CCM acheni kumpamba zito ni msaliti aliyekubuhu.

Status
Not open for further replies.

12STONE

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
1,109
1,475
CCM mnafanya makosa makubwa tena kwa makusudi huku mmekodoleana Macho bila ya kukosoana ninyi kwa ninyi kwa kuambiana ukweli.

Zito ni mwana CCM tangu lini? Ndani ya CHAMA CHA MAPINGUZI wapo vijana akina Nape Nnauye,January Makamaba,Riziwani Kikwete na wengine wengi.

Kwanini kumtukuza Zito msaliti kana kwamba Anayoyafanya ndani ya CHADEMA ni mema.

Kwa mfano wa Nchi ya England ccm jifunzeni,Inapotokea mchezaji mzawa anafanya vizuri kwenye Team yao ya Taifa watamtukuza kwenye vyombo vya habari mpaka kila mtu atajua kuna mchezaji wa Uingereza ameibuka siku hizi,hata kama uwezo wake sio wa kiwango cha juu kiasi hicho watampamba bila kukoma.

Chako ni chako tu hata kama kina chongo.CCM pambeni makada wenu,Mwacheni Zito aubebe mzigo wake mwenyewe ili wananchi wamuone jinsi atakavyoutua itakuwaje.

Kwenye mitandao ya Kijamii Makada wa ccm wanamtukuza Zito sana kuliko vijana wao.Hii ni aibu kubwa sana kwa chama Tawala.

Anawafaa kwa lipi kama sio kusema kwa matendo yenu CCM Mnatoa ujumbe kwa Watanzania wote Zito ni Mateka wenu? Na mpango mliomtuma hajaukamilisha na mbinu yenu chafu imebainika.Hilo hamkulitegemea kama litatokea,Kwenu limekuwa ni Jambo la Kuwashangaza ama Kuwaduwaza.


Ukitaka kujua ZZK ni Msaliti aliyekubuhu wee ona jinsi anavyofanya Mikutano yake.

Kama kweli Zito yuko Pamoja Viongozi wake kiutendaji Kwanini asiambatane nao kwenye mikutano.

Watu wawili hawezi kutembea pamoja pasipo kuwa na nia moja.Zito ni Muasi ndani ya chama Anastahili kufukuzwa kabisa.

Wewe Katibu wako Mkuu wa chama amepita kufanya mkutano Mkoa A naye bila aibu unafanya mkutano Mkoa huo huo.HUO SIO UASI NINI?

Mwisho wa Zito ndani ya Chadema lazima uwe mbaya tu. Hata kama CHADEMA Wangekuwa na mawazo ya kumvulia sasa mwenendo wake wauvulijki tena.Lazima Watamfire tu. Wengi tulitarajia wakati huu ndio Zito angeutumia kwa kutulia ili kila mmoja ajue kweli huyu kijana ni mwanasiasa makini.

Mbona Kitila Mkumbo kanyamaza kimya na wote wako na tuhuma moja?

Kwa jinsi unavyoenda tunazidi kubaini wewe kweli ni Msaliti maana kwenye Maji matamu (soft water) huwezi kupata maji machungu (hard water). Kijana sasa anapandikiza sumu kwa wanachama na raia kwa ujumla. KAMA INAWAUMA CCM MCHUKUENI MSALITI ILI MKAMPAMBE MNAVYOWEZA HUKO HUKO MTAA WA LUMUMBA .
 

manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
3,536
2,000
hao CCM Zito kala vyao na wao hawawezi kumacha salama lazima wamteketeze kabisa katika Siasa ili asije leta madhara kwa chama chao baadae, na litakalofuata ni kumkaribisha CCM ili awekwe benchi kama Masumbuko Lamwai , Msabaha n.k Pole Zito , hili linafanyika ili utabili utimie kwamba mwaka 2015 ndo mwisho wa CCM LAKINI KABLA YA HAPO wata karibisha kirusi hatari kutoka upinzani kitakachovuruga kabisa chama.
 

12STONE

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
1,109
1,475
Kumshabikia Zito peke mpaka dakika hii CCM watajutia hilo,Mkumchukua mtalia na kusaga meno.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom