CCCC mdai wa TPA kwa Gati 13 na 14 yapigwa marufuku miaka 10 kwa rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCCC mdai wa TPA kwa Gati 13 na 14 yapigwa marufuku miaka 10 kwa rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jizalendo, Jul 13, 2012.

 1. J

  Jizalendo Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana Jf mmeona kwenye Daily News ya tarehe 13 Julai 2012 kuwa PPRA imeipiga marufuku kampuni ya Chinese Communication Construction Company (CCCC) kupewa mradi wowote hapa nchini kwa kipindi cha miaka kumi kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa duniani kote. Kampuni hii ndio ambayo Mamlaka ya Bandari na Kamati ya Miundombinu ya Bunge ilitaka ipewe mradi wa Gati 13 na 14. Mnalionaje hilo?
   
 2. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Tayari Mfutakamba naye alikuwa ameshavuta ndo maana safari zake za China alikuwa anatoroka bila ruhusa ya bosi wake waziri Nundu
   
 3. J

  Jizalendo Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado ninaikumbuka hotuba ya Mh. Nundu bungeni na press conference yake. Huyo Mfutakamba walisema alipelekwa na hao CCCC pia Gambia na Guinea akiwa peke yake kinyume na taratibu. Walienda kufanya naye nini huko? Swali ni je alikuwa peke yake kwenye mipango hiyo ya ulaji? Swali zito zaidi ni kwanini Nundu alitafutiwa kila uzushi ili aondoke alipojaribu kuzuwia njema ya kumpa kazi hiyo CCCC kinyume na taratibu? Sasa tuone wote hao waliokuwa wanapika njama watafanywa nini: Mfutakamba, Mgawe, Chambo, Serukamba, Kilango-Malecela etc? Wenye uchungu na nchi hawatakiwi hapa!
   
 4. m

  mharakati JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Hii inaonyesha kabisa kua Nundu alionewa....yeye hakutaka hawa wahuni, naibu wake, wakuu wa TPA walikua na mpango wa kuvuta za kustaafu huku kamati ya bunge ikiwa na mpango wa kuvuta za kuongeza nguvu ya kisiasa tukielekea 2015.
   
 5. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,476
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Kama kuna watu walidhani kuondoka kwa Mh. Nundu kutaisaidia CCCC kupata kazi ishakula kwao.
   
 6. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hawa mafisadi hawawezi kufanywa chochote kwani nyuma yao katika hili dili yupo mkweree mwenyewe!!!
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Mwenyekiti wa kamati ya bunge miundo mbinu anakuwa upande gani kwenye hili? Na bodi ya TPA wanaachwa wapi kwenye hii rushwa?
   
 8. FuturePresident

  FuturePresident JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  CCCC....ndio ilisbabisha uonevu na majungu..yaliyopigwa na ile kamati ya kule mjengoni...kumbe nao pia walishavuta chao...diuuu aibu tupu...
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Watu wali comment kuwa Nundu alionewa kabisa na alikuwa anapambana na mafisadi wengi na wazito bila kujua,ni aibu sana ile kamati inatakiwa ijiudhuru haraka na Mgawe,Chambo hawatakiwi pale walipo imetosha!! Ni aibu kubwa sana
   
 10. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,476
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Mwenyekiti wa kamati ya bunge alishauri cccc wapewe kazi akijua wazi kua kazi yenyewe haijatangazwa popote wakati huo akimshutumu vikali waziri(Nundu) kwa kuizuia cccc kupewa kazi hiyo. Sijui alikua na maana gani.
   
 11. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu, sometimes siyo kila tuhuma ni za kweli, Nundu alionewa sana!
   
 12. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Rushwa hawa Wachina walimpa nani haswa kwa jina lake?kampuni/mamlaka ya Bandari hazitembei wala kuzungumza.Kuna watu wenye dhamana na hapa kuna wakurugenzi wa Kichina ,Makuwadi wa Kitanzania na Kichina na Walaji wa Kitanzania.
  Kule China hawa watoaji huchapwa risasi hadharani mchana kweupuee!
  Huku NYUMBANI HAWA MAKUWADI NA WALAJI HUKARIBISHWA KWENYE HAFLA za KUJENGA MAKANISA,MISIKITI NA HARUSI ZILE KUBWA KUBWA ZA WAKUBWA na hata wakiwajibishwa kisiasa hujiandalia mapokezi ya red carpet majimboni kwao!
  Hii ni TZ bwana!
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Lakini Nundu pia alikuwa anamsagia kipenzi cha Kikwete aliyekuwa kwenye huo wadhifa kabla yake Shukuru Kawambwa

  Ndiye aliyeweka Mikataba na hao CCCC; Nundu akataka kuvuruga yote kuanza Upya na Dr. Kawambwa naona alisha

  chota his 10%; sasa Nundu akianza upya ina maana watalazimishwa warudishe hizo sadaka...

  Ugomvi ulikuwa mkali... JK akacheza NUNDU akapewa boot...
   
 14. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Kumbuka kuwa JK aliahidi kuwa hatua zitachukuliwa kwa wote aliowaita kuwa "husababisha majungu hayo"
   
 15. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,318
  Likes Received: 610
  Trophy Points: 280
  Waziri kivuli wa miundombinu afuatilie hili kwa umakini ili siku ya kusoma maoni yake wananchi wengi wapate ukweli.
   
 16. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,105
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  Hii ni kichekesho hiyo kampuni ilishafungiwa Philipine kwa rushwa inakuwaje leo hii PPRA ndio waifungie tokea mwaka 2009 wamefanya hivyo kujikosha pia wamefungia Oxford Press University wakati tayari imeshapewa tenda ya kuchapisha vitabu na serikali kutokana na pesa ya rada wakati tayari benki ya dunia imeshaifungia na wao PPRA wanasema kama ilikuwa imepewa kazi iendelee hapa kuna mchezo unachezwa kama ilifungiwa kwa rushwa ina maana hata hiyo kazi iliipata kwa rushwa.
  Wakati waziri Nundu akitolewa baadhi tulijaribu kumtetea lakini tulionekana kituko kamati ya bunge ya miundo mbinu inayoongozwa na Serukamba inapasa kuchunguzwa kwani kuna uwezekano mkubwa ilipewa rushwa kutokana na sifa ya hiyo kampuni lakini vyombo vyetu kama BOT,Takukuru wanafanya nini mtashangaa kwanini naitaja BOT lakini wao wana uwezo wa kupata taarifa za makampuni yote toka nje
  Mwisho inabidi Nundu aombwe radhi kwani inaonyesha alikuwa anatetea maslahi ya taifa
   
Loading...