Catherine Ruge: Kakoko alinitishia kuniua baada ya kuibua madudu mengi TPA

Ujinga kama virusi. Unaelewa kweli maana ya ukoloni. Nyie kama hamnaga cha kuandika. Mjiue tu.
Hatujiui ng'o! Tutabanana hapa hapa huku tukiwaambieni ukweli wa uhujumu nchi wenu. Watu wanakufa umaskini nyie mnauita uhuru huo? Hebu tembelea mahospitali makubwa ukaone binadumu wenzio wakikosa matibabu wakiachwa kujifia pole pole.
 
Acha uwongo unaweza bainisha hapa ukatili wa kakoko ulikuwa wapi? Na tangu wamchunguze je alishawahi kufikishwa mahakamani? Vijana fanyeni kazi acheni majungu kwa wakubwa zenu
Kakoko alikuwa mtu katili sana akiamini kuwa Magufuli angeishi milele. Alikuwa anatumia muda mwingi TPA kuliko hata nyumbani kwake. Alikuwa ni mtu wa mipango ya wizi tu huku akigawana na Magufuli.
 
Story hapo ni ya Ndugai huyo Kakoko hana story hapo
Na hilo ndiyo lengo la thread na ni bora umelibaini, majority wameshindwa kubaini story halisi ni ipi wako busy wanapambana na kivuli.
 
Aaaagh atupisheee naye!
Angemwambia hata kigogo amsaidie kutoa hizi taarifa!
Sisi tuko na Job, #wapi_Job
Anasema sasa hivi ili iweje??
 
Sijachanganya mafaili ndio huyu msimbe anayeng’ang’ania wanaume za watu na kuishia kufanya fujo hadi kwenye misiba ya watu.

Baada ya kupoteza ubunge amekuwa kama kachanganyikiwa.
Acha ubishi..Wa CCM Magige ,ndiyo alizua Timbwili
 
Aliyekuwa mbunge wa viti maalum CHADEMA na Katibu mkuu BAWACHA ndugu Catherine Ruge amedai kwamba wakati akiwa mbunge akifanyia kazi kamati ya PAC alitishiwa kifo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini TPA ndugu Kakoko ambaye alikuja kutumbuliwa kwa tuhuma za ufisadi na kushtakiwa mahakamani.

Hali hiyo ilikuja baada ya yeye kuibua Madudu mengi ya ufujaji wa pesa katika Mamlaka hiyo na kubainisha kuwa kulikuwa na baadhi ya watumishi wazalendo wa kutoka mamlaka hiyo walikuwa wakimpa nyaraka za ndani za matumizi mabaya ya pesa ambazo Bwana Kakoko alikuwa akizificha.

Akiongea kwa njia ya mtandao kupitia mjadala unaoendeshwa kupitia mtandao wa Clubhouse, Pia ndugu Catherine Ruge alisema amedokeza anashangaa watu wakihoji alipo aliyekuwa Spika wa bunge ndugu Job Yustino Ndugai wakati yeye anafahamu kuwa yupo Katika matibabu hospitali ya Apollo nchini India na Kuna ulinzi mkali umeimarishwa katika mahali alipo mgonjwa.

Taarifa za kuugua kwa Ndugai, Catherine Ruge amedai kuwa amezipata kutoka kwa mdogo wake ambaye walikuwa wakitibiwa pamoja katika hospitali hiyo.
CHADEMA wameanza kuwa movie stars - akiona ameanza kupoteza soko hapo hapo anaita magazeti kumhoji akisema "I WAS RAPPED IN SCHOOL". Hapo hapo chati zinapanda tena.
 
Alitoa taarifa polisi?

20220128_221738.jpg
 
Back
Top Bottom