Elections 2010 CCJ yakwama kuwasilisha maombi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,116
CHAMA Cha Jamii (CCJ), jana kilishindwa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, maombi ya usajili wa kudumu na kitendo hicho sasa kitafanyika mapema wiki ijayo.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CCJ, Renatus Muabhi, taratibu zote kuhusu maombi hayo zimekamilika.

Alisema taratibu hizo ni pamoja na chama kufanikiwa kupata zaidi ya wanachama 10,000 idadi ambayo alisema imevuka ile iliyotakiwa na msajili, ya wanachama 200.

Muabhi alisema walikuwa wamepanga kuwasilisha maombi hayo jana, lakini yeye alikuwa safarini kwenda mkoani Dodoma na mwenyekiti wake alikuwa anakwenda Zanzibar.
Msajili Msaidizi wa vyama vya Saisa, Ibrahim Kiyabo, alisema hadi jana kufikia saa 5:00 asubuhi, alikuwa hajapokea maombi hayo kutoka katika chama hicho chenye usajili wa muda.

Ilidaiwa kuwa CCJ ilichukua fomu ya usajili wa kudumu, wiki iliyopita na kutangaza kuwa jana kingewasilisha rasmi maombi yake ya usajili wa kudumu, ambao hadi sasa umeingia wa mashaka.
Hali hiyo inatokana na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kutangaza mpango wa kuanza uchunguzi ili kuona kama kilianza shughuli za kisiasa miaka miwili iliyopita au la.

Tendwa aliipa CCJ usajili wa muda Machi 2 mwaka huu na kuitaka ihakikishe kuwa ndani ya miezi sita kiwe imepata wanachama 200 kutoka mikoa kumi ya bara na kisiwani.

Hata hivyo, CCJ imetumia muda wa takribani miezi miwili kukamilisha kazi hiyo, jambo ambalo linajenga shaka kuwa huenda ilianza kupata wanachama kabla ya kupata usajili wa muda, hatua ambayo Tendwa alisema ni kinyume na sheria na kwa kufanya hivyo kinaweza kufutwa kabisa.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/5-habari-za-siasa/1433-ccj-yakwama-kuwasilisha-maombi
 
Hawa wana wasiwasi tu; hivi unaweza vipi kuorganize watu kuanzisha chama bila ya kukutana na watu hao kabla ya kuomba usajili wa muda? CCJ inawasumbua kwa sababu wanatafuta sababu ya kukinyima usajiili wa kudumu. Kwa mfano, sisi hapa JF tukiamua hatimaye kuanzisha chama tutaambiwa kuwa tumeshapata wanachama kwa vile tumekuwa tukizungumzia mambo haya kwa miaka sasa?

Hawa watu waanze kutumia uwezo waliopewa na Mungu kufikiria.
 
Ubabaishaji huo, wanatoa ahadi na kushindwa kutimiza.

Hicho chama kimefulia kabla hata ya kupata usajili wa kudumu. Walitangaza vigogo wa CCM kwenye mkutano wao, SIFURI. Wakatangaza siku ya kuwakilisha majina ya wanachama, SIFURI. Wametangaza tena siku ya kuwakilisha majina, bado imekuwa SIFURI.
 
CCJ wanatumia mgongo wa vigogo wa CCM kujizolea umaarufu. mpendazoe tayari, tusuiri wale watakaoshindwa kura za maoni ndio watakimbilia huko. CCJ ni walalamishi na hupenda kukimbila media kutafuta huruma ya wananchi, fateni sheria.........
 
Kwa mujibu wa Blog ya michuzi tayari wameeshakabidhi majina kwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa mchana huu

Katibu+wa+CCJ,+Richard+Kiyabo+akionyesha+risiti.JPG


Mwenyekiti akionyesha risiti ya malipo ya kuwakilisha mchana huu
http://www.issamichuzi.blogspot.com/
 
naona wakandiaji wametoweka tena; jamani kama CCJ siyo kitu, geresha or whatever have you just give usajili wa kudumu halafu waache wafe kifo cha vile vyama vingine.
 
Back
Top Bottom