Cartoon Yenye Ujumbe Mzito! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cartoon Yenye Ujumbe Mzito!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 27, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 27, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Na. M. M. Mwanakijiji (Tanzania Daima)

  MARA baada ya Rais Kikwete kumaliza kuhutubia hotuba yake iliyokuwa inangojewa kwa hamu na Watanzania, nilijikuta katika mawazo yangu yaliyopotoka nikimuona Rais Kikwete kama “baba” wa ule mchezo wa utotoni wa ‘watoto wangu eh!’

  Niliweza kumuona upande mmoja Rais Kikwete akiwa amesimama na kuwaangalia Watanzania na huku akijibizana nao katika kuwatahadharisha kuhusu simba aitwaye fisadi. Ilikuwa hivi:

  JK: “Watanzania eh”

  WTZ: “Eh”

  JK: “Mimi Rais wenu!”

  WTZ: “eh!”

  JK: “Sina nguvu tena!”

  WTZ: “Eh”

  JK: “Ya kukamata mafisadi”

  WTZ: “Eh”

  JK: “Mafisadi ni wajanja”

  WTZ: “Eh”

  JK: “Wamekomba Benki Kuu” Watoto wanaendelea kuitia “Eh” kwa shauku!

  JK: “Wamelangua na Rada”

  “Wameiba Meremeta”

  “Wamechota nayo EPA”

  “Na makampuni mengine”

  “Sasa kimbieni!

  Watanzania kila mmoja anavyojua anaanza kutimkia kwake na kufanya mambo yake kuokoa maisha yake na ya familia yake. Kwa hakika hivyo ndivyo nilivyomuona Rais Kikwete.

  Katika makala yangu ya wiki iliyopita yenye kichwa cha habari: “Macho ya Taifa yanakutazama Kikwete”, nilisema kuwa hotuba ya Rais Kikwete inaweza kuwa ni ya kuleta matumaini au ya kukata matumaini.

  Na nilisema kati ya mambo mengi ambayo wananchi walikuwa wanasubiri kuyasikia ni suala la Zanzibar na maamuzi ya suala la EPA.

  Kuhusu Zanzibar nilisema kuwa: “La maana katika kujadili matatizo ya ndoa yetu ni kusema kuwa kwanza ndoa ipo na halali; kwamba Muungano upo na halali.

  Na la pili ni kukubali ‘on principle’ and in fact kuwa zile nchi mbili zilizoungana hazipo tena (siyo kuwa moja ipo nyingine haipo) na kilichopo ni nchi moja.

  Ni kutoka hapo ndipo mjadala wa kero za Muungano unaweza kufanyika. Hili la kusema ati mmoja bado ni nchi na mwingine siyo nchi ni kuzugana. Je, Rais Kikwete alikisema hiki?

  La hasha! Rais Kikwete alijaribu kwa kiasi kikubwa kujibu suala la Zanzibar ni nchi au si nchi lakini kwa kufanya hivyo akawa amejiingiza kwenye tatizo jingine. Kwa maoni ya Rais katika mambo yetu ya nje na mahusiano na mataifa mengine nchi ni ‘Tanzania’. Katika mambo yetu wenyewe nchi ni ‘Zanzibar’ na nchi ni ‘Tanganyika’.

  Kwa maneno mengine Rais wetu anaamini kuwa kuna nchi tatu! Kuna nchi moja ambayo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ndani yake kuna nchi mbili, ambazo bado zipo nazo ni Zanzibar na Tanzania.

  Hili linapinga kauli yake ya awali kwenye hotuba hiyo kuwa nchi hizo mbili ‘zilisalimu’ mamlaka yake na kuunda nchi moja Aprili 26, 1994.

  Kwamba nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika ziliamua kutoweka ili kujenga nchi moja yenye mamlaka yote ya nchi (sovereignty).

  Rais Kikwete alishindwa kuitetea Katiba kwa kuweka wazi kuwa nchi hiyo moja (kwa mujibu wa Katiba Ibara 1- 4) inaongozwa na serikali mbili (si nchi mbili).

  Katiba inaeleza wazi kuwa nchi hiyo moja iitwayo Tanzania, inaongozwa na Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, si Serikali ya nchi ya Tanganyika na Serikali ya nchi ya Zanzibar.

  Sasa haya siyo maneno ya Mwanakijiji, bali ndivyo ilivyo katika mkataba wa Muungano ambapo inasemwa hivi: “Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitaungana na kuwa Jamhuri moja ya hakimiya.”

  Na katika mkataba huo huo unaelezea kuwa Rais wa Zanzibar “atakuwa ndiye msaidizi wa Rais wa Jamhuri katika kuendesha na kusimamia Serikali ya Zanzibar”.

  Hivyo mkataba wa Muungano wa awali ulimweka Makamu wa Rais wa Muungano (kati ya makamu wawili) kuwa ndiye atakuwa Rais wa Zanzibar.

  Sitaingia kwa undani suala hilo, lakini ukweli ni kuwa walioboronga na kuharibu ni pale wakati wa kuandika Katiba ya Kudumu mwaka 1977 na mabadiliko yake ya 1984, ndipo walipovikoroga vipengele vya Muungano wetu.

  Ni hapo ndipo tulipoanza kupotea kweli kweli na ndipo ambapo sisi wengine tuliamini kuwa Rais Kikwete angeweza kuonyesha njia ya kurudia.

  Hakufanya hivyo na badala yake kudai kuwa “nchi ya Tanganyika” nayo ipo, kitu ambacho wote tunajua haipo (isipokuwa kwenye mawazo ya Mtikila na Watanganyika wengine).

  Lakini Kikwete alisema kweli pale alipohamaki kuwa “kama kuna jingine waliseme” wale wanaoendeleza mjadala huu.

  Kitu ambacho mimi niliandika wazi kwenye makala ile na kusema wanachogombea Zanzibar si “nchi au ni nchi”, kwa sababu Mkataba wa Muungano upo na unajulikana.

  Wanachogombea nilisema “ndugu zetu wa Zanzibar wanapigia kelele kuwa si nchi, wanachogombania kwa kweli ni kuwa nchi kamili, kisheria na kwa kila hali.”

  Na nikisema kama mtu haamini maneno yangu, Rais Kikwete asikike akitangaza kuwa Tanzania ni nchi moja na Zanzibar ni sehemu ya Muungano, si nchi.

  Zanzibar hakutakalika, kwani CCM Zanzibar itameguka kutoka Bara, watashikamana na CUF na kwa pamoja watatangaza nchi huru.

  Kikwete hakuwa na ujasiri wa kusema embe ni embe na chungwa ni chungwa, licha ya uwezo na mamlaka yote kuwa nayo. Akabakia kulia tu ‘sina nguvu tena.’

  Kwenye suala la EPA niliandika hivi wiki iliyopita hata kama Rais Kikwete atatangaza hatua dhidi ya watu na makampuni yaliyochukuliwa hatua, kufilisiwa au kurudisha fedha, ukweli utabakia kuwa pongezi hizo atazipata Kikwete.

  Nilisema hivyo kwa sababu kina Mwanyika walishindwa kufanya walichoagizwa na Rais kufanya.

  Na leo tumesikia Rais Kikwete akitangaza kwa majigambo kuwa watuhimiwa hao wamenyang’anywa pasi zao za kusafiria, magari na majumba na ati wana hali mbaya kweli.

  Katika mawazo yetu ya kupenda kuzugwa tukashangilia na kupiga makofi. Hatukujiuliza hayo magari yaliyofilisiwa yameegeshwa wapi? Wapiga picha huru waonyeshwe magari hayo! Vinginevyo yamefilisiwa na kupigwa mnada na walionunua ni wakuu wengine wa serikali!

  Yaani vyawezekana vimetoka kwa fisadi huyo kwenda kwa “potential fisadi”.

  Hatukujiuliza hayo majumba yaliyokamatwa yako vitalu gani, maana hata kibanda cha nyasi nacho ni nyumba!

  Leo hii makundi ya watu wamevaa njano na kijani wanaandamana kuunga mkono maneno. Wakati wengine tulifunga safari kutembea miguu kuunga mkono Azimio la Arusha lilioendana na vitendo thabiti leo hii kwa kupenda kuzugwa tumejikuta tunaandamana kushangilia maneno na si vitendo.

  Tunakumbuka tulivyoimba wakati ule ‘mabepari walia, mabepari walia, kukatiwa mirija, walipotangaziwa, walipotangaziwa Azimio la Arusha.”

