CCJ na Ajenda ya siku 100 za kwanza; yapeleka barua kwa mabalozi, yaandaa maandamano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCJ na Ajenda ya siku 100 za kwanza; yapeleka barua kwa mabalozi, yaandaa maandamano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 9, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Chama cha Jamii kikiendelea kuonesha dhamiri yake ya kutokukubali kusukumwa pembeni kimetangaza jana baadhi tu ya ajenda zake ambazo ndio kiini cha kuwekewa mizengwe ya kupata usajili wa kudumu. Pamoja na ajenda hizo za siku 100 za kwanza na mwaka mmoja wa kwanza wa wabunge wake CCJ vile vile inandaa maandamano ya wanachama wake na pamoja na hayo imeandika barua kali kwenda kwa mabalozi kuelezea jinsi serikali ya CCM imekuwa ikiunyanyasa mchakato wa demokrasia tangu kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992.

  Ajenda hiyo kali ambayo imegawanywa katika mafungu mbalimbali ikiwemo ya kisheria (legislative) na ya kiutendaji (executive) ina lengo la kuanzisha mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala na utendaji nchini. Kuvuja kwa taarifa za ajenda hiyo tangu kuanza kwa CCJ ndiko kunakotajwa kulisababisha CCM na vyombo vyake kuapa kamwe CCJ isipate usajili wa kudumu kwani ajenda hiyo haiwezi kukubaliwa na CCM kwani ndiyo ajenda pekee itakayoweza kukingoa Chama cha Mapinduzi madarakani.

  Pamoja na hayo, CCJ inapanga kuhoji uwezo wa msajili kuuliza kadi za uanachama kwani hakuna mahali popote katika sheria ya vyama vya siasa ambapo panataka mwanachama wa chama cha siasa kuwa na kadi ili ajitambulishe kuwa ni mwanachama. Masharti ya kupewa usajili wa kudumu kwa mujibu wa sheria hiyo hayahitaji wanachama wawe na kadi ya vyama ili kutambulisha uanachama wao kwani wanatakiwa kutimiza tu masharti ya kuweza kupiga kura - na katika hayo hakuna lenye kutaka wapiga kura wawe na kadi.

  Hii ndiyo sababu mwanzoni tulisema kuwa uanachama wa CCJ ni wa itikadi na wa kadi! Kama ilivyo katika nchi nyingi za kidemokrasia kukubaliana na imani, malengo na mtazamo wa chama fulani cha kisiasa kunamfanya mtu kujitambua kuwa ni mwanachama wa chama hicho na ana haki ya kukitetea na kushiriki shughuli zake. Hii haimlazimishi kuwa na kadi.

  Matakwa ya kuwa na kadi ili kumridhisha msajili ni kinyume na katiba ambayo inatakataza kulazimisha watu kujiunga na vyama - kwa kutaka wawe na kadi msajili analazimisha watu wawe kwenye vyama! Alichotakiwa kufanya ni kukubali orodha aliyopewa na kukubali wananchi wenyewe wanapojitambulisha kuwa ni wanachama wa CCJ na kuwa majina yao yako kwenye orodha hiyo.

  Kwa mujibu wa vyanzo hivyo hoja hii ya mwisho ina lengo la kupindua kabisa nafasi na majukumu ya msajili wa vyama kwani amejipa uwezo asiokuwa nao na yaweza kuwa msingi wa kesi ya kikatiba huko mbeleni.

  AGENDA ZA SIKU 100 ZA KWANZA NA MWAKA MMOJA WA KWANZA:

  Kisheria:
  - Kuleta mswada wa mabadiliko ya sheria mbalimbali nchini ambazo zimekuwa kikwazo cha mabadiliko ya kweli. Baadhi tu ya sheria ambazo CCJ italeta Bungeni ili kuzifuta au kuzifanyia mabadiliko makubwa ni pamoja na

  • Sheria ya Magazeti ya 1976
  • Sheria ya Madaraka ya Rais wakati wa Dharura ya 1986
  • Sheria ya vyama vya siasa ili kuweka tume huru ya uchaguzi na hatimaye kuruhusu wagombea binafsi
  • Sheria ya Usalama wa Taifa ili kujenga idara mpya ya usalama wa taifa isiyofanya kazi kisiasa.

