CCM acheni kutumia Bunge kuzungumzia matatizo yenu ya ndani ya chama

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,031
2,000
Wakuu, nimekuwa nafuatilia mijadala inayoendelea huko Bungeni. Ukisikiliza kwa makini utagundua ni mijadala ambayo ingetakiwa kufanyika ndani ya Chama. Bungeni ni sehemu ya kuongelea mambo yaliyo ya maslahi mapana ya taifa hususani utungaji wa sheria, kurekebisha sheria mbalimbali na kuisimamia serikali.

Najua kuna moto unafukuta huko chini kwa chini kati ya kambi mbili na wanajaribu kuuzima kabla hawajafika katika vikao vya chama ila mimi nasema kutumia rasilimali za nchi hususani taasisi kubwa kama BUNGE kuongelea na kujaribu kutatua tofauti zao siyo jambo sahihi kabisa. Wananchi wengi tu hawana maslahi wala ushabiki na Chama Cha Mapinduzi na wengi tu hawajali hata hiko chama kingejifia leo hii.

Hili linaloendelea halikubaliki!
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
10,815
2,000
Bunge ni sehemu ya chama chao.

Ni mwanzo wa mwisho wa chama hicho, anguko laja.
 

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,031
2,000
Kingine, kueneza propaganda kwa kuwatumia hawa kina Harmonize na Rayvanny kama DIVERSION kuwapumbaza watanzania hasa vijana ili wasijue mambo muhimu yanayoendelea katika taifa lao nalo si jambo sahihi. Sisi wenye jicho la tatu haya mambo tunayajua sana yanavyofanya kazi.

Halafu kesho mnakuja kulalamika kuwa vijana hawajui kitu kuhusu taifa lao!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom