Uchaguzi 2020 CCM 2020: Mambo yazidi kunoga, kipyenga chapulizwa rasmi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,376
217,435
maneno matupu hayavunji mfupa

IMG-20190519-WA0000.jpg
 
Baada ya Mkapa Taifa letu halijawahi tena kuwa na viongozi wanaoweza kujieleza, hasa kuelezea wanachokifanya.

Nakumbuka kuna siku moja pale dodoma, Com walikuwa wanasheherekea moja ya annivesaries zao, Rais Kikwete akawaambia wanaccm wasiwe wanyonge, watembee vifua mbele kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya nne.

Siku hiyo yeye mwenyewe kikwete hakuweza kuelezea hayo mafanikio ni yepi?

Magufuri nae hawezi, yaani yuko bizeeeee lakini hawezi kusema serikali yake imefanya nini, nasikia kabeba wateule wake wakaione SGR hahahahaha nadhani ili waje watuambie wananchi kwa inajengwa.

Kumuambia mtu mwenye njaa, ambaye tayari ameishaanza kuamini kwamba hiyo njaa umemsababishia wewe kwamba unajenga SGR ni kazi ngumu sana, inahitaji busara na hekima katika uelewa , uelezaji na uongo.

Sasa hata huyu membe, hajui kujieleza, membe ni kama samaki ukimtoa majini anakufa. Yeye anajua sana mambo ya mahusiano ya kimataifa, ukimsikia anazungumzia mambo hayo utatamani angekuwa mjomba wako.

Sielewagi alifikaje top 3 ya ccm 2015,hahahaha nadhani 2015 kigezo vya mgombea wa ccm vilihusisha mgombea ni lazima awe na kiwango fulani cha ujinga hahaha sababu kama membe, Mheshimiwa Rais na yeye, na hajabadirika mpaka leo, ukimtoa kwenye mabarabara na madaraja na yeye ni kama samaki nchi kavu. Nisimzungumzie mama samia sababu dhana ya wanawake wakiwezeshwa wanaweza inaeleweka vizuri tu.

Wote tunaona mapungufu ya rais katika mambo ya sheria na utawala bora, mambo makubwa kabisa ya kikatiba, hahahaha korosho, bureau we changes, makinikia n.k

Wasiwasi wangu membe nae ni mtu wa hivi, sasa Mimi 2020 ntapiga kura kisayansi zaidi, najua Haito count lakini huwezi jua, ntapiga kisayansi, nimejifunza mambo mengi sana siku za hivi karibuni hasa mambo ya kisiasa, sio ya kuyaangalia kwa darubini moja tu, toka lowassa arudi ccm mpaka kufikia rostam azizi kuwa political analyst, ni darasa kubwa.
 
Yote haya kayataka Jiwe na roho yake ya korosho/mbaya, tamaa yake ya kuzitaka pesa za wanyonge wa korosho, imemletea laana kubwa na kumuondolea thamani mbele ya watu wa kanda ya pwani na kusini. Mvua hizi watu wananjaa kweli na korosho zao zinaoza magharani. #MembeRais2020
 
Baada ya Mkapa Taifa letu halijawahi tena kuwa na viongozi wanaoweza kujieleza, hasa kuelezea wanachokifanya.

Nakumbuka kuna siku moja pale dodoma, Com walikuwa wanasheherekea moja ya annivesaries zao, Rais Kikwete akawaambia wanaccm wasiwe wanyonge, watembee vifua mbele kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya nne.

Siku hiyo yeye mwenyewe kikwete hakuweza kuelezea hayo mafanikio ni yepi?

Magufuri nae hawezi, yaani yuko bizeeeee lakini hawezi kusema serikali yake imefanya nini, nasikia kabeba wateule wake wakaione SGR hahahahaha nadhani ili waje watuambie wananchi kwa inajengwa.

Kumuambia mtu mwenye njaa, ambaye tayari ameishaanza kuamini kwamba hiyo njaa umemsababishia wewe kwamba unajenga SGR ni kazi ngumu sana, inahitaji busara na hekima katika uelewa , uelezaji na uongo.

Sasa hata huyu membe, hajui kujieleza, membe ni kama samaki ukimtoa majini anakufa. Yeye anajua sana mambo ya mahusiano ya kimataifa, ukimsikia anazungumzia mambo hayo utatamani angekuwa mjomba wako.

Sielewagi alifikaje top 3 ya ccm 2015,hahahaha nadhani 2015 kigezo vya mgombea wa ccm vilihusisha mgombea ni lazima awe na kiwango fulani cha ujinga hahaha sababu kama membe, Mheshimiwa Rais na yeye, na hajabadirika mpaka leo, ukimtoa kwenye mabarabara na madaraja na yeye ni kama samaki nchi kavu. Nisimzungumzie mama samia sababu dhana ya wanawake wakiwezeshwa wanaweza inaeleweka vizuri tu.

Wote tunaona mapungufu ya rais katika mambo ya sheria na utawala bora, mambo makubwa kabisa ya kikatiba, hahahaha korosho, bureau we changes, makinikia n.k

Wasiwasi wangu membe nae ni mtu wa hivi, sasa Mimi 2020 ntapiga kura kisayansi zaidi, najua Haito count lakini huwezi jua, ntapiga kisayansi, nimejifunza mambo mengi sana siku za hivi karibuni hasa mambo ya kisiasa, sio ya kuyaangalia kwa darubini moja tu, toka lowassa arudi ccm mpaka kufikia rostam azizi kuwa political analyst, ni darasa kubwa.

Hujui kuandika? Huna herufi kubwa kwenye majina ya watu! Rudi kwanza shule ujifunze kuandika. Hapa ni Membe tu
 
Back
Top Bottom