CCM acha kuifuatafuata CHADEMA, bali waiache imalizane na madiwani wake Arusha - Malisa

ESAM

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,163
546
Inaonekana wamekumbuka shuka kukiwa asubuhi kwamba wantmia muda mwingi kupambana na Chadema kumbe wanaijenga wakati inazidi kupaa wao wanadidimia. Soma hapa chini kwa undani:

- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -

Waandishi wetu, Arusha
KAIMU Mwenyekiti wa Umoja Vijana wa CCM (UVCCM), Benno Malisa amewataka vigogo ndani ya chama hicho tawala kuacha kuingilia mambo ya chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema hasa mgogoro wake na madiwani wa Arusha Mjini na badala yake watafute suluhu ya matatizo ya msingi yanayoikabili nchi kama mfumuko wa bei na tatizo la ajira.Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Hospitali ya Mtakatifu Thomas, Malisa alisema wapo baadhi ya watu ndani ya CCM ambao siyo wana Chadema lakini wamekuwa wakijihusisha na mgogoro wa chama hicho pinzani.

Alisema wana CCM hao wamekuwa wakiingilia mgogoro kati ya Chadema na madiwani wake ambao tayari chama hicho kilikwishaamua kuwafukuza na kusisitiza kuwa mambo ya chama hicho pinzani yaachwe yasiingiliwe.

Kauli hiyo ya Malisa inakuja kipindi ambacho Chadema kimekuwa kikilalamikia baadhi ya mawaziri wa Serikali kupuuza uamuzi wake wa kuwatimua madiwani wake.

Chadema imewahi kumnyooshea kidole Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi,) George Mkuchika kwamba alikuwa na ajenda ya siri baada ya kuendelea kuwatambua madiwani hao.

Pia Chadema kimekuwa kikituhumu baadhi ya makada wa CCM mkoa wa Arusha na taifa, kujaribu kuingilia uamuzi huo wa Chadema wa kutimua madiwani hao kutokana na uamuzi wao wa kuingia muafaka wa Umeya wa Arusha.

Kaimu Mwenyekiti huyo wa UVCCM, alisema si sahihi kwa CCM kutumia hata vyombo vya serikali kudhoofisha demokrasia kwa vyama vya upinzani akionya kwamba
mwisho wa siku matokeo yake hayatakuwa mazuri kwa taifa.

Alisema demokrasia inapaswa kuachwa ichanue kwa vyama vya upinzani ili kujenga ustawi mzuri wa nchi.

"Nitumie nafasi hii kumuomba Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), kaka yangu (Godbless) Lema kuwa mstari wa mbele katika kuleta umoja na mshikamano hapa mjini na kumaliza tofauti za UCCM na UCDM (U - Chadema) ili wakazi wa Arusha wapate maendeleo. Sasa uchaguzi umekwisha tujenge nchi yetu."

Alisema CCM kinapitia katika wakati mgumu hivi sasa na kuonya kwamba badala ya kuisimamia Serikali wapo wanaohangaika kutafuta wachawi na kutuhumu watu.
"Tuache kabisa. Hili jambo halisaidii chama wala taifa letu, kumekua na dhana na fikra potofu juu ya ushindi wetu wa 2010 matokeo yale na tuliyoyaona Igunga ni funzo kwetu na hasa vijana," na kuongeza kuwa vijana wengi wameanza kukosa imani na CCM kwa sababu:

"Tunashindwa kuwaonyesha kuwa tuna majibu ya matatizo yao. Tumebaki tunaimba historia na kumtaja Baba wa Taifa na kutumia nukuu zake bila kuwapa matumaini vijana kuwa Tanzania yao itakua njema, watapata elimu nzuri, afya na itakua ya uhakika."

Alisema vijana wanataka kusikia uchumi umekua, ajira zinapatikana, fursa za kujiajiri zipo, mikopo inapatikana na kusisitiza: "Tusipotoa matumaini haya na kuyafikia 2015, wapiga kura milioni sita wapya watatukataa, uelewa wa vijana wa Kitanzania sasa umekua mkubwa. Wanajua haki na wajibu wao tuache kufanyia siasa maisha ya Watanzania."

Wanaotaka urais 2015
Akizungumzia mbio za urais kwa mwaka 2015 ndani ya CCM, Malisa aliwataka makada wa chama hicho wanaotaka kuwania nafasi hiyo kuacha kuwagawa vijana na kuvuruga chama akisema kufanya hivyo ni hatari kwa uhai wa chama.

"Wapo baadhi ya watu wanaopita wenzangu msiishi kwa kutarajia madaraka ya kupewa wapo wengine wanapita wanakusanya CV za vijana na kuwaahidi vyeo vya U-DC. Msipotoshwe na wala msifungwe fikra kwa sababu mmepewa ahadi ya kuteuliwa U DC. Tuna bahati mbaya wapo ambao mpaka leo wanaishi kwa kusubiri U DC wamegeuka kuwa ndiyo mzee na watumwa kifikra, tuukatae utumwa huu UVCCM."

"Tusiwe ndiyo mzee. Nawaagiza wenyeviti na makatibu wa mikoa na wilaya zote Tanzania, wafuatilie katika halmashauri zao kujua mipango ya maendeleo inayohusu vijana na kufuatilia utekelezaji wake wakiona hakuna utekelezaji, watumie kamati za siasa za wilaya kuwabana wenyeviti wa halmashauri. Nazitaka wilaya zote zifuatilie zituletee taarifa juu hili jambo. Tusikubali kuwa ndiyo mzee lazima tusimamie maslahi ya Vijana."
Alisema huu si wakati Serikali ya CCM kukaa likizo badala yake ifikirie namna ya kufikia matarajio ya Watanzania.

Dowans
Akizungumzia suala la mitambo ya Dowans Malisa alisema: "Watu waliosababisha hasara wawajibike, walitudanganya. Kama taifa leo tumeshindwa kesi mitambo ile waliyosema haifai leo inatumika na kampuni ya Symbion. Wanatufanya Watanzania mazuzu. Walisema heri tukae giza wakati wao wanatumia majenereta na wanalipiwa na Serikali huku wakinunua aspirini kwa mamilioni."

"Leo wanajifanya wazalendo. Nilitarajia wawajibike walidanganya taifa, Serikali ikavunja mkataba. Wakasema mitambo haifai mibovu leo imenunuliwa na Wamarekani na wanatuuzia umeme... wanafiki wametufikisha hapa niwaombe UVCCM na vijana wa vyama vyote tuungane hawa wawajibike."

Watunishiana misuli na polisi

Kabla ya kuhutubia, Malisa na msafara wake waliingia katika mgogoro na vyombo vya dola, baada ya kufanya maandamano na mikutano ya uzinduzi wa matawi mapya ya UVCCM ambayo awali, yalizuiwa na polisi kabla ya kuruhusiwa baadaye.

Mamia ya vijana wa CCM walianza kukutana kuanzia asubuhi katika Ofisi za UVCCM mkoani hapa, lakini walipoanza matembezi walizuiwa na polisi mbele ya Jengo la CCM Mkoa.
Sababu ya kuzuiwa inaelezwa kuwa ni mgogoro ndani ya chama hicho katika Wilaya ya Arusha. Viongozi wa umoja huo wanadaiwa kupinga ziara ya viongozi hao wa kitaifa. Hata hivyo, maandamano hayo yaliendelea baada ya mazungumzo baina ya polisi na viongozi hao wa UVCCM huku wakikubaliana njia za kupita.

Lakini, mara baada ya kukamilika kwa uzinduzi wa matawi hayo viongozi wa umoja huo walionyesha kukerwa kwao na hatua ya polisi na baadhi ya viongozi wa chama hicho kutaka kuzuia kazi hiyo.

Inaonekana wamekumbuka shuka kukiwa asubuhi kwamba wantmia muda mwingi kupambana na Chadema kumbe wanaijenga wakati inazidi kupaa wao wanadidimia. Soma hapa chini kwa undani:

- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -

Waandishi wetu, Arusha
KAIMU Mwenyekiti wa Umoja Vijana wa CCM (UVCCM), Benno Malisa amewataka vigogo ndani ya chama hicho tawala kuacha kuingilia mambo ya chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema hasa mgogoro wake na madiwani wa Arusha Mjini na badala yake watafute suluhu ya matatizo ya msingi yanayoikabili nchi kama mfumuko wa bei na tatizo la ajira.Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Hospitali ya Mtakatifu Thomas, Malisa alisema wapo baadhi ya watu ndani ya CCM ambao siyo wana Chadema lakini wamekuwa wakijihusisha na mgogoro wa chama hicho pinzani.

Alisema wana CCM hao wamekuwa wakiingilia mgogoro kati ya Chadema na madiwani wake ambao tayari chama hicho kilikwishaamua kuwafukuza na kusisitiza kuwa mambo ya chama hicho pinzani yaachwe yasiingiliwe.

Kauli hiyo ya Malisa inakuja kipindi ambacho Chadema kimekuwa kikilalamikia baadhi ya mawaziri wa Serikali kupuuza uamuzi wake wa kuwatimua madiwani wake.

Chadema imewahi kumnyooshea kidole Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi,) George Mkuchika kwamba alikuwa na ajenda ya siri baada ya kuendelea kuwatambua madiwani hao.

Pia Chadema kimekuwa kikituhumu baadhi ya makada wa CCM mkoa wa Arusha na taifa, kujaribu kuingilia uamuzi huo wa Chadema wa kutimua madiwani hao kutokana na uamuzi wao wa kuingia muafaka wa Umeya wa Arusha.

Kaimu Mwenyekiti huyo wa UVCCM, alisema si sahihi kwa CCM kutumia hata vyombo vya serikali kudhoofisha demokrasia kwa vyama vya upinzani akionya kwamba
mwisho wa siku matokeo yake hayatakuwa mazuri kwa taifa.

Alisema demokrasia inapaswa kuachwa ichanue kwa vyama vya upinzani ili kujenga ustawi mzuri wa nchi.

“Nitumie nafasi hii kumuomba Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), kaka yangu (Godbless) Lema kuwa mstari wa mbele katika kuleta umoja na mshikamano hapa mjini na kumaliza tofauti za UCCM na UCDM (U - Chadema) ili wakazi wa Arusha wapate maendeleo. Sasa uchaguzi umekwisha tujenge nchi yetu.”

Alisema CCM kinapitia katika wakati mgumu hivi sasa na kuonya kwamba badala ya kuisimamia Serikali wapo wanaohangaika kutafuta wachawi na kutuhumu watu.
“Tuache kabisa. Hili jambo halisaidii chama wala taifa letu, kumekua na dhana na fikra potofu juu ya ushindi wetu wa 2010 matokeo yale na tuliyoyaona Igunga ni funzo kwetu na hasa vijana,” na kuongeza kuwa vijana wengi wameanza kukosa imani na CCM kwa sababu:

“Tunashindwa kuwaonyesha kuwa tuna majibu ya matatizo yao. Tumebaki tunaimba historia na kumtaja Baba wa Taifa na kutumia nukuu zake bila kuwapa matumaini vijana kuwa Tanzania yao itakua njema, watapata elimu nzuri, afya na itakua ya uhakika.”

Alisema vijana wanataka kusikia uchumi umekua, ajira zinapatikana, fursa za kujiajiri zipo, mikopo inapatikana na kusisitiza: “Tusipotoa matumaini haya na kuyafikia 2015, wapiga kura milioni sita wapya watatukataa, uelewa wa vijana wa Kitanzania sasa umekua mkubwa. Wanajua haki na wajibu wao tuache kufanyia siasa maisha ya Watanzania.”

Wanaotaka urais 2015
Akizungumzia mbio za urais kwa mwaka 2015 ndani ya CCM, Malisa aliwataka makada wa chama hicho wanaotaka kuwania nafasi hiyo kuacha kuwagawa vijana na kuvuruga chama akisema kufanya hivyo ni hatari kwa uhai wa chama.

“Wapo baadhi ya watu wanaopita wenzangu msiishi kwa kutarajia madaraka ya kupewa wapo wengine wanapita wanakusanya CV za vijana na kuwaahidi vyeo vya U-DC. Msipotoshwe na wala msifungwe fikra kwa sababu mmepewa ahadi ya kuteuliwa U DC. Tuna bahati mbaya wapo ambao mpaka leo wanaishi kwa kusubiri U DC wamegeuka kuwa ndiyo mzee na watumwa kifikra, tuukatae utumwa huu UVCCM.”

