CBE kuandamana kupinga sheria ya mavazi

Sidhani kama kuna ukweli ktk hili la maandamano!
Bse lazima wapewe kibali na uko polisi watasema wanaandamana kwa ajili ya nini?Kutembea uchi?
Na kama wakiandamana ama sure wengi watakuwa mabinti ni kuwatafuta ring leaders na timua chuo wote pumbavu sana.
Wamekuja kusoma au kuinadi miili yao?

Kuandamana hakuihitaji kibali cha polisi. Unawataarifu unless wana sababu za kiinteligensia juu ya maandamano.
 
Sioni tatizo katika mavazi bana, kwani chuo ni cha Kanisa au madrasa hiyo? Utamlazimishaje mtu avae asivyotaka yeye sababu ya udhaifu wa watu flani? Hebu acheni udictator bana... Aaaaaaaarrrrrggg..!:car:
 
..Tatizo lipo katika vipaumbele vya hawa wanafunzi wa CBE. Mbona mimi sijawahi kuwasikia wakiandamana kwa jambo lolote kabla? Ndo kusema kati ya mambo yote ambayo nchi yetu imepitia hivi karibuni, hili la mavazi ndo limewagusa sana? Hii ni aibu yetu wasomi!
 
..tatizo lipo katika vipaumbele vya hawa wanafunzi wa cbe. Mbona mimi sijawahi kuwasikia wakiandamana kwa jambo lolote kabla? Ndo kusema kati ya mambo yote ambayo nchi yetu imepitia hivi karibuni, hili la mavazi ndo limewagusa sana? Hii ni aibu yetu wasomi!
wanaoandamana kwa mambo ya maana si hawa mkuu wao wako kwenye show za mavazi wanasubili wenzao wapigane badala yao, wapuuzi kweli sijui kukaa mjini saana ndo kunawazuzua!?
 
Wanafunzi wa College of Business Education wanatarajia kuandamana leo kupinga sheria mpya chuoni hapo inayopiga marufuku uvaaji wa suruali zinazobana, sketi, blouses na mavazi mengine yanayoacha wazi tumbo, kifua na kiuno. Pichani hapo chini ni sehemu ya tangazo lenyewe hapo chuoni likionyesha mifano ya mavazi yaliyopigwa marufuku.

552286_400391069988409_100000525597189_1458472_477520496_n.jpg

Kuna uhusiano (correlation) wa karibu sana kati ya kupenda kuonyesha vitu ambavyo wengi wetu hupenda kuficha, na uwezo wa akili wa jumla (uwezo wa akili wa jumla huhusisha intellect na wisdom). Ukiona mtu anapenda, kwa mfano, kulegeza suruali yake ili **** lake angalau moja lionekane hadharani, au anaachia 'chest' yake wazi ili angalau kipande fulani cha titi kionekane hadharani, basi mtu huyo, hata kama ana intellect kubwa (anaweza kufikiri sana), hawezi kuwa na wisdom (rational judgment). Kwa hiyo basi, mtu wa aina hii ni mtu ambaye ana upungufu wa uwezo wa akili wa jumla. Kwa hiyo tena, mtu wa aina hiyo ni kilema ingawa hawezi kujitambua kuwa ni kilema kwa sababu ya ukosefu wa wisdom.

Chuo kikuu au taasisi yoyote ya elimu haitoshi kumsaidia mtu wa aina hii...ni lazima kuwa na vituo maalum kwa ajili ya kuwarekebisha (centers for mental rehabilitation) ili wawe wasomi waliokamilika (wawe na balance ya intellect na wisdom) ili wafae zaidi kwa jamii. Tatizo hili ambalo mimi hupenda kuita MD (Mental Defect) lipo kila nchi duniani. Uarabuni na sehemu zenye waislamu wengi pia tatizo hili lipo lakini linafichwa kwa sababu ya uoga wa sheria kali na maadili makali ya kiislam...lakini ukifanya diagnosis kwa uangalifu, utaona hata baadhi ya mashekh wanalo. Ulaya ndiyo kwenyewe maana wagonjwa wa MD wanaruhusiwa kuonyesha hadharani ugonjwa wao na sheria zinawalinda. Hakuna sheria inayozuia--kuna freedom iliyozidi mipaka.

Kwa hiyo suluhisho si kuwakataza au kuwazomea wagonjwa hawa tu, nenda kwenye mzizi wa tatizo (yaani balance kati ya intellect na wisdom), changanua mzizi huo kwa uangalifu (wachache wanaweza kuiga tu), uwapate wale wenye shida ya MD, anzisha Mental Rehabilitation Centers (MRCs), peleka hawa ndugu huko ili wapate balance hiyo baada ya kupigwa msasa kitaalam. Hata chagudoa wengi wana MD ila wanahitaji program tofauti ktk MRC kuliko wale walioko vyuoni....hii itawachefua wengi, lakini ni lazima tuuseme ukweli kama ulivyo.
 
