CCK: Tunajenga chama mbadala

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=2]Wednesday, November 28, 2012[/h]Hivyo basi, baada ya kukiacha CCJ kife, viongozi kutoka mikoa 14 Tanzania Bara na Visiwani walikutana Dar es Salaam, Julai 20, 2010, kukubaliana juu ya uanzishwaji wa chama kipya ambacho walikipendekeza kwa jina la Chama Cha Kijamii (CCK), na ndipo ukafanyika uchaguzi wa viongozi wake wa muda. Watanzania wengi ndani na nje ya Tanzania walishirikishwa wazo hili na wakaliunga mkono.


cck.jpg

Baadhi ya wanachama wa CCK wakiwa wameshika bendera ya chama chao.


KATIKA gazeti hili, toleo namba 04525, Jumatano Novemba 14, 2012, Mwandishi Joseph Zablon, aliandika makala kwenye ukurasa wa tatu yenye kichwa cha habari, “ Wamenivua uongozi CCK kunidhoofisha - Muabhi”.


Baada ya kuisoma kwa makini makala hii nikaona kuna kila sababu ya kuijibu ili kuweka uwaza wa jambo hili ambalo kwa mujibu wa mwandishi, tafsiri inayopatikana ndani ya makala yenyewe ni kana kwamba kuna mgogoro ndani ya Chama Cha Kijamii (CCK).


Katika aya ya kwanza ya makala kunasomeka, “Ngoma ikivuma sana hupasuka. Wakati kinaanzishwa kilivuma sana, Chama Cha Kijamii (CCJ), kilipata usajili wa muda haraka, lakini ilipofika wakati wa uhakiki ili kipate usajili wa kudumu, kikakutwa hakina wanachama, na papo hapo kikafutwa” unasema utangulizi wa makala husika.


Aya ya pili inasema, wahusika hawakuridhika walijizoazoa tena na kuanza harakati mpya za kukianzisha upya kama Chama Cha Kijamii (CCK), na kupata usajili wa kudumu mwaka 2011. Ukweli ni kwamba chama kilichofutwa ni Chama Cha Jamii ambacho kifupi chake kilikuwa (CCJ) na siyo Chama Cha Kijamii (CCK).


Labda, niseme mojawapo ya sababu za kufutwa kwa CCJ ilitokana na waandishi wa habari wasiopenda kujituma na kufanya uchunguzi wa mambo kwa kina. Sababu kubwa ya kufutwa kwake ni kwamba CCJ ilikosa viongozi wa kukisimamia, achilia mbali sababu za kiuhakiki kama mwandishi anavyojaribu kueleza katika utangulizi wake.


Kilikosa uongozi kwa sababu baadhi ya waasisi wake walikihama na kuhamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa ajili ya kuwahi ratiba ya uchaguzi mkuu wa 2010, na hivyo kusababisha viongozi waliobaki kutafakari upya safari hiyo ndefu na ngumu ya kisiasa na hatimaye Julai 16, 2010 viongozi ngazi za juu walimwandikia Msajili wa Vyama kujiuzulu nafasi zao na hivyo kukiacha kife.



Kwa kifupi, CCJ ilikufa yenyewe Julai 16, 2010 kabla ya Msajili kukifuta rasmi Julai 23, 2010, siku alipokipatia usajili wa muda Chama Cha Kijamii (CCK).


Hivyo basi, baada ya kukiacha CCJ kife, viongozi kutoka mikoa 14 Tanzania Bara na Visiwani walikutana Dar es Salaam, Julai 20, 2010, kukubaliana juu ya uanzishwaji wa chama kipya ambacho walikipendekeza kwa jina la Chama Cha Kijamii (CCK), na ndipo ukafanyika uchaguzi wa viongozi wake wa muda. Watanzania wengi ndani na nje ya Tanzania walishirikishwa wazo hili na wakaliunga mkono.


Baada ya matukio ya mwaka 2010 ambapo tulitambua kuwa baadhi ya watu waliotaka kuanzisha chama pamoja nasi walikuwa na lengo la kutaka madaraka tu na siyo kutumikia wananchi, tuliamua kutoka wakati ule kutoshirikisha watu wanaoitwa “vigogo” isipokuwa wale tu ambao hawana mpango wa kutumia chama chetu kupata madaraka ya haraka.


Hivyo, CCK iliamua tangu mapema kabisa kuwahusisha wananchi moja kwa moja na kwa ushawishi wa hoja na kuwaonesha kuwa yawezekana chaguo bora liko nje ya vile ambavyo watu wamevipokea au kuaminishwa kuwa ndio chaguo pekee.


Hivyo, tulitiwa moyo jinsi tulivyopokewa mikoani na vijijini ambapo watu walikaa chini kutusikiliza na kutupa nafasi ya kuwashawishi.


Hatukutumia magazeti au vyombo vikubwa vya habari na badala yake tulikwenda vijijini na mijini ambapo tulikutana na wananchi ambao baada ya kutusikiliza wengi walikuwa wanatuambia maneno ya matumaini kuwa “hiki ndicho chama walichokuwa wanakisubiria”. Hivyo, CCK haijavuma magazetini kama zama zile za CCJ, hii maana yake ni kwamba kuna kitu kikubwa kinatengenezwa.


Katika aya zinazofuata mwandishi ameeleza kwamba ilipata usajili wake wa kudumu mwaka 2011, jambo ambalo si sahihi, bali usajili wa kudumu wa CCK ulikuwa Januari 27, 2012, na kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, sheria namba 5 ya mwaka 1992 na marekebisho yake mwaka 2009, CCK kinatakiwa kifanye mkutano mkuu ndani ya kipindi kisichozidi mwaka mmoja, tofauti na mwandishi anavyoeleza katika aya yake ya sita kwamba CCK itafanya uchaguzi mkuu Januari 30, 2013.


Madai ya aliyekuwa Katibu Mkuu wetu, Komredi Renatus Muabhi, kuondolewa kwake katika wadhifa huo ni mpango mahususi wa kumdhoofisha eti kwa kuwa yeye anawaka ndani ya chama, ni madai ya kitoto sana. Jambo hili lilisababisha uongozi mzima wa chama kuitwa mezani kwa Msajili, Julai 3, 2012, Msajili alitoa fursa hii ili asikie undani wa jambo hili, alitusikiliza na mwanasheria wake akapitia vifungu vya sheria na uhalali wa vikao na kubainika kwamba hakukuwa na kasoro yoyote katika kufikia maamuzi hayo.


Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom