Catherine Ruge: Rais Samia anawanyima Wazanzibar wenzake fursa ya kuwa nchi yenye Mamlaka kamili

Halafu akilinda maslahi ya Zanzibar atalaumiwa kama JPM kwa "ukanda/ukabila."

Dear Chadema, jitahidini kufahamu vipaumbele vya Watanzania kisha muwe kipazasauti cha vipaumbele hivyo. Kadhalika, jibidiisheni kusoma upepo wa kisiasa ulivyo. Mama Samia anapendwa na Watanzania, pengine kutokana na kuwa Rais wa kwanza mwanamke. Lakini pia anaongea lugha ya kistaarabu. Sasa mkicheza ovyo karata zenu, mtaishia kuonekana mnam-bully.

Mwisho, mjibidiishe kuwa proactive. Anzisheni mijadala itakayowafanya Watanzania wafanye tafakuri badala ya sasa ambapo mnaendeshwa kwa matukio. Mnasubiri Mama Samia atamke hili au lile mpate cha kuongea.

Povu ruksa 😊
Katiba mpya KWANZA.
Twahitaji kujenga taasisi imara ili kuimarisha utawala bora. Nchi yahitaji kuongozwa kwa sheria zinazolinda haki za waTz na sio kutegemea matamko yanayoeleaelea.
Mijadala yenu pendwa ya kwenye mbio za mwenge haijawahi kusaidia TAIFA hili.
 
Muungano ni kama NDOA YA WAZAZI WAKO iliyofungwa kabla ya wewe kuzaliwa.....

Hauhojiki KUPITILIZA....
Hauvunjwi......
Hauvunjiki......

Hapa "UAMSHO" wanaweza kutupa funzo kubwa......

#KaziIendelee
Pole ndugu,
Sijui ni nani aliyekulisha porojo hizo.
Kilichokuja kwa 'maridhiano' chaweza pia kuhojiwa, kuboreshwa na pale itakaposhindikana, hata kufikiria kuvunjwa ili kuleta amani.
 
Pole ndugu,
Sijui ni nani aliyekulisha porojo hizo.
Kilichokuja kwa 'maridhiano' chaweza pia kuhojiwa, kuboreshwa na pale itakaposhindikana, hata kufikiria kuvunjwa ili kuleta amani.
Amani ipo....
Amani tunayo....
 
"Niko Unguja na Wazanzibari wanamwambia Mama Samia "Kitendo cha yeye Kuzuia madai ya Katiba Mpya ni kuwanyima Wazanzibari fursa ya kuwa nchi yenye Mamlaka kamili, wanamkumbusha kuwa yeye kama mzanzibari anatakiwa alinde Maslahi ya Zanzibar asilewe Madaraka"-CPA Catherine Ruge

Waambie wanyamaze sana sana wamwambie ahakikishe anaiendelea sana zanzibar kwa Tanganyika kulipa gharama. katiba mpya haitaruhusu mzanzibar kutawala bara.
 
Ni vyema Wazanzibar wakaonesha msimamo wao mapema wakati huu Rais wa Tanzania akiwa ni Mzanzibari mwenzao. Badala ya kulilia usawa usio na tija kivile, wangeipambania Katiba Mpya inayotambua uwepo wa Serikali Tatu.

Kinyume na hapo, kero za Muungano hazitokuja kuisha kamwe.
Hakika kabisa.
 
Back
Top Bottom