Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,724
- 239,332
Wakuu natanguliza salamu za pasaka,
Baada ya salamu naweka wazi ukweli ambao kuna wanaotaka ufichwe, CCM haikushinda umeya Tanga mjini na wala haikushinda uchaguzi mkuu eneo hilo.
Waachieni washindi ambao ni UKAWA kupitia CUF wamsimike meya maana walishinda ubunge na viti vingi vya madiwani, huyo mkurugenzi anayetaka kuwabeba atakuja kuwaumbua siku si nyingi.
Zipo taarifa kwamba mnataka kulivunja baraza la madiwani katika ile mbinu ya kishamba ya TUKOSE WOTE, lakini wananchi hawatakubali na mtaitambua nguvu ya umma.
Muungwana ni vitendo na asiyekubali kushindwa si mshindani, itisheni upya uchaguzi wa meya na washindi watangazwe.