  Hivi baada ya hotuba ya Kikwete mnafikiri kuna fisadi yeyote analia kwa sababu amekatiwa mirija ya ufisadi?

  Rais amebakia kusema tu “mimi rais wenu, sina nguvu tena”.

  Lakini cha kufurahisha zaidi ni pale alipodai kuwa ana nguvu za kumsweka mtu yeyote ndani na maswali baadaye.

  Walio waoga wakaamini maneno hayo. Wapo walioamini kuwa Rais wa Tanzania ana nguvu ya kuamuru Mtanzania akamatwe pasipo sababu yoyote na nje ya sheria.

  Yaani rais aote ndoto “mwanakijiji anamboa” halafu kesho yake asema mkamateni mwanakijiji!

  Nguvu hizo hana, hajawahi kuwa nazo katika Tanzania huru, na kama kuna mtu amemdanganya kuwa anazo, huyo mtu atimuliwe kazi!

  Rais wa Tanzania ana nguvu ambazo tumempatia kikatiba na kisheria.

  Nje ya hapo hana nguvu zozote zile. Mahali pekee ambapo Rais wa Tanzania anaweza kujihisi dikteta ni pale atakapotumia sheria ya madaraka ya Rais wakati wa hatari (Emergency Powers Act) ya mwaka 1986.

  Hata hivyo pamoja na sheria hiyo, nayo inaweka mipaka ingawa inampa rais uwezo mkubwa sana.

  Hata hivyo nguvu hizo zinaingia tu pale ambapo rais ametangaza hali ya hatari, na kwa kadiri ninavyojua mimi Tanzania haijatangazwa hali ya hatari.

  Sasa kama kina Mwanyika wamemzuga Rais kuwa ana nguvu za kufanya lolote kwa kutumia sheria hiyo pasipo kutangaza hali ya hatari na wao wakaenda kuwanyang’anya watu mali zao na hati zao kwa sababu “Rais kaagiza”, naamini ni kinyume cha sheria na wale ndugu walionyang’anywa mali zao wana haki ya kwenda mahakamani kudai warudishiwe.

  Sasa ninaelewa kwa nini serikali haikutaka kwenda mahakamani.

  Inaogopa kuumbuliwa. Mara nyingi serikali imekuwa ikidai kama una ushahdi wa ufisadi wa mtu nenda mahakamani. Leo hii wao wana ushahidi mkubwa wa wizi wa EPA na mambo mengine lakini wamekuwa wa kwanza kukwepa mahakama.

  Wakati sisi vidagaa tunaambiwa tukiwa na ushahidi dhidi ya kiongozi yeyote basi twende mahakamani, wao ambao wana ushahidi wa wizi, kughushi, na matumizi mabaya ya madaraka wanakwepa mahakama hizo.

  Sababu kubwa na ya kipuuzi ni kuwa ati wakienda mahakamani watuhumiwa wanaweza kushinda kesi na fedha zisirudishwe na wao wasikutwe na hatia.

  Hii ni sababu ya kijinga kwa sababu mahakama ndio mahali ambapo ukiwa na mashtaka dhidi ya mtu, ukweli utachambuliwa ili kuona haki inapatikana.

  Kama utashindwa kuthibitisha kuwa alifanya unachodai kufanya, basi ni kosa lako wewe mwenyewe na watu wakifunguliwa ndio utawala wa sheria.

  Si wengi tunakumbuka kisa cha kada wa CCM kule Arusha aliyetuhumiwa kufanya ujambazi, mahakama ya chini ikamuona kuwa na hatia na baadaye mahakama ya juu ikaamua kumuachilia kutokana na ushahidi dhaifu.

  Si tunakumbuka kesi ya Rage na jinsi alivyoanza kutumikia kifungo na baadaye kuachiliwa? Si tunakumbuka kesi ya Nalaila Kiula, ambaye naye baada ya kudaiwa kuwa ni fisadi, alijikuta akiachiliwa na mahakama?

  Jamani, hivyo ndivyo mahakama zinatakiwa kufanya kazi.

  Kwa serikali kutokwenda mahakamani imeonyesha kuwa inatafuta haki kwa upendeleo au uonevu.

  Serikali ikienda mahakamani mashahidi wataitwa, ushahidi utawekwa hadharani, na watuhumiwa wataweza kujitetea na pia kuwahoji wanaowatuhumu, hiyo haki ya mtu kufikishwa mahakamani (Habeas Corpus) ni haki ya msingi.

