CCJ na Ajenda ya siku 100 za kwanza; yapeleka barua kwa mabalozi, yaandaa maandamano

kwahio mkuu msajili anavyo kwenda kwenye hii mikoa kuhakiki wana chama proof inayohitajika ni ya kauli tu kutoka kwa hao watu 200 na sio kuonesha kadi ya uanachama wa chama kinachofanyiwa huakiki? au nimekuelewa vibaya?

duh.. jamani someni pole pole ninachosema basi. Inakuwa kazi kurudia kitu kile kile kwa watu wale wale.
 
asante sana mkuu hata mimi najiuliza haraka ya nini ? na kama walikuwa na haraka sana kwanini walichelewa mda wote huo mpaka dakika hizi za mwisho?

maswali mengine basi myafikirie.. kwani inakatazwa wapi na nani kuanzisha chama cha siasa wakati wowote wa mwaka? Hakuna mahali popote inapokatazwa kuanzisha chama ati kwa sababu inakaribia uchaguzi! Msajili hatakiwi kuangalia mambo mengine yoyote yale isipokuwa merits za chama na kukipa usajili - sasa kama kitataka kushiriki uchaguzi au la hilo ni suala la chama chenyewe siyo suala la msajili.
 
mWANAKIJIJI, NADHANI LABDA CCJ WAMESHINDWA KUISOMA VIZURI SIASA YA TANZANIA, KWA TANZANIA WATU WANAPENDA WATU NA WALA SIO SERA AU ITIKADI, WATU WANAANGALIA SURA NZURI, MTOA MIPASHO MIZURI NA VITU KAMA HIVYO,

HEBU NOTE HIKI, CCJ HAKIWEZI NA HAKITAWEZA KUKUBALIKA KAMA HAO BIG FISH HAWATAJITOKEZA ADHARANI, NA HILO NDIO KOSA KUBWA LA CCJ (USIRI), WAKIWAWEKA WATU WAO ADFHARANI NA SUPPORT ITAKUWA KUBWA MNO, HIVI WANACHOKIOGOPA NI NINI KUJITOA ADHARANI?
INA MAANA MNATAKA KUNIAMBIA MZEE WA KIRARACHA NDIO ALIKUWA SHUJAA WA KWELI KWA KUTOKA CCM BILA KUOGOPA, INA MAANA SALIMU,WARIOBA, BUTIKU NA WENGINEO PAMOJA NA EXPOSURE, ELIMU NA UWEZO WALIOKUWA NAO WANASHINDWA KWELI KUWA FREE, HIVI KWELI WATATUFAAA HAO KUWA VIONGOZI WA KUINDESHA HII NCHI? AMBAYO KWA SASA INAHITAJI KIONGOZI JASIRI NA MWENYE KUJITOA ILI AZIRUDISHE FEDHA ZETU ZOTE ZILIZOPORWA NA MAFISADI NA PIA KUISUKUMA HII NCHI KWENYE MAISHA BORA NA UTU KWA KILA MTANZANIA?

HII NCHI INAHITAJI UKOMBOZI WA KWELI NA TUNAHITAJI WATU MAHILI NA WASIO NA WOGA WA KUOGOPA KUTENGWA NA CHAMA CHA MAPINDUZI, NINA WASIWASI SANA NA APPROACH YA CCJ, HAKIINGII VIZURI KWENYE SIASA ZA TANZANIA
 
maswali mengine basi myafikirie.. kwani inakatazwa wapi na nani kuanzisha chama cha siasa wakati wowote wa mwaka? Hakuna mahali popote inapokatazwa kuanzisha chama ati kwa sababu inakaribia uchaguzi! Msajili hatakiwi kuangalia mambo mengine yoyote yale isipokuwa merits za chama na kukipa usajili - sasa kama kitataka kushiriki uchaguzi au la hilo ni suala la chama chenyewe siyo suala la msajili.

haya maswali nilikua najiuliza mwenyewe kwa maoni yangu. naona mambo yanakuwa ya kulazimisha bila kujiandaa kikamilifu ndio maana msajili ana pata upenyo wa kuleta zengwe.
 
duh.. jamani someni pole pole ninachosema basi. Inakuwa kazi kurudia kitu kile kile kwa watu wale wale.
Hii inayodaiwa kuwa ndiyo ajenda ya CCJ sasa nakumbuka waliileta akina Mapalala, Mtikila, Mabere, Ndimara, etc (interestingly familiar names, huh?) mwaka 1991 pale Nkurumah UDSM - tulishangilia kwelikweli, the rest is history. Ninachotaka kusema ni kuwa inachokileta CCJ sasa hakina haiba mpya - tulishayaiona nearly 20 yrs ago!!
 
unaposema registered siyo sawa na card carrying member.. wanachama wanaweza kuwepo waliojiandikisha kama ambavyo CCJ imefanya na wapo wenye kubeba kadi lakini hakuna masharti ya kuwa ili utambulike kuwa mwanachama wa chama cha siasa nchini ni lazima uwe na "kadi". Sijui kama unaweza kunionesha kwenye sheria ni wapi panataka wanachama wa chama cha siasa wawe na kadi na kwamba mtu akisema mimi ni mwanachama wa chama fulani na nimejiandikisha basi huwezi kumtambua hadi akuoneshe kadi!?

Mzee Mwanakijiji,
Hapa unaruka ukweli, hawa wanachama wa CCJ to begins with hawakufika 200. Na vilevile achilia mbali kadi zao (za CCJ) wenyewe hawakuwa hata na vitambulisho vya kupiga kura, sasa sijui we ulitaka msajili atumie mbinu kuna kuwahakiki?
Mbona unakataa kujibu hoja ambazo mi pamoja na watu wengi tu humu wanaziona ziko wazi kuwa hawa viongozi wa CCJ ni wazembe, hata wao wenyewe viongozi hawakuwa na ID sasa kweli hawa ndio wanategemea kupewa dhamani ya nchi? Kubali hii ni bonge ya PR disaster kwa CCJ and they have only themselves to blame for!
Ni bora nguvu zetu za kura na hoja tuzielekeze kwenye vyama vya siasa vilivyopo ambavyo at least viko serious i.e. CUF na Chadema na kuachana na huu ujinga wa CCJ
 
Hii inayodaiwa kuwa ndiyo ajenda ya CCJ sasa nakumbuka waliileta akina Mapalala, Mtikila, Mabere, Ndimara, etc (interestingly familiar names, huh?) mwaka 1991 pale Nkurumah UDSM - tulishangilia kwelikweli, the rest is history. Ninachotaka kusema ni kuwa inachokileta CCJ sasa hakina haiba mpya - tulishayaiona nearly 20 yrs ago!!

umeisoma ajenda yenyewe au ndio yale yale ya kudhania kinachodaiwa? ajenda ya CCJ kama ilivyo sasa na kwa undani wake haijatolewa na chama kingine chochote kwa namna hii na haiwezi kutolewa na chama kingine.
 
I rest my case!
 
Ni bora nguvu zetu za kura na hoja tuzielekeze kwenye vyama vya siasa vilivyopo ambavyo at least viko serious i.e. CUF na Chadema na kuachana na huu ujinga wa CCJ

sasa jamani si mviunge mkono tu hivyo vingine hata kama havina ajenda kali ya mabadiliko na haviwezi kukumbatia ajenda ya mabadiliko kama ya CCJ?
 
I rest my case!

bila ya shaka umeelewa kwanini CHadema na CUF hawawezi kukumbatia ajenda kama hiyo na mengine ambayo CCJ haijaweka wazi. Vyote vimebakia ni moderate lukewarm parties.. na anayefikiria watapata viti zaidi ya 70 kwa ajenda ya "tuing'oe CCM tu" anaota!!
 