  - Kuanzisha mazungumzo ya utaratibu wa kuanza mchakato wa uandishi mpya wa Katiba yetu ili hatimaye kuondoa “kero” za Muungano, kuimarisha taifa letu, na hatimaye kutengeneza utaratibu bora, wa wazi na uwajibakaji na kusimamiana katika utawala wa taifa letu. Katika hili CCJ inakusudia kupunguza idadi ya wabunge ikiwemo kufuta ubunge wa kuteuliwa au wa kupewa na Rais na kuanzisha chemba ya juu ya Bunge ili Bunge letu liwe na sehemu mbili – bicameral. Kuandika Katiba yetu upya ni ajenda kuu zaidi kwa CCJ na itaanza utaratibu ndani ya mwaka mmoja na kuhakikisha inakamilika ili uchaguzi mkuu mpya unafanyika chini ya Katiba Mpya.
  -
  Kiutendaji:
  Serikali ya CCJ itachukua hatua kadhaa za kiutendaji ili kurudisha uwazi, uwajibikaji na uadilifu serikali bila kumuonea mtu, upendeleo, woga au jambo lolote lenye kuonesha uonevu. Baadhi TU ya hatua hizo ni pamoja na:

  - Kuanzisha Mahakama Maalum ya Wahujumu Uchumi kwa mujibu wa sheria ya Mitandao ya Uhalifu na Wahujumu Uchumi ya 1984. Katika hili CCJ haitamwogopa mtu yeyote awe ni kiongozi wa wakati huu au wa huko nyuma ambaye amehusika kwenye vitendo vya kulihujumu taifa hili. Wale wote ambao wameshiriki katika kudhulumu utajiri na jasho la Watanzania watasimamishwa kujibu mashtaka dhidi yao bila uonevu, katika uwazo na haki yote. Tuko tayari kushirikiana na taasisi za kimataifa kuwafikisha wahusika wote kizimbani.
  - Pamoja na hilo hapo juu CCJ itaanzisha uchunguzi wa viongozi na watendaji mbalimbali wa serikali ambao wanatuhumiwa au kuna sababu ya kuamini wanahusika katika kutumia madaraka yao vibaya kujitajirisha au kuficha mabilioni ya fedha ya nchi. Katika hili kila senti iliyochukuliwa pasipo uhalali kutoka kwa walipa kodi wa nchi yetu tuipendayo itarudishwa nchini bila kujali ni nani ameificha na wapi imefichwa. Tayari tuna uhusiano na watu mbalimbali ambao wanazo taarifa za viongozi na watendaji hao.
  - Kuvunja Bodi ya Mikopo ya Elimu (pamoja na kufanyia mabadiliko ya sheria yao) ili hatimaye tuunde chombo kilicho huru, cha haki na cha uwezo ambacho kitasimamia mikopo ya wanafunzi nchini ili kuhakikisha hakuna kijana wa Kitanzania ambaye hapati elimu kwa sababu tu hana fedha. Katika hili tutawafanyia uchunguzi watumishi wote wa bodi hiyo ili kuhakikisha hawajatumia nafasi zao kujinufaisha wao nje ya taratibu za kisheria. Katika hili hatuna mapatano.
  - Kufanya mabadiliko makubwa katika jeshi la Polisi kwa kubadili mfumo na muundo wake ili kulifanya liwe jeshi jepesi, la haraka, makini, la kisasa na lenye uwezo wa kushughulia uhalifu wa aina zote kwa utaalamu na weledi wa juu na kulibadilisha ndani ya miaka mitano kuwa Jeshi bora zaidi la Polisi katika Afrika nzima. Tunao wataalamu wenye kutushauri juu ya jambo hili.

  na mengine kadhaa ambayo hakuna chama kingine cha upinzani kinaweza kuyapigania bila kujiuma meno.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  soma magazeti ya leo.. kuweza kujua ajenda hiyo ya siku 100 ni ipi?
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ushauri wangu kwa CCJ,
  Ni vizuri ikaacha uchaguzi huu upite ili ijipange zaidi kwa uchaguzi wa mwaka 2015 kwa kurekebisha makosa ambayo imeyafanya mwaka huu.
  Swala la ku'arange maandamano sidhani kama litasaidia kwa chama hiki kusajiliwa on time.
  CCJ ijifanye wajinga kwa sasa as longer as wameshajua kuwa kuna hujuma dhidi yao wapange mambo yao kimya kimya na watimize tu yote wanayoyataka akina Tendwa ili wakose pa kuwabania.
   
 4. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Nchi hii baadhi ya watu wameshaifanya yakwao kwani"-
  • Jeshi la polisi
  • Msajiri wa vyama
  • Usalama wa Taifa
  • Tume ya uchaguzi,
  hawa wote wako kwa ajili ya kuhakikisha nchi inakuwa masikini kwa kuamua mambo yanayowapa kuendelea kuwa madarakani na kuhakikisha hawatolewi madarakani. Tena viongozi wengi wa CCM shule zao hazitishi, na hawana jinsi yoyote ya kuishi mpaka wanataka wabakie madarakani.
  Hili jambo la kutumia vyombo walivyoviweka kudhibiti demokrasia vitatuletea balaa ktk nchi. Wasi wasi wangu siamini kuwa demokrasia nchini ipo.
  Kama mgombea anasimama jukwaani na kusema sitaki kura zenu na ana uhakika wa kushinda hii ina maana gani wapendwa? Tunakoenda TZ hakujulikani.
   
 5. P

  Paul S.S Verified User

  #5
  Jun 9, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  huu ndio mw nzo wa mwisho wa hichi kinacho jiita ccj, mamabo ya kufanya kwa kukurupuka hayasaidii kutaka ku force usajili ili uwahi uchaguzi wakati wameshindwa hata kuwaandaa wanachama 200 tu hapa dar. yaani nashindwa kuelewa umakini wa hawa ccj wnataka kutambuliwa bila kadi hii habari ya pi jamani, sasa wanaanza kutafuta umaarufu kwa mahakama, maandamano, kwa mabalozi. najua utawala uliopo ni onevu lakini kwa hili ccj rudini mkajipange upya
   
 6. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  CCJ...CCJ...CCJ... Hawawezi kufanikiwa kwa kuptia media support, Watanzania ni wasahaulifu mno...kama media inasaidia yapo wapi mswala ya Richmind, Kagoda, Meremeta, na mengine mengi yaliopamba media, nawashauri watlie wajipange upya kwa 2015
   
 7. W

  WaMzizima Senior Member

  #7
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mzee Mwanakijiji,
  Pamoja na juhudi zako zote kujaribu kutushawishi kuwa hii CCJ ndio chama halisi mbadala hapa Tz ukweli on the ground is quite the opposite. Huko ulipo Michigan, it is easy to dream kama tulivyo wengi kuwa tunahitaji chama mbadala cha kweli ambacho kiko organised na kuwa na sera zenye kueleweka.
  Ukweli ni kuwa CCJ imeshindwa kuorganise hata watu 200 ambao waTz wengi tuna uwezo angalia tulivo bize kwenye kuandaa harusi n.k sasa mimi kwa kweli nilifadhaishwa sana na CCJ kushindwa kuleta hao wanachama ilhali walishadai kwenye vyombo vya habari kuwa wana wanachama zaidi ya 2,000 Dar pekee na waliotokea pale mwembe yanga ni 130 tu...you can not avoid factas on the ground kwa hili CCJ hawana wa kumlauma bali wenyewe...
  Kuhus hoja yako na utawala wa Msajili hayo ni malalamiko ya mtapatapa, sikatai kuwa kuna mapungufu katika hizi sheria lakini je si kweli kuwa wakati CCJ inasajiliwa ilisema haina tatizo na hayo matakwa ya msajili? kuhusu mada yako ya uanachama kuwa na kadi, mbona huo ndio mpango hata huko ughaibuni, yaani USA na UK pia wanachama wa Demecrats na vinginevo wana some sort of ID kuwatambua?
  Haya ni maneno ya mfa maji hiyo iko wazi...
   