  Lakini serikali yetu inaonekana wameamua kwenda nje ya utawala wa sheria.

  Naamini wale wanaotuhumiwa kuiba EPA wataaamua kufanya kile ambacho serikali haitaki kufanya, nacho ni kwenda mahakamani kupinga maamuzi hayo ya serikali.

  Hatuwezi sisi kama taifa kukubali kuwa na mifumo sambamba ya sheria ambapo mwizi wa kuku anakamatwa na kufikishwa mahakamani na haambiwi aende kutafuta kuku mwingine arudishe bali anakutana na mkono mrefu wa sheria wakati walioiba mabilioni ya EPA wanapewa karibu miezi nane ya kutafuta fedha na kuzirudisha.

  Lakini wakati huo huo Rais anasema ana mamlaka makubwa.

  Yaani ana mamlaka makubwa ya kushindwa kuagiza sheria ifuatwe, yaani ana mamlaka makubwa ya kukubali kupokea ripoti ya kitu ambacho hakuagiza, yaani rais wetu ana mamlaka makubwa ya kutuzuga, tukazugika!

  Kilichonishangaza mimi zaidi ni jinsi gani baadhi yetu wanapenda na wanafurahia mazingaombwe.

  Niliandika siku chache kabla ya hotuba kule kwenye mtandao wa Jamiiforums.com kuwa mwishoni mwa wiki mtasikia watu wakiandamana kupongeza hotuba ya rais.

  Niliyasema hayo kabla ya kusikia hotuba yenyewe! Sikuhitaji kuisikia na sikuhitaji kukisia mwitikio wa watu.

  Ni jambo ambalo sasa hivi tunalielewa ni hulka ya Watanzania. Tumeacha kushangilia vitendo na sasa tumebakia kushangilia maneno.

  Na wiki hii yote mtaendelea kusikia mikoa mbalimbali na jumuiya mbalimbali zikipongeza hotuba ya rais na sitashangaa mtaona kwenye magazeti wakianza kutuma salamu za pongezi kwa hotuba.

  Watasimama watetezi wa maneno kuwa hotuba ilikuwa ni nzuri, imekuja wakati muafaka, na imeonyesha kuwa Kikwete yuko makini! Kumbe walichofanyiwa ni mchezo wa “watoto wangu eh!”

  Yaani Watanzania tunaambiwa kuwa Tanzania sasa si kichwa cha mwendawazimu, bali ni kinyozi, tunaandamana kushangilia ingawa wenyewe tumeshuhudia kuwa tunashindwa hata kulinda goli letu moja hadi tunafungwa na golikipa! Wenyewe tunasema tumefanikiwa katika soka.

  Binafsi ningeona Watanzania wameamka kama wangeunga mkono maneno machache aliyosema Spika Sitta ambayo ilikuwa ni kuwaambia wenye mamlaka ukweli (speaking truth to power).

  Maneno ya Spika ya dakika saba ndiyo ambayo wengi wetu yalitupa faraja na matumaini kuliko maneno ya saa tatu na nusu ya rais.

  Rais angeweza kusema alichosema ndani ya saa moja na mafanikio ya serikali yake angemuachia Waziri Mkuu atakapoahirisha Bunge baadaye siku chache zijazo.

  Sasa namuonea huruma Pinda sijui na yeye ataimba sifa gani za Serikali ya Awamu ya Nne.

  Nasema tukubali tu yaishe. Tukubali kuwa miaka miwili na nusu iliyopita tumeuziwa mbuzi kwenye gunia na tulichopata ndicho tunachostahili.

  Tukubali ya kwamba miaka miwili ijayo haitakuwa tofauti na iliyopita, kwani kama wameshindwa kumkunja samaki angali bado mbichi wataweza akikauka?

  Tukubali kuwa tulifanya makosa tulipomchagua Kikwete na sasa aidha tuangalie humo humo CCM au nje yake, mtu ambaye ataliongoza taifa letu kwenye neema ifikapo 2010.

  Mwenzenu nimeshaamua kuwa mhula mmoja wa utawala wa Kikwete unatosha. Tumuombee uzima na afya, ili aendelee kuitawala nchi yetu kwa amani, umoja na mshikamano.

  Tumuombee aendelee kuvuta muda hivyo hivyo na ufisadi ili hatimaye wananchi wauchoke kweli kweli.

