Caught kissing on camera! do I need to bribe the IT guy? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Caught kissing on camera! do I need to bribe the IT guy?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pape, Dec 24, 2009.

  1. Pape

    Pape JF-Expert Member

    #1
    Dec 24, 2009
    Joined: Dec 11, 2008
    Messages: 5,513
    Likes Received: 26
    Trophy Points: 0
    Nanukuu...

    Mimi ni mfanyakazi wa kampuni fulani hapa Dar. Ni muajiriwa yapata miezi mi 4 sasa. Tangu nianze kazi hapo kuna dada ambaye ameonyesha kila dalili ya kutaka kuwa na mimi kimapenzi! Ninafamilia na watoto kwahiyo sipendi kujihusisha katika mambo kama hayo. Siku moja wakati wa sherehe ya kuwapongeza baadhi ya wafanyakazi huyu dada alinibana katika kona akataka kunibusu (busu kubwa) lakini nilimzuia na hakufanikiwa!

    Siku mbili baadae nilipokuwa nikiingia kazini asubuhi kwa kutumia 'elevator' mambo yalikuwa sivyo kwani dada huyo aliingia katika 'elevator' ambayo mimi nilikuwemo kupitia floor ya 2! Kwabahati mbaya tulikuwa wawili tu! Baada ya kuingia na kuanza kuelekea floor ya 6 hapo katikati alinikumbatia ghafla huku akinibusu kwa lazima! Kitendo hicho kilinihuzunisha kwani halikuwa lengo langu pia nilijua mule ndani ya 'elevator' kuna kamera za ulinzi!!

    Ilipofika saa kumi jioni mtu wa IT wa kampuni yetu alinipigia simu kwamba anamazungumzo nami na aliniambia kwamba ameona vyoote 'tulivyofanya katika elevator'

    Ameniomba nimpe Tshs. 2.5M haraka iwezekanavyo ili aweke kapuni hizo picha na kama sivyo basi atazipeleka kwa bosi!!!

    Sasa mimi uwezo wangu ni mdogo kwani hizo pesa sina...

    Je, nikambembeleze huyu IT amezee? Nikajikamatishe kwa bosi na kumueleza ukweli? Je, mke wangu akijua itakuwaje kwani nashindwa namna ya kumuelezea!!

    Naomba msaada wenu...

     
  2. Utingo

    Utingo JF-Expert Member

    #2
    Dec 24, 2009
    Joined: Dec 15, 2009
    Messages: 7,121
    Likes Received: 184
    Trophy Points: 160
    Ni wa it au security!!!!!??????? Story yako ina utata. But kama ni kweli tengeneza mazingira kila mtu ajue huyo mwanamke anakutaka kabla huyo jamaa hajakusumbua zaidi.

    Ushauri zaidi peleka issue yako takukuru watakushauri nini cha kufanya.
     
  3. pcman

    pcman JF-Expert Member

    #3
    Dec 24, 2009
    Joined: Oct 9, 2008
    Messages: 744
    Likes Received: 33
    Trophy Points: 45
    Pole sana ndugu yangu kwa Majaribu haya.Ninajua jambo moja,kweli itakuweka huru.Go tell truth and the peace of the Lord will be with you.
     
  4. Teamo

    Teamo JF-Expert Member

    #4
    Dec 24, 2009
    Joined: Jan 9, 2009
    Messages: 12,286
    Likes Received: 51
    Trophy Points: 145
    j.pape,
    mara kadhaa nimekulalamikia FONTI ya post zako lakini unajifanya kichwa ngumu!nitakupa ban kama utaendelea hivyo

    pia huyo mtaalamu wa I.T naona anataka pesa ya x-mass ingawa stori yako IMETUNGWA!
     
  5. NGULI

    NGULI JF-Expert Member

    #5
    Dec 24, 2009
    Joined: Mar 31, 2008
    Messages: 4,812
    Likes Received: 31
    Trophy Points: 135
    Story ya kutunga hii

    1. Kwa nini IT wamwite na kumhoji na sio SECURITY?
    2. Alifanyiwa au alifanya? si alifanyiwa sasa kwa nini atakwe 2.5m na sio mfanyaji ambaye ni mwanamke?
     
  6. Eqlypz

    Eqlypz JF-Expert Member

    #6
    Dec 24, 2009
    Joined: May 24, 2009
    Messages: 4,069
    Likes Received: 11
    Trophy Points: 0
    Hii story yako imepinda pinda na ina matundu kama Swiss Cheese.
    Sasa kama uliweza kumzuia siku mbili kabla ya tukio ulishindwa vipi kumzuia kwenye elevator, utakuwa na wewe ulikuwa unataka si bure, au unataka maujiko tuu uonekane kuwa na wewe ni wanted commodity.
     
  7. c

    compressor Member

    #7
    Dec 24, 2009
    Joined: Nov 26, 2009
    Messages: 76
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    nashindwa kuelewa unaogopa nini kama atelezwa boss kwamba ulitaka kubakwa ndani ya elevator,picha zitajielezea,hakuna haja ya hongo hapo.kama ulitoa ushirikiano katika kula mate,utajijua mwenyewe.kwa hapa ulichosema ni ulikuwa unalazimishwa kwa hiyo ulionyesha upinzani
     
  8. E

    Edo JF-Expert Member

    #8
    Dec 24, 2009
    Joined: Jun 11, 2008
    Messages: 728
    Likes Received: 3
    Trophy Points: 33
    Kama ulilazimishwa huna cha kuogopa, acha zionekane na ueleze stori nzima kwa huyo bosi, na kujihami muambie mkeo mapemaaaaaaaa hilo lililotokea ! Huyo changu na huyo "mlinzi" ukiwashinda kesi yako kwa bosi wataipeleka kwa mkeo. Lakini, pia si ajabu kuna mshindani wako kwenye hiyo nafasi anataka kukuharibia ili aipate yeye-watch out!
     
  9. NGULI

    NGULI JF-Expert Member

    #9
    Dec 24, 2009
    Joined: Mar 31, 2008
    Messages: 4,812
    Likes Received: 31
    Trophy Points: 135
    Waswahili sisi mh!! siku zote ndio mawazo yetu hayo. Vipi kama jamaa ni messenger.....
     
  10. s.fm

    s.fm JF-Expert Member

    #10
    Dec 24, 2009
    Joined: Jul 8, 2009
    Messages: 669
    Likes Received: 3
    Trophy Points: 35
    aaaaah...xmass ina mbinu nyingi! ila hiyo stori ungeitunga vizuri ungefanikiwa kutudanganya but kuna some points umedoda!
     
  11. Brooklyn

    Brooklyn JF-Expert Member

    #11
    Dec 24, 2009
    Joined: Mar 17, 2009
    Messages: 1,453
    Likes Received: 28
    Trophy Points: 145
    Story yakutungwa hiyo!!

    Kwani kukiss ni kosa kama mtasema mliridhia???

    Mi naamini kama hii story ni ya kweli then hakuna kosa ulilotenda hapo, eti hongo TZS. 2.5 mil.... for what...

    Pape tatizo thread zako zote ni za uongo usioendana na ukweli hata chembe!!
     
  12. Ngalikihinja

    Ngalikihinja JF-Expert Member

    #12
    Dec 24, 2009
    Joined: Sep 1, 2009
    Messages: 16,419
    Likes Received: 3,766
    Trophy Points: 280
    Kuna sera yoyote hapo kazini kwenu inayokataza yalikutokea...???
     
  13. GP

    GP JF-Expert Member

    #13
    Dec 24, 2009
    Joined: Feb 5, 2009
    Messages: 2,073
    Likes Received: 16
    Trophy Points: 135
    Uuutttuuummmbbbooo mmmtttuuupppu.
     
  14. Ngalikihinja

    Ngalikihinja JF-Expert Member

    #14
    Dec 24, 2009
    Joined: Sep 1, 2009
    Messages: 16,419
    Likes Received: 3,766
    Trophy Points: 280
    Wenzio twalia ndiziiiiiii ................:)
     
  15. GP

    GP JF-Expert Member

    #15
    Dec 24, 2009
    Joined: Feb 5, 2009
    Messages: 2,073
    Likes Received: 16
    Trophy Points: 135
    mkuu!!,
    MERRY XMAS
     
  16. C

    Chupaku JF-Expert Member

    #16
    Dec 24, 2009
    Joined: Oct 15, 2008
    Messages: 1,045
    Likes Received: 132
    Trophy Points: 160
    Duh, nakumbuka watoto wa kike wakati nasoma primary walikua na siku zao wanasutana, wambea na waongo wanawekwa kati wanasutwa kwa kutumia majivu. Pape, pole. Umesutwa sana leo. Ndio zawadi yako ya XMAS hiyo. Sina comment juu ya story yako.
     
  17. Pape

    Pape JF-Expert Member

    #17
    Dec 24, 2009
    Joined: Dec 11, 2008
    Messages: 5,513
    Likes Received: 26
    Trophy Points: 0
    Ndio maisha hayo...amini usiamini hiyo kitu imetokea kweli...
     
  18. Pape

    Pape JF-Expert Member

    #18
    Dec 24, 2009
    Joined: Dec 11, 2008
    Messages: 5,513
    Likes Received: 26
    Trophy Points: 0
    Tunga yakwako halafu iweke jamvini...

    For your information you are NOT forced to go through my threads, HATER
     
  19. Pape

    Pape JF-Expert Member

    #19
    Dec 24, 2009
    Joined: Dec 11, 2008
    Messages: 5,513
    Likes Received: 26
    Trophy Points: 0
    ukome na ukomae...anzisha yako ambayo ni nyama....hater...
     
  20. Chimunguru

    Chimunguru JF-Expert Member

    #20
    Dec 24, 2009
    Joined: May 3, 2009
    Messages: 9,843
    Likes Received: 270
    Trophy Points: 180
    Sidhani kama IT wanahusika na camera za majengo lazima itakuwa ni Security company, kingine kwani camera zimewekwa kukamata watu wanaomegana au wezi? kuna sheria yoyote hapo kwenye JENGO hilo zinazokataza watu wasi KISS? maana naona siku hizi watu wengi wana kisiana midomoni(LIPS) lkn si kufika kula denda na ku HUG vizuri tuu. Jamani mwanaume huwa habakwi, najua ulitoa ushirikiano na nadhani ukaenda mbele zaidi kwenye KUPIMA OIL (maana hamchelewi nyie) saa jamaa alivyoona akajua kapata MTAJI, sasa anakutishia ili umpe 2.5M, nenda TAKUKURU, mtegeshee mtego, mwombe hata namba yake ya simu au e-mail mtumiane mail mbili tatu za kutengeneza ushahidi, ili siku takukuru wakimnyaka kwenye huo mtego uwe na ushahidi mwingine. Kuwa mwangalifu sana mwambie mkeo tukio lote najua atamind lkn haitakuwa mbaya sana kama akiambiwa na mtu juu ya tukio hilo
     
Loading...