“Tusiwe ndiyo mzee. Nawaagiza wenyeviti na makatibu wa mikoa na wilaya zote Tanzania, wafuatilie katika halmashauri zao kujua mipango ya maendeleo inayohusu vijana na kufuatilia utekelezaji wake wakiona hakuna utekelezaji, watumie kamati za siasa za wilaya kuwabana wenyeviti wa halmashauri. Nazitaka wilaya zote zifuatilie zituletee taarifa juu hili jambo. Tusikubali kuwa ndiyo mzee lazima tusimamie maslahi ya Vijana.”
Alisema huu si wakati Serikali ya CCM kukaa likizo badala yake ifikirie namna ya kufikia matarajio ya Watanzania.

Dowans
Akizungumzia suala la mitambo ya Dowans Malisa alisema: “Watu waliosababisha hasara wawajibike, walitudanganya. Kama taifa leo tumeshindwa kesi mitambo ile waliyosema haifai leo inatumika na kampuni ya Symbion. Wanatufanya Watanzania mazuzu. Walisema heri tukae giza wakati wao wanatumia majenereta na wanalipiwa na Serikali huku wakinunua aspirini kwa mamilioni.”

“Leo wanajifanya wazalendo. Nilitarajia wawajibike walidanganya taifa, Serikali ikavunja mkataba. Wakasema mitambo haifai mibovu leo imenunuliwa na Wamarekani na wanatuuzia umeme... wanafiki wametufikisha hapa niwaombe UVCCM na vijana wa vyama vyote tuungane hawa wawajibike.”

Kuna mwenye taarifa au ufahamu wowote wa kitu gani UVCCM imewafanyia au kuwasaidia/kusaidiana na vijana wa nchi yetu zaidi tu ya siasa za majukwaani na mishati yao ya kijani na maskafu shingoni?
 
Aisee, huyu jamaa sasa kathibitisha rasmi kumbe huwa wanaahidiana vyeo vya U-DC ili wawe ndiyo mzee, ili wafikiri kwa kutumia tumbo badala ya vichwa. Kumbe Tanzania inahitaji mabadiliko makubwa ya kifikira hasa kwa wananchi ili wawachague viongozi wenye maono sahihi kwa Tanzania.
 
uelewa wa vijana wa Kitanzania sasa umekua mkubwa. Wanajua haki na wajibu wao tuache kufanyia siasa maisha ya Watanzania.
Poor CCM, a sinking boat!
Hivi mwenyekiti wa UVCCM ni nani? Naona kuna makamu na katibu.
 
Aisee, huyu jamaa sasa kathibitisha rasmi kumbe huwa wanaahidiana vyeo vya U-DC ili wawe ndiyo mzee, ili wafikiri kwa kutumia tumbo badala ya vichwa. Kumbe Tanzania inahitaji mabadiliko makubwa ya kifikira hasa kwa wananchi ili wawachague viongozi wenye maono sahihi kwa Tanzania.

Sasa mambo wakati mwingine yanakuwa tofauti..... nasikia zambia marafiki wa banda walipoona mambo yake sio mazuri, wakaanza kujikomba kwa sata, Mzee sata kawatosa wote, anateua wasomi na wale waliwekwa pembeni kwa hira ndio viongozi kwa sasa...... siasa za makundi zina mweisho mbaya sana
 
wametafutia njia ya kujia arusha,ngoja wakanyagane wanafikiri arusha ni sawa na pwani?
malaria(ccm) haikubaliki arusha.
 
hawana jipya hawa, huku ndio kumejaa watoto wa vigogo wanao andaliwa kuwa viongozi mie mtoto wa kapuku sina changu, tumeshafahamu na kuamka na kuja mkombozi wa kweli wa watz ni nani.

Anasema watu wasiishi kwa matumaini ya kupewa nafasi, mbona yeye kufika hapo ni kwa matumaini na kubebwa na Rizone?au anatufanya hatujui?
 
nimeipenda hotuba yake, nampongeaza , kumbe ndani ya ccm bado kuna watu wenye akiri timamu,? safi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom