CCM acheni kufanya biashara ya elimu, nchi hii ni yetu wote

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,975
2,000
Chama cha Mapinduzi Manyara kimeshauri CCM nchi mzima ianzishe biashara ya shule za Jumuiya ya Wazazi! Elimu haitakiwi kufanywa biashara tena na chama kilichopo madarakani, taswira inayoonekana ni kuwa vyama vitakuwa vinanyang'anya ushindi wa uchaguzi mkuu ili viweze kufanya biashara ya elimu! Na huenda ndicho kilichofanyika uchaguzi uliopita.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,221
2,000
Hela za ruzuku zinawawashawasha... wanaweza kufanya wakitaka maana ni mabilion ya shilling mengi watapata kila. Mwezi baada ya kufanikiwa kuua upinzani nchini kwa hila
 
mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,013
2,000
Ndani ya muda wa miaka miwili toka sasa, yaani ifikapo mwaka 2022 kuelekea 2023 ndipo Watanzania watakapo elewa umuhimu wa vyama vya upinzani. Watawala waliokosa maono wataanza kutafuta kila aina ya kisingizio cha kushindwa kutekeleza ilani ya chama chao.

Nafasi ya kumtafuta mrithi wa aliyepo madarakani kwa hivi sasa itakuwa ni mwiba mkali kwao. Na kwa haiba na hulka zake za kiuongozi ni lazima patatokea patashika nguo kuchanika. Hii si ramli chonganishi isipokuwa ni jambo lenye kusubiri wakati wake maalum wa kufikia utimilifu wote.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Hamiyungu

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
426
500
Chama cha Mapinduzi Manyara kimeshauri CCM nchi mzima ianziishe biashara ya shule za Jumuia ya Wazazi! Elimu haitakiwi kufanywa biashara tena na chama kilichopo madarakani, taswira inayoonekana ni kuwa vyama vitakuwa vinanyang'anya ushindi wa uchaguzi mkuu ili viweze kufanya biashara ya elimu! Na huenda ndicho kilichofanyika uchaguzi uliopita.

Mbona shule za jumuia ya wazazi wa CCM zipo siku nyingi sana!?hazijaanza leo....TEGETA SECONDARY, SANGU SECONDARY, META SEC na nyingine nyingi ni baadhi ya shule za jumuia ya wazazi wa CCM.
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,975
2,000
Mbona shule za jumuia ya wazazi wa CCM zipo siku nyingi sana!?hazijaanza leo....TEGETA SECONDARY,SANGU SECONDARY,META SEC na nyingine nyingi ni baadhi ya shule za jumuia ya wazazi wa CCM.
Mimi ninaijua vizuri Meta nilisoma hapo ikiwa Middle School shule ya serikali ila cha ajabu CCM waliipora, Sangu pia haikuwa ya CCM na ilianzia karibuni ya kanisa la Anglikana, shule ya wazazi TAPA ilikuwa mabatini karibuni ya hosipitali, CCM ilichukua baadhi ya shule zilizokuwa za halmashauri ya serikali za mitaa kama ilivyopora viwanja vya mpira. CCM kuigeuza elimu kuwa kitegauchumi ni kutoelewa wajibu wao wa uongozi kwani wataua shule za serikali ili zao zipate wanafunzi, pia watang'ang'ania madaraka kwa halinamali ili kulinda biashara yao.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
44,668
2,000
Chama cha Mapinduzi Manyara kimeshauri CCM nchi mzima ianzishe biashara ya shule za Jumuiya ya Wazazi! Elimu haitakiwi kufanywa biashara tena na chama kilichopo madarakani, taswira inayoonekana ni kuwa vyama vitakuwa vinanyang'anya ushindi wa uchaguzi mkuu ili viweze kufanya biashara ya elimu! Na huenda ndicho kilichofanyika uchaguzi uliopita.
Tangu lini CCM ikawa na nia njema na watanzania?
 
Mulokozijr12

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
2,041
2,000
Jumuiya ya wazazi CCM ina shule zake toka siku nyingi sana ndugu, binafsi ni matunda ya shule hizo nikiwa nimesoma Lomwe High School, Usangi, Mwanga,Kilimanjaro.

Hakika CCM ni chama cha mfano Tanzania nawashukuru kwa elimu nzuri waliyonipatia.
 
residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
3,814
2,000
Jumuiya ya wazazi CCM ina shule zake toka siku nyingi sana ndugu, binafsi ni matunda ya shule hizo nikiwa nimesoma Lomwe High School, Usangi, Mwanga,Kilimanjaro.

Hakika CCM ni chama cha mfano Tanzania nawashukuru kwa elimu nzuri waliyonipatia.
Muathirika wa ujinga wa elimu ya CCM unashukuru kwa kufanywa mjinga!
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
11,465
2,000
Chama cha Mapinduzi Manyara kimeshauri CCM nchi mzima ianzishe biashara ya shule za Jumuiya ya Wazazi! Elimu haitakiwi kufanywa biashara tena na chama kilichopo madarakani, taswira inayoonekana ni kuwa vyama vitakuwa vinanyang'anya ushindi wa uchaguzi mkuu ili viweze kufanya biashara ya elimu! Na huenda ndicho kilichofanyika uchaguzi uliopita.

Serikali ya CCM imeshagundua kosa lililofanyika hadi elimu kuwa biashara, tena biashara inayojenga matabaka kwenye jamii.
Kazi ya kumshughulikia hili inaendelea vizuri.... elimu bora ni haki ya kila mtanzania
 
mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
6,167

Hivi kile Chuo kikuu cha siasa na propaganda cha ccm kule kwa mfipa,,kinatoa course gani?
Au ni siasa tu?
Na wakisema propaganda wanamaanisha nn?

Kweli siasa ni uongo mtupu.
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
11,465
2,000
Waliochagua kufanya biashara ya elimu wajitafakari upya kama ni biashara sahihi na biashara endelevu kwao
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,975
2,000
Hivi kile Chuo kikuu cha siasa na propaganda cha ccm kule kwa mfipa,,kinatoa course gani?
Au ni siasa tu?
Na wakisema propaganda wanamaanisha nn?

Kweli siasa ni uongo mtupu.
Ni mchinamchina, CCM inalenga kutawala vilaza ikipiga vita elimu, ujinga wetu ndiyo fahari kwa CCM.
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,975
2,000
Tangu lini CCM ikawa na nia njema na watanzania?
Polepole alisema CCM itatawala zaidi ya miaka 90 ijayo akijua ajenda iliyoko ndani mwao huu us elimu isiyokidhi viwango ambavyo itawezesha kuwa na taifa la vilaza wanaotawalika kirahisi.
 
At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
3,594
2,000
Polepole alisema CCM itatawala zaidi ya miaka 90 ijayo akijua ajenda iliyoko ndani mwao huu us elimu isiyokidhi viwango ambavyo itawezesha kuwa na taifa la vilaza wanaotawalika kirahisi.
Kwani lazima usome shule za CCM!?
 
smaki

JF-Expert Member
Jan 23, 2019
2,224
2,000
Serikali ya CCM imeshagundua kosa lililofanyika hadi elimu kuwa biashara, tena biashara inayojenga matabaka kwenye jamii.
Kazi ya kumshughulikia hili inaendelea vizuri.... elimu bora ni haki ya kila mtanzania
matabaka hayakosi hata mbinguni yako makelabi na maserafi hawawezi kuwa sawa na malaika wengine. House boy hawezi lalia kitanda chako hata km haupo mwaka mzima labda aibie ibie.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom