CCK kujaribu kuzuia mchakato wa Katiba Mpya... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCK kujaribu kuzuia mchakato wa Katiba Mpya...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 19, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  VIONGOZI wa vyama viwili vya siasa nchini wameibuka na kutoa notisi ya siku 90 kwa Serikali kusitisha mchakato wa mabadiliko ya Katiba mpya unaoendelea kwa madai kwamba mchakato wa Sheria ya kuunda Katiba hiyo haukushirikisha wananchi.

  Aidha wamesema mchakato huo wa sheria haukufuata utaratibu na pia Tume ya kukusanya maoni iliyoundwa hivi karibuni ni batili.

  Wakizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam juzi, viongozi hao wa Chama cha Kijamii (CCK) na Chama cha Sauti ya Umma (SAU) walidai kutokana na upungufu wa sheria hiyo watakwenda mahakamani kusititisha mchakato huo.

  Viongozi hao ni Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Herman Shelutete, Naibu Katibu Mkuu wa SAU, Erick Mchatta na Kiongozi wa masuala ya sheria wa chama hicho Godbless Msofe.

  Muabhi alisema tayari wamewasilisha juzi notisi hiyo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa Waziri wa Katiba na Sheria na kabla hawajaenda mahakamani wataelezea mapungufu yote yaliyopo katika sheria.

  Akizungumza na gazeti hili, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alisema yuko safarini na hajaiona barua hiyo lakini akasema kama ipo ataifanyia kazi atakaporejea ofisini.

  Alisema lakini kwa mujibu wa sheria kinachotakiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoa kibali cha kwenda Mahakamani ndipo serikali itakapojibu.

  Kuhusu kuzuiwa kuendelea kwa mchakato wa Katiba alisema hilo haliwezekani labda litakapofika mahakamani na mahakama ikaamua kusitisha mchakato huo.

  HABARI LEO:
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mbona wamechelewa walikuwa wapi siku zote wenzao waliomba ahadi na JK kwenda Ikulu kujadali mustakabali wa taifa letu kuhusu Katiba.

  CCK kwani wao wametumwa kuwasemea Watanzania lini walifanya makongamano ya katiba na kukusanya maoni ya Watanzania.

  CCK mlitembelea maeneo yapi katika mikoa ya Tanzania kuchukuwa maoni.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wanatafuta single ya kutokea?
   
 4. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  vipi anii,wataka kuhama bara, na kale kabanda ka mzee mtakahamisha vipi?au mtapiga bei?ikifikia hapo unijulishe na mimi nitawaunganishia cha mjomba wangu pale unguja.
   
 6. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hiki kipengele kinafurahisha, kimekalia kama vile serekali imejipigilia vingiti isipate kushtakiwa.
   
 7. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  tehe tehe tehe aaaaaaaaaaa jamani cck nanyie mpo? njaa hizi jamani zitawapeleka pabaya sana
   
 8. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  wasicheleweshe ukombozi
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Neno "kujaribu" linaonesha hamjui mlifanyalo na mnatafuta pakutokea.
   
 10. H

  Hacha Member

  #10
  May 20, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani wana point, lkn bahati mbaya mahakama zetu siyo huru
   
 11. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Wanataka mwaliko Ikulu hao hawana lolote.
   
 12. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji hio heading yako ilitakiwa kusema 'CCM kujaribu kuzuia mchakato wa Katiba Mpya...':hat:
   
 13. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MMM bado upo CCK au?
   
Loading...