchi zilizoendelea hufanya uchaguzi na kupata viongozi wapya na vyama vipya ili kuja na mawazo mapya mwisho wa siku wananchi wanapata maendeleo,kwa ilivyo sasa viongozi na chama twawala kimekosa ubunifu na kimebaki kuiga iga tu sera za jamaika na thailand hasa brn kilimo kwanza,nk
nawasilisha.
 
masanjasb

masanjasb

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Messages
2,364
Likes
20
Points
135
masanjasb

masanjasb

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2011
2,364 20 135
Umesema kitu muhimu sana mkuu,ccm ndiyo watakaingiza nchi yetu vitani na sio vyama vya upinzani,nashukuru tu wananchi wamekuwa waelewa wanapuuza kauli za kijima za maccm.

Kila mkutano wa ccm unapofanya uwe wa kata au kijiji,wahutubiaji wengi hutumia kauli za kidini na kikanda kuzima hoja za upinzani hili nimelishuhudia mwenyewe kwa macho yangu.
 

Forum statistics

Threads 1,252,246
Members 482,057
Posts 29,801,536