 8. W

  WaMzizima Senior Member

  #8
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimejaribu kujibu hoja zako kwa msingi, majibu yangu yapo kwenye red sijajua namna ya kutumia multi quote wadau naomba msaada!
   
 9. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #9
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tulishaandika humu, watu lazima waache ushabiki wa ajabu, wakati mikiwa bize na chama cha kiini macho wenyewe wanajiimalisha kwelikweli sitashangaa kama wataibuka tena na ushindi wa katrina!
   
 10. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kadi gani unazungumzia hapa? ya chama au ya kupigia kura??

  Na mnapotoa kadi kwa wanachama wenu (wa CCJ) kuna manufaa gani kama mtu anaweza kuwa mwanachama bila kuchukua kadi??
  Na mtu huyo si lazima awe na kitambulisho...???

  Mnachojaribu kufanya ni kutumia udhaifu wa kisheria kwa manufaa yenu, ila msajili hawezi tu, kumkubali mtu yeyote ili mradi yumo kwenye orodha bila utambulisho wowote..! Nini maana ya kuhakiki sasa..? it doesnt make sense..!
   
 11. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Yaa utasikia Registered democrat or republican. In texas kuna more register republican than Democrat. How do they know?
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,564
  Likes Received: 18,299
  Trophy Points: 280
  .

  Mzee Mwanakijiji, with due respect, kumbe "uanachama wa CCJ ni wa itikadi na wa kadi!"!.
  What a double standards!. Utatofautishaje wanachama na washabiki?., taarifa hii kuwa baadhi ya wanachama wenu ni wale wa itikadi na sio wa kadi, inaanza kuniaminisha kuwa kumbe CCJ ni chama cha washabiki na wafuasi na sio chama cha wanachama!.
  Rejea katiba ya CCJ uliotumwagia humu JF.
  Kwa kusaidia tuu, hizi ndizo sifa za uanachama wa CCJ.


  UANACHAMA
  • 8. Sifa za Mwanachama:
   1. awe ni raia wa Tanzania;
   2. awe na umri usiopungua miaka kumi na nane;
   3. awe na akili timamu;
   4. awe anaikubali, anaiamini na kuitii Katiba ya CCJ na Kanuni zilizotungwa chini yake;
   5. awe na kadi iliyolipiwa ada stahili za Chama;
   6. asiwe mwanachama wa chama kingine cha siasa;
  Hiyo ya uanachama wa itikadi, umeitoa wapi wewe?!.

  CCJ ilipoanza tuu, nilicoment mahali kuwa kuna uwezekano CCJ ni 'Ghost Party'. Mpendazoe alipojiondoa CCJ na kujiunga CCJ, nilicoment mahali kuwa amefanya grave mistake, nikajisemea ningekuwa mimi ndio Mpendazoe, baada ya kukata shauri moyoni mwangu kuwa wakati wa kuachana na CCM, umefika, ningeitisha Press Conference na kuivua nguo CCM ili kuonyesha uchafu wake kwenye kadamnasi ya watu ili CCM wanifukuze, ndipo ningeonekana shujaa, na ningeondoka na wafuasi wengi waliochoshwa na uchafu wa CCM. Kitendo cha kujiengua kwa ahadi ya tutakufuata, amebugi step na this is the begining of his downfall, labda kama Chadema watamuokoa vinginevyo asubiri 2015, by then will be reduced to nothing!.

