Lancashire
JF-Expert Member
- Sep 20, 2014
- 14,057
- 10,365
Habari za Jumapili mabibi na mabwana.
Kwanza kabla ya yote ningependa Ku declare interest kwamba Mimi bado ni muumini wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na changamoto nyingi ninazopitia kutokana na baadhi ya matendo yasiyo yakuridhishwa yanayofanywa na Chama Changu.
Kama heading inavyojieleza nauona mwaka 2020 kama kaburi la chama changu huku nikizingatia wanachama wengi tunaoipitisha CCM huku mashinani ndio sisi tunaoisoma namba kwa sasa kutokana na hali ngumu sana ya kimaisha tunayoipitia.
Ni kweli kabisa serikali inatekeleza miradi mbali mbali kama ujenzi wa Kiwanja cha kimataifa cha Chato, ununuzi wa Boeing na bombardier na sasa tunaanza ujenzi wa reli ya kisasa.bila kusahau kuhamia Dodoma.
Lakini nikitafakari kwa undani haya yote hayamsaidii mwananchi wa kawaida huku kijijini ambako kwa sasa kilo ya sukari ni 2800 mpaka 3000 kunywa chai ni anasa. Kilo ya unga wa sembe ni 2000 hadi 2200, bei za bidhaa sokoni zimepanda kuliko wakati wowote ule.
Biashara ndogo ndogo ambazo wengi hutegemea kwa kipato na kujiendesha kimaisha zimekwama hakuna wateja, TRA wanadai kodi tumeishia kufunga. Sasa natafakari kwa kina mwisho utakuwaje. Jibu ni rahisi sana Wengi tutatafuta mbadala wa kutusaidia na hakutakua na mwingine zaidi ya Chadema chama kikuu cha Upinzani.
Nisingependa iwe hivyo lakini hakutakuwa na namna. Hapo mengi sana sijayaongelea ila kwa kifupi haya ndio nilitaka kukitahadharisha chama change ili hatua za dharura zichukuliwe mapema kuokoa uchumi wa nchi hii ambao unaelekea shimoni.
Wasalaam.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.