Hivi msajili anapohakiki wanachama hutumia tafsiri ipi kuwa huyu ni mwanachama? Minadhani hutumia tafsiri ya katiba ya chama husika. sasa je katiba ya CCJ inasemaje kuwa mtu anasifa zipi kuwa mwanachama wa CCJ ? je katiba haisemi kuwa pamoja na sifa zingine kadi pia ni mojawapo?. lakini jamani hata kutumia akili ya kawaida tu uanachama bila kadi utatambulikaje duniani kote wanavyama huwa na kadi. tusichanganye mambo kati ya uanachama na ushabiki. Hivi umakini wa viongozi wa CCJ upo wapi hasa, watu wanaotaka tuwaamini kuwa niwakombozi kwa sera zao moto moto, watu wanaotaka tuwaamini tuwape nchii watuongoze wanashindwa kuorganise kitu ndogo kama hii tena hapa Dar hata idadi haikutimia, hii ni aibu. unapoingia katika mapambano lazima umjue adui yako vyema na hii ndio sifa mojawpo ya watu makini, kama kweli wanazijua siasa za tz walipaswa kujiandaa kweli kweli na si kwenda kwenye uhakiki na watu wachache tena walioorodheshwa bila kadi na wenye kadi namba zipo shaghala bagala na kuishia kutamka kwa jazba maneno hayana hata mantiki,.je hawa ndio wanaotaka tuamini wapinzani wa kweli. Lazima tufikie mahali tutambue kuwa, kuwa upinzani si mara zote kuwa sahihi watu wanafanya upuuzi tu hata kwa vitu vidogo alafu tuwasapoti tu kisa wapo upinzani na ccm inawaonea,Huwezi kufanya mambo kiholela holela kisha ukasingizia mfumo mbovu. chama bado hata hakijapata usajili wa kudumu mnakimbilia mahakamani ati kisa kadi. hata huko ubalozini wata waona wapuuzi, Sina matatizo na CCJ kama chama ila jinsi wanavyofanya mambo yao ndio ninamatatizo, hapa swala ni kurudi wajipange upya watapata usajili tu, maana hapa tatizo ni kushiriki uchaguzi bahati mbaya wamekosea timing
 
unaposema registered siyo sawa na card carrying member.. wanachama wanaweza kuwepo waliojiandikisha kama ambavyo CCJ imefanya na wapo wenye kubeba kadi lakini hakuna masharti ya kuwa ili utambulike kuwa mwanachama wa chama cha siasa nchini ni lazima uwe na "kadi". Sijui kama unaweza kunionesha kwenye sheria ni wapi panataka wanachama wa chama cha siasa wawe na kadi na kwamba mtu akisema mimi ni mwanachama wa chama fulani na nimejiandikisha basi huwezi kumtambua hadi akuoneshe kadi!?

Mkuu,wewe ni mtu makini sana,na maandiko yako yanachukuliwa kwa uzito mkubwa (naamini unatambua kuhusu hilo).Sasa unapojaribu kutetea uzembe wa CCJ,inatuwia vigumu wengine kukuelewa.Kwani CCJ walipotangaza wamekamilisha matakwa ya usajili wa chama chao,na kuthibitisha idadi ya wanachama waliopatikana,walikuwa hawafahamu kuwa Msajili atadai uthibitisho wa uwepo wa wanachama hao?

Na unaposema hakuna sheria inayosema ili uwe mwanachama wa chama lazima uwe na kadi nashindwa kabisa kukuelewa.Labda tusaidie ni namna gani Msajili angeweza kuthibitisha kuwa waliojitokeza katika tathmini sio wahuni tu wa mtaani bali wana CCJ?Faida ya kadi za chama ni nini kama sio utambulisho?

Kumbuka hapa hatuzungumzii kutembea na kadi ya unachama kama urembo bali kuwa na kadi ya uanachama kwa madhumuni ya uthibitisho.

Hawa jamaa ni wazembe wa daraja la kwanza.Na wanazidi kudhihirisha ubabaishaji wao kwa kulalamika sasa ilhali walikuwa na msimamo tofauti wakati wanamwalika Tendwa kufanya uhakiki wa wananchama.

Mwisho,tusiwe kama CCM ambao hawakubali kukubali ukweli hata pale ukweli unapojidhihirisha waziwazi.
 
of course.. si walimpelekea majina ya orodha ya wanachama wote waliojiandikisha?

Hivi kweli mlalahoi unaamini kuwa mtu akiwa na kadi ya chama fulani basi ni mwanachama? Kipimo cha 'kadi' ni kipimo ambacho hakina msingi kwa namna yoyote ile.

Na unaposema hakuna sheria inayosema ili uwe mwanachama wa chama lazima uwe na kadi nashindwa kabisa kukuelewa.Labda tusaidie ni namna gani Msajili angeweza kuthibitisha kuwa waliojitokeza katika tathmini sio wahuni tu wa mtaani bali wana CCJ?Faida ya kadi za chama ni nini kama sio utambulisho?

Hoja ni zaidi ya hilo, Msajili hana sababu ya kuhakiki uanachama wa mtu yeyote yeye anatakiwa kutoa usajili kwa chama ambacho kimetimiza masharti ya Ibara ya 10 ya sheria ya vyama vya siasa. Kama chama kinasema huyu ni mwanachama wetu na huyo mtu anakubali kuwa ni mwanachama, msajili anatakiwa akubali kuwa ni mwanachama. Nje ya hapo ni kwenda juu ya madaraka yake.

Kumbuka hapa hatuzungumzii kutembea na kadi ya unachama kama urembo bali kuwa na kadi ya uanachama kwa madhumuni ya uthibitisho.

Huwezi kuthibitisha uanachama wa mtu kwa kuangalia kadi; hivi unaweza kusema mtu ni mkristu kwa kukuonesha cheti cha ubatizo? au kwamba fulani ni muislamu kwa sababu umemkuta kashika Msahafu na tasbihi?
Hawa jamaa ni wazembe wa daraja la kwanza.Na wanazidi kudhihirisha ubabaishaji wao kwa kulalamika sasa ilhali walikuwa na msimamo tofauti wakati wanamwalika Tendwa kufanya uhakiki wa wananchama.

Hili laweza kuwa kweli lakini ni uzembe mkubwa zaidi kuamini uanachama unapimwa kwa kuwa na kadi.

Mwisho,tusiwe kama CCM ambao hawakubali kukubali ukweli hata pale ukweli unapojidhihirisha waziwazi.

hili nakubaliana na wewe.
 
Hivi msajili anapohakiki wanachama hutumia tafsiri ipi kuwa huyu ni mwanachama? Minadhani hutumia tafsiri ya katiba ya chama husika.

Hapana; yeye anatakiwa kuangalia sheria inasema nini? Sheria inasema chama kiwe na wanachama wenye kutimiza masharti ya kupiga kura ambayo yameainishwa na Katiba ya JMT. Masharti hayo hayahusishi kuwa na kadi ya chama cha siasa. Hivi hili ni gumu sana kulielewa?

sasa je katiba ya CCJ inasemaje kuwa mtu anasifa zipi kuwa mwanachama wa CCJ ? je katiba haisemi kuwa pamoja na sifa zingine kadi pia ni mojawapo?.

Ndiyo inasema lakini msajili hafuati katiba za vyama anafuata katiba ya nchi!
lakini jamani hata kutumia akili ya kawaida tu uanachama bila kadi utatambulikaje duniani kote wanavyama huwa na kadi.

Si kweli!

tusichanganye mambo kati ya uanachama na ushabiki. Hivi umakini wa viongozi wa CCJ upo wapi hasa, watu wanaotaka tuwaamini kuwa niwakombozi kwa sera zao moto moto, watu wanaotaka tuwaamini tuwape nchii watuongoze wanashindwa kuorganise kitu ndogo kama hii tena hapa Dar hata idadi haikutimia, hii ni aibu.

Uanachama wa chama cha siasa hautakiwi kulazimisha watu kuwa na kadi, kinachohitajika ni kukubaliana na itikadi, sera na mipango ya hicho chama. Marekani ukienda kujiandikisha kupiga kura kuna majimbo yanauliza wewe ni chama gani mtu anaandika Republican au Demokrat lakini haulizwi "kadi yako iko wapi"! Hata Uingereza sijui kama wanachama wa Conservatives na Labour wanatakiwa kuwa na kadi ili wawe wanachama!

unapoingia katika mapambano lazima umjue adui yako vyema na hii ndio sifa mojawpo ya watu makini, kama kweli wanazijua siasa za tz walipaswa kujiandaa kweli kweli na si kwenda kwenye uhakiki na watu wachache tena walioorodheshwa bila kadi na wenye kadi namba zipo shaghala bagala na kuishia kutamka kwa jazba maneno hayana hata mantiki,.je hawa ndio wanaotaka tuamini wapinzani wa kweli. Lazima tufikie mahali tutambue kuwa, kuwa upinzani si mara zote kuwa sahihi watu wanafanya upuuzi tu hata kwa vitu vidogo alafu tuwasapoti tu kisa wapo upinzani na ccm inawaonea,Huwezi kufanya mambo kiholela holela kisha ukasingizia mfumo mbovu. chama bado hata hakijapata usajili wa kudumu mnakimbilia mahakamani ati kisa kadi. hata huko ubalozini wata waona wapuuzi, Sina matatizo na CCJ kama chama ila jinsi wanavyofanya mambo yao ndio ninamatatizo, hapa swala ni kurudi wajipange upya watapata usajili tu, maana hapa tatizo ni kushiriki uchaguzi bahati mbaya wamekosea timing

Inawezekana unafikiri umesema kitu cha mantiki sana. Ukirudia pole pole utaona ni jinsi gani hakina mantiki kama nilivyoonesha hapo juu.
 
CCJ ni failure...kama mnashindwa kupanga, maana yake mmepanga kushindwa...!!!

Maandamano si sawa na Matembezi ya Hisan...Waulize wale wanaojua kufanya Maandamano na nini huwa kinawakuta...!!!....nguvu hio HAMNA

Bro Mwanakijii i can see unatumika vibaya either kwa kujua au unatumika bila kujijua...!!!..Muda ambao unautumia kuilelezea CCJ, ungetumika kuangalia mapungufu ya vyama vya upinzani vya sasa na namna ya kubadili...basi alau tungekuwa tuna matumaini kiasi ya uchaguzi ujao.

By the way...ningewashauri wadau kuachana na discussion za CCJ, nawashauri wadiscuss vyama vya Upinzani vilivyopo weakness na strength...na kujua ni kifanyike kukabiliana na CCM...Kila inapokaribia karibu na Uchaguzi mambo kama CCJ kuwaondoa wananchi ktk Focus ya maana ndio yanayotakiwa na CCM...!!!
 
Nothing makes me mad than the sheer arrogance and foolishness of this CCJ nonsense.

Eti CCJ wanatoa ajenda ya siku 100 baada ya kukamata nchi. Is this real life or a theory exercise???

Chama kimeshindwa kuonyesha wanachama 200 kwa mikoa 10 tu hapa nchini, watashinda vipi uchaguzi??

Let me make an assumption that CCJ has 200* 100 members kwenye kila mkoa TZ, will that give u guys even 1 MP??? Wil that get CCJ the presidency??

Yaani less than 140 days kabla ya uchaguzi, badala ya watu kufikiria namna ya kuongeza wabunge wa upinzani bungeni, tunaburuzwa na hii ndoto eti CCJ itakuwa chama ambacho hakijawahi kuonekana na kitaleta mabadiliko!!! In 140 days right??

Yaani ukifanya analysis deep, unaweza kabisa kufikia conclusion kuwa CCJ ni pandikizi la CCM kupunguza upinzani nchini, maana it is absolute a Futile attempt kama CCJ ni upinzani wa kweli kufikiria kushinda 2010.
 
kukomalia mgeni asiye hata na tiketi ya kuja kwako ni sawa na kula ugali kwa picha ya samaki!!!!!!!! pateni usajili kwanza

GADEMU!!
 
Back
Top Bottom