  Nilirudsha imani kidogo na CCJ, siku wewe Mzee Mwanakijiji ilipojibainisha na kujitanabaisha wazi kuwa sasa uko CCJ. Imani hiyo sio kwamba mimi ni mfuasi wa Mwanakijiji, bali ni background ya maandiko yako na kauli zako ambazo japo najua huna kadi ya CCM, ila kwa muda mrefu umekuwa mfuasi wa CCM au Mkereketwa wa mkubwa wa CCM, ndio maana ulipoandika tuu kuhusu CCJ, nikajiaminisha kuwa japo bado ni siri kujua who is who in CCJ, uwepo wako CCJ ni uthibitisho kuwa CCJ has substance in it, japo pia nilitoa angalizo usijekuta uko CCJ kikazi zaidi, yaani uko "kazini".

  Hii ya leo ya uanachama wa kiitikadi tuu, imenirudisha kule kule, kumbe CCJ is a hoax!.

  Forget kuhusu sheria taratibu na kanuni za usajili zinasema, kama vyama vyote vilivyosajiliwa vimefuata utaratibu fulani kupata usajili na nyinyi CCJ mkaufuata ili msajiliwe, lakini baada ya kuthibitika kumbe mna wanachama hewa, kama nilivyohisi ghost party, sasa ndio unatuletea hii double standard phenomena ya wanachama hewa, wenye imani tuu, wasiosajiliwa, wasio na kadi ndio mnampelekera msajili ili msajiliwe?.
  Kama CCJ ndio hii, huyo msajili hata ningekuwa mimi, siwapi usajili na mahakamani mtapoteza tuu muda wenu bure!.

  Hayo matakwa ya kisheria, ndio mmeyaona leo?!. Katiba inatoa haki kwa kila Mtanzania kushiriki harakati za kisiasa bila mizengwe yoyote, huku katiba hiyo hiyo ikiweka shurti la kupitia chama cha siasa. Mtikila kalipeleka hili Mahakama Kuu, ikalikubali ikatoa agizo kifungu husika kifutwe.

  Kama CCJ inajipanga kwenda mahakamani kuomba usajili kwa kupitia ghost members wenye imani tuu, don't waste your time na resources, you'll be fighting a loosing battle!.

  Naurudia tena na tena ushauri wangu huu kwako na washabiki wa CCJ,
  Good fighters ni wale wapambanaji mpaka kwa motto ya 'no retreat, no surrender' mpaka risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu linamwagika. Ila kwa ma strategic fighters, they don't try war!, they either fight or at all. They don't go to war when they know they will loose with their motto never fight a loosing battle!. In this cenario, CCJ is in a loosing side where there are left with only one option, surrender or die trying!.

  In everything there are always two ways. The right track and the wrong track, both tracks will reach you to the final destination, but if you take a wrong one, it will take you too long and you risk getting lost along the way such that you might not reach at all.
  Its not too late kuamua the right way! just act, the choice is yours! act now!
   
 13. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mzee tumeelewa, lakini hizo ajenda za siku mia moja zingekuwa za mwanzo katika kuhakikisha wale wanachama 200 wanapatikana na orodha yao anaipata Tendwa, Leo mmetukatisha tamaa hasa kwa kuonekana mambo ya kisanii na kurukia hoja kama hizo.
  Hayo yote si mliyajua, mngekataa uhakiki kwa sababu ulituambia CCJ kinaendesha mambo yake kisayansi. Mzee au hii ndumba na ngai?

  Mwaka huu sipigi tena kura
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  unaposema registered siyo sawa na card carrying member.. wanachama wanaweza kuwepo waliojiandikisha kama ambavyo CCJ imefanya na wapo wenye kubeba kadi lakini hakuna masharti ya kuwa ili utambulike kuwa mwanachama wa chama cha siasa nchini ni lazima uwe na "kadi". Sijui kama unaweza kunionesha kwenye sheria ni wapi panataka wanachama wa chama cha siasa wawe na kadi na kwamba mtu akisema mimi ni mwanachama wa chama fulani na nimejiandikisha basi huwezi kumtambua hadi akuoneshe kadi!?
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  sijasema kuwa uanachama wa kadi haupo au haufai; na kumbuka tunazungumzia katiba ya CCJ ya muda. Ninachozungumzia ni kuwa msajili wa vyama vya siasa halazimishwi na sheria kuuliza kadi za watu ili kujua uanachama wao.

  Sheria ya vyama vya siasa ya 1992 inaeleza kuwa chama kitapewa usajili wa kudumu endapo kitakuwa na wanachama 2000 kutoka mikoa 10 ambayo miwili kati yake ni kutoka Zanzibar. Wanachama hao ni wale ambao "who are qualified to be registered as voters for purpose of parliamentary elections". Sasa ukiangalia masharti ya kuwa mpiga katika Tanzania hakuna linalosema kuwa "ni lazima uwe mwanachama wa chama cha siasa".

  Hivyo, natofautisha matakwa ya chama chenyewe kinavyotambua wanachama wake na majukumu ya msajili kukipa usajili wa kudumu. Msajili hana uwezo wa kisheria wa kukataa kutambua wanachama wanaojitambulisha kwake kuwa ni wa wanachama wa chama fulani cha siasa ati kwa sababu hawana kadi! Unless mtu aniambie huu uwezo msajili kautoa wapi?

  Wengine wanauliza kwanini hoja hii haikutokea mapema si kila kitu kinafikirika mara moja. Mambo mengine tutaweza kuyafikiria na kuyatambua kwa kadiri tunavyokwenda mbele hatuwezi kuwa wafungwa wa historia yetu au kukwama kwetu huko nyuma.
   
 16. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  kwa kumbukumbu nilizonazo, hivi msajili alihakiki kadi wanachama wa ccm? mbona tuliona tu wanapewa cheti na wakajiita CCM No.1? hapo kuna hoja ya msingi..................
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  of course hawakuhakiki, wali presume kuwa kwa vile CCM iko madarakani itakuwa inao wanachama zaidi ya 2000 - wakaandika hivyo kwenye sheria na kukipa CCM usajili wa kudumu bila kuomba wala kuanza upya.
   
 18. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  asante sana mkuu hata mimi najiuliza haraka ya nini ? na kama walikuwa na haraka sana kwanini walichelewa mda wote huo mpaka dakika hizi za mwisho?
   
 19. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  kwahio mkuu msajili anavyo kwenda kwenye hii mikoa kuhakiki wana chama proof inayohitajika ni ya kauli tu kutoka kwa hao watu 200 na sio kuonesha kadi ya uanachama wa chama kinachofanyiwa huakiki? au nimekuelewa vibaya?
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  hakuna kitu kibaya kwani sheria kama ni dhaifu ni mbaya! Na si kosa kwa mtu kutumia sheria kwa manufaa yake! ulitaka aitumie kwa manufaa ya nani? SIJASEMA akubali mtu bila utambulisho wowote!!! Natumia maneno yangu vizuri sana, nasema ninachotaka kumaanisha na ninmaamisha ninachosema. Ili unielewe vizuri NImesema ni makosa kwa msajili kukataa wanachama ati kwa kutokuwa na kitambulisho kimoja tu cha kadi ya chama cha siasa hata kama mtu huyo anavitambulisho vingine!! Kwani huo uwezo wa kuhakiki upo kwenye sheria ipi? Serikali ikisema na kufanya vitu tunakubali tu lazima tuanze kujiuliza maswali.
   
Loading...