Weng hawajijui nafasi zao na matarajio yao

tatizo ndo hilo. Watu wakiwa vyuoni hawafikiriagi kwamba kuna siku watakuja kuutafuta uongozi wa jamii ila wanachofikiria ni wakati uliopo wa kufanya ukahaba na uhuni mwingine. Kwani mtu usipotuonesha matak.o,mapaja, tumbo unapungukiwa nini? Kama unataka kufanya ukahaba si usubiri jioni uende jolies ukauze mbweche yako? Wasomi wa kitanzania tu watu wa ajabu sana. Wenzetu wanafikiria wajukuu zao watakuja kuishi vp sie tunafikiria kuvutia wengine. Inabidi kwenye katiba mpya kiwekwe kipengela cha wale wote wenye historia chafu wasipewe uongozi maishani mwao. Hawa hawa ndo tutasiki wanagombe uvccm,bavicha nk. Mwisho wanaishia kufanya ngono kwenye mikutano ya kampeni.
 
..tatizo lipo katika vipaumbele vya hawa wanafunzi wa cbe. Mbona mimi sijawahi kuwasikia wakiandamana kwa jambo lolote kabla? Ndo kusema kati ya mambo yote ambayo nchi yetu imepitia hivi karibuni, hili la mavazi ndo limewagusa sana? Hii ni aibu yetu wasomi!
wanaoandamana kwa mambo ya maana si hawa mkuu wao wako kwenye show za mavazi wanasubili wenzao wapigane badala yao, wapuuzi kweli sijui kukaa mjini saana ndo kunawazuzua!?
 
CBE wamefanya vema kulitolea macho suala hili maana ni wazi kwamba watu wengi wanakwazika na hali hiyo, tukumbuke kuwa wanachuo ndo viongozi wetu wa kesho sasa kama wataachiwa tu wafanye mambo yasiyo na msingi, wapo wasomi ambao hawapendi kuona mazingira kama hayo, cbe wakifanikiwa ktk hili basi vyuo vingine pia vitafuatia
 
Nyakati za ajabu kabisa hizi....wanaandamana kudai haki ya kukaa nusu uchi kwa kweli utamaduni wetu umekumbwa na kansa ya damu has kwetu sie vijana
 
Sioni tatizo katika mavazi bana, kwani chuo ni cha Kanisa au madrasa hiyo? Utamlazimishaje mtu avae asivyotaka yeye sababu ya udhaifu wa watu flani? Hebu acheni udictator bana... Aaaaaaaarrrrrggg..!:car:

Watu wengine wanadhani wamepewa madaraka ili wawatawale wenzao - .. hadi namna ya kuvaa! Ok, Wakataze pia uvaaji wa kaunda suti (yanachora matumbo ya wanaume) na wanaume wasivae mashati ya vitenge (mashati ya kike)!
 
hizi haki za binadamu too much sasa ...ngoja tuendelee kulea majanga sugu kama hili la mavazi kwa sisi vijana wake kwa waume ..........UKWELI NI KWAMBA MAVAZI YANAVALIWA VYUONI NA BAADHIYA WATU KIMAADILI HAYAFAI BANA .......
DAAH UKIWA MWANAHARAKATI KWENYE HILI MHH .........
 
Wanafunzi wa College of Business Education wanatarajia kuandamana leo kupinga sheria mpya chuoni hapo inayopiga marufuku uvaaji wa suruali zinazobana, sketi, blouses na mavazi mengine yanayoacha wazi tumbo, kifua na kiuno. Pichani hapo chini ni sehemu ya tangazo lenyewe hapo chuoni likionyesha mifano ya mavazi yaliyopigwa marufuku.

552286_400391069988409_100000525597189_1458472_477520496_n.jpg

WANAWAONEA TU! Likifanikiwa hilo mtasikia wanawake ni lazima wavae baibui kwasababu mwanamke ni lazima ajisitiri. Ni mtazamo wangu
 
Watu wengine wanadhani wamepewa madaraka ili wawatawale wenzao - .. hadi namna ya kuvaa! Ok, Wakataze pia uvaaji wa kaunda suti (yanachora matumbo ya wanaume) na wanaume wasivae mashati ya vitenge (mashati ya kike)!

Tanzania hii inakera kinomba asee, kama tupo SaudiA. Khaaaa! Waacheni watu wajivalie watakavyo bana..!!
 
Mimi nawaunga mkono wanafunzi, niliangalia kwa makini zile picha za mavavi zinazokatazwa zimewalenga akina dada wenye miili minene tu. Watu wengine ndio maumbile yao sasa wafanyeje?. Kwa nini wasiitake serikali ipige marufuku kutengeneza na kuagiza nguo za kubana?. Hivi CBE ni state, province au nini? mbona ina sheria zake ambazo vyuo vingine havizifuati?. Nakubaliana na wanasema sheria hii ziweka na kiongozi mmoja mwislam hapo chuoni. Kwa nini wasipige marufu hijabu?. This is a secular state, imani zenu ni hukohuko misikitini na makanisani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom