Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,447
- 39,857
Swahiba wa Makamba akimbilia CCJ
Na Lulu George
Aliyekuwa Kada na mpiga debe wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Yahya Gadaffi, ametangaza kukihama chama hicho kujiunga na Chama cha Jamii (CCJ) na kugombania ubunge Jimbo la Tanga.
Kada huyo ameahidi kutimkia CCJ akiambatana na wafuasi zaidi ya 1000 wa kutoka CCM na vyama vingine vya siasa vilivyopo mkoani Tanga.
Alisema hatua hiyo ni ya kumuunga mkono aliyekuwa Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe, kwa kile alichodai kuwa kuhamia kwake CCJ ni kuonyesha uzalendo wa hali ya juu na kujali maslahi ya Watanzania.
Alifafanua kuwa wanachama anaohama nao CCJ 600 ni kutoka CCM na 400 waliobaki ni kutoka vyama vingine vya siasa vilivyopo mkoani Tanga.
Alisema uamuzi wa kuihama CCM ni kutokana na kuchoshwa na ahadi hewa alizopewa na viongozi wa juu wa chama hicho wakati alipokuwa akijiunga nacho mwaka 2007 kwamba kingesaidia kuleta mabadiliko ya Mkoa wa Tanga, ahadi aliyosema kuwa haikutekelezwa mpaka sasa.
CHANZO: NIPASHE
Wakati huo huo, CCJ inaendelea taratibu kukamilisha taratibu za kupata usajili wa kudumu na kama mambo yataenda inavyotarajiwa hilo litafanyika ifikapo mwanzoni mwa mwezi Juni na hivyo kuweka CCJ katika ulingo wa kushiriki uchaguzi mkuu kikiwa na lengo la kusimamisha wagombea katika viti vyote vya Ubunge na Urais... MM