CCHADEMA yang'ara Uchaguzi mdogo wa Udiwani Sengerema, CCM na magari yao wanazomewa kila kona!

Pwaaaa

JF-Expert Member
Feb 16, 2013
248
0
Viongozi na makada wa CCM hapa Sengerema mkoani Mwanza wamekata tamaa ya kushinda udiwani kata ya Nyampulukano na Lugata!. Kwa hapa mjini Sengerema kila mwana CCM anayeonekana kavaa kijani ama njano anapigiwa miluzi mwanzo hadi mwisho. Na ili kuonesha kwamba watu wamechoshwa na CCM, hata gari la matangazo kila linakoelekea miluzi ya kufa mtu!. Alama za 'V' na Peeeeeeeeeeopleeeeeeeeeeeeeessssssssss za kumwaga.

CHADEMA kata ya Nyampulukano wanawakilishwa na mgombea wao, Zakaria Emmanuel Mnwaniz. Kule kata ya Lugata CHADEMA kasimama mtu mzima na msomi, Injinia Dk. Adirian TIZEBA.
CCM wao wanawakilishwa na Charles Gabriel Lugabandana ambaye anatuhumiwa kwa ufisadi wa mamilioni ya fedha ndani ya halmashauri ya Sengerema. Alifukuzwa kazi kwenye halmashauri hiyo kwa tuhuma za ufisadi.
TLP na NCCR-Mageuzi nao wamesimamisha wagombea ambao kimsingi siwajui kabisaaaaaa.
 
nemasisi

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
1,936
1,250
Mwaka huu kitaeleweka tu, ni wakati wa watu kuendesha nchi yao badala ya kundi fulani kutawala watu, wananchi wanataka nchi yao
 
Mna Nassa

Member
Jun 10, 2013
19
0
Nipo viwanja vya shule ya msingi sengerema,chadema ni noma kiwanja kimejaa,ccm wako mnadani wa mgeni wao ni wasira,pamoja na matangazo mengi yupo mgeni,njeleja na watoto wa shule
 
Alfred Daud Pigangoma

Verified Member
Mar 30, 2009
1,792
1,250
Nimepita Sengerema nikitokea Karagwe, yaani muda wakati CCM walipokuwa wanaelekea uwanjani huku wakiwa wamewakodi vijana wa boda boda wakiwa wamejaziwa mafuta kwenye pkpk, buku 10 pamoja na bendera kwa kila mmoja. Juu ya malipo hayo niliambiwa na mwendesha boda boda baiskeli ambaye alionekana kutoridhishwa na malipo ya buku 2. Kwa kweli ukifanikiwa kuona hata mkutano mmoja tu wa CCM ndo utajua kuwa waTANGANYIKA wakichoka chama na viongozi wake.
 
Brahnman

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
1,716
2,000

CCM wana kazi na mpaka kufika hiyo 2015 watakuwa wamenyoosha mikono!
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,981
1,500
Mkuu tunaomba matokeo
Viongozi na makada wa CCM hapa Sengerema mkoani Mwanza wamekata tamaa ya kushinda udiwani kata ya Nyampulukano na Lugata!. Kwa hapa mjini Sengerema kila mwana CCM anayeonekana kavaa kijani ama njano anapigiwa miluzi mwanzo hadi mwisho. Na ili kuonesha kwamba watu wamechoshwa na CCM, hata gari la matangazo kila linakoelekea miluzi ya kufa mtu!. Alama za 'V' na Peeeeeeeeeeopleeeeeeeeeeeeeessssssssss za kumwaga.

CHADEMA kata ya Nyampulukano wanawakilishwa na mgombea wao, Zakaria Emmanuel Mnwaniz. Kule kata ya Lugata CHADEMA kasimama mtu mzima na msomi, Injinia Dk. Adirian TIZEBA.
CCM wao wanawakilishwa na Charles Gabriel Lugabandana ambaye anatuhumiwa kwa ufisadi wa mamilioni ya fedha ndani ya halmashauri ya Sengerema. Alifukuzwa kazi kwenye halmashauri hiyo kwa tuhuma za ufisadi.
TLP na NCCR-Mageuzi nao wamesimamisha wagombea ambao kimsingi siwajui kabisaaaaaa.
 
Omuregi Wasu

JF-Expert Member
May 21, 2009
749
195
Mkuu nadhani umekosea jina la mgombea udiwani kwa tiketi ya Chadema kata ya Lugata. Eng. Dr. Adrian Tizeba ni Naibu waziri wa Uchukuzi na mbunge wa Buchosa hivyo awezi kugombea udiwani kwa tiketi ya Chadema.

Ninajua anaye kaka yake ambaye alikuwa diwani wa CCM ila akahamia Chadema. Labda ndo anagombea kwa ticket ya chadema

Top Bottom