  Na tumuombee kuwa ifikapo 2010 atatambua kuwa hana sababu ya kugombea tena urais, na yeye mwenyewe kwa kutumia hekima na busara ataamua kumpisha mwana CCM mwingine au rais mwingine kutuongoza kwenye neema ya kweli.

  Inawezekana ni kweli yeye ni chaguo la Mungu, saa na wakati huu ili kutuonyesha Watanzania kuwa kuanguka kwa CCM kumeanza. Yawezekana kama vile Farao alivyosimamishwa na moyo wake kufanywa mgumu ili wana Waisraeli waondoke Misri kwa mkono wa maajabu wa Mungu.

  Yawezekana Kikwete naye amesimamishwa ili Watanzania hatimaye tuuone ukuu wa Mungu. Kwani na sisi tunastahili nchi ile ya ahadi, inayotiririka maziwa na asali, ambapo mafisadi hawawezi kukinga mikono tena kuchota.

  Hata hivyo Kikwete bado anaweza kuokoa urais wake na kujipa nafasi nyingine. Nitakuambia wiki ijayo kwa vipi.

  “Watanzania eh!”

  NB: Asante Said Michael kwa kuchora katuni hii kwa muda mfupi. Ubarikiwe. Kazi zake nyingine zinaonekana kwenye kijarida na kwenye bulogu yake HAPA
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mwanakijiji nakumbuka kwenye ule mchezo wa watoto wangu ee....mwisho unaambiwa "haidhuru piteni" ....
  sasa na JK nae kasema natupite tu, atakaekamatwa na ufisadi na yeye akawa fisadi ni sawa, atakae amua kupita kwa njia nyengine ni sawa......YEYE hana tena nguvu na tusimtegemee
   
 3. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Suala la hao mafisadi kuwa katika hali mbaya ni la uongo sana!Benson wa Arusha na Njake wote wa Arusha ni moja kati ya watu waliopo huko EPA.Benson angekuwa na hali mbaya angekuwa naendesha Range Rover Super Sport?JK asitufanye wajinga bwana!
  Mh Mwnakjj huyu JK ni mroho wa madaraka maana he is evrywhere!hatweza kumuachia mtu mwingine madaraka coz anataka kila baada ya Mwenzi mmoja aende US akasalimie vimada vyake huko!
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mambo yote haya JK kayasemea BUNGENI. Bunge ambalo KIKATIBA linammudu RAIS wetu.
  Ni nini kinawatokea Wabunge wetu?
   
 5. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Dawa ni kuwanyima kura wale wote wanao support ufisadi na JK wao ambao wamedhamiria kuwafanya Watanzania maskini zaidi na zaidi!Tunahitaji new brains and fresh minds to take over the parliament!
   
 6. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2008
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mwanakijiji maelezo yako yamegusa pande zote, kwa mtizamo wangu naona huyu mh staili yake ya kuongoza inaendana mno na wakati wa ruksa kila mtu kufanya atakalo ili kuweza kuishi. Hali hii ni mbaya sana, Watangzania inabidi tufungue macho na masikio, tuangalie na kusikiliza yanayofanyika kwa wenzetu. Dunia inabadilika kwa kasi mno, Watanzania hatuwezi kujitenga kwenye mabadiliko hayo. Kama kuna vikwazo lazima tuungane kuviondoa ama kujinasua kutokana na vizingiti hivyo. Dunia ya mwaka 1985 sio Dunia ya mwaka 2008. Tuna uwezo wa kusema HAPANA kwa viongozi wanaotuongoza ndivyo sivyo. Tuache kudanganywa kwa maneno ya kejeli kutoka kwa watu kama Makamba, tuache kushabikia mambo ambayo hayajisimamii hata yakiwekewa nguzo. Wabunge wetu naomba mtafakari maneno machache ya kiranja wenu Samwel Sita, mnayo nafasi kubwa ya kusema imetosha na wananchi tutawapa support.
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2008
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,655
  Likes Received: 21,868
  Trophy Points: 280
  swali la msingi kabisa. Kama kuna wa kulaumiwa basi ni bunge kwa kumlea raisi aliyeshindwa kutimiza wajibu wake.
  Kungekuwepo walao hata jaribio moja la kupiga kura ya kutokuwa na imani naye,hata kama lingeshindwa ni wazi angerekebika kwa kuona wabunge hawataki blabla.
   
 8. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi binafsi nadhani Spika Samuel Sitta apewe sifa kwa kufanya yale anayosema kwa kiingereza "to walk the talk." Ndicho alichokifanya 21 Aug 08. Aliwahi kuwaambia wabunge kwamba yeye sio mwoga wa kuongea analoliamini na alifanya hivyo baada ya Rais kumaliza hotuba. Kwa kifupi Spika alimwambia JK kwamba pamoja na hotuba ndefu na maneno matamu hotuba yake haikukidhi kiu ya watanzania! Mwenye masikio na asikie.
   
 9. H

  Haika JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  MIMI BADO SWALA LA KUWA HELA SI YA WATANZANIA BADO SIJALIELEWA VIZURI.
  NACHUKULIA MFANO, NIMEJITENGEA HELA YA KULIPA DENI FULANI, JAPO BADO SIJALILIPA, HELA NIMEISHIKA, IKIIBIWA, NITAPATA WAPI BAJETI YAKULIPA DENI KAMA SI MFUKONI KWANGU?
  KWA HIO MIMI BADO NAONA HELA HII YA WATU, MAADAMU ILIKUWA MIKONONI MWETU, KWA DHAMANA YA SERIKALI AU CHOMBO CHA SERIKALI, TUKIDAIWA SERIKALI INABIDI ITOE FUNGU KULIPA HAO WADENI WA NJE, KAMA HILO FUNGU HALIONEKANI, SI LAZIMA WANGEMEGA KODI ZETU? AU WANGEFANYAJE?
  NDUGU ZANGU NAOMBA UFAFANUZI MWENZENU HAPO?

  Nilikutana na 'mtuhumiwa' mmoja wa EPA akawa anasema kuwa hawangeweza kushtakiwa kwa kuwa hawajaiba, ila waliingia tu mkataba kuchukua hela fulani sehemu, manake ilikuwapo tu, yeyote ambaye angejua angeweza kuchukua kufanyia shughuli zake. kwa hiyo wakirudisha ni basi, hakuna sheria ya kuwashtaki,
  eti ni kweli?
   
 10. H

  Haika JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  ni kwa sababu hii mimi naomba rekodi ya kila mbunge, binafsi yake ya maamuzi/msimamo/au upande anaoegemea wa kila mjadala bungeni uwekwe wazi kwa kumbukumbu zitakazotumika wakati wa kugombea tena.
  kwa sasa ni wale wenye kumbukumbu tu au waandishi ndio wanaoweza kujua huyu mbunge alikuwa anapendelea/anakubaliana na swala gani, au alichangia kwa kiasi gani maamuzi fulani kuchukuliwa na bunge.
  Napendekeza kuwa kila jambo/neno lipigiwe kura na mbunge bungeni ili aje aweze kusimamia na kufungwa na maneno au kura yake mwenyewe.
  tunataka kujua wabunge wanaokubaliana na hotuba ya raisi, wanaotaka muungano kama ulivyo, wanaotaka marekebisho ya katiba, na kadhalika kusiwe na kificho. kificho au siri kunaongeza unafiki ambao unaiua nchi.
   
 11. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  MWkjj
  Si ulisema unastaafu JF mpakam sijui memba afikishe post elf ngapi? Duuuuuu kazi kweli kweli.
  Ama ulikua una beep kama DR Idrisa ,kwi kwi kwi kwi kwi wewe uki beep sisi tunapiga kabisaaa.
   
 12. Mujuni2

  Mujuni2 Senior Member

  #12
  Aug 27, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hebu soma hii ya Prof
  Soma hii ni mtazamo wa Prof Baregu kuhusu the recent speech ya JK...[/B]

  Kwa kusikiliza hotuba ya raisi ya leo kumenifanya nibadili mtizamo wangu kwa kiasi kikubwa sana ; Kawaida yangu siyo kwenye siasa tu lakini hata katika maisha ya kawaida napenda kuamini kuwa wanadamu ukiwapa nafasi ya kufanya wema watafanya wema; Nimejifunza kumpa mtu nafasi ya kukosea na kujisahihisha. Nimejifunza kutokuwa na hukumu kali sana kwa mwanadamu mwingine.

  Lakini katika hilo pia nimejifunza kuwa kuna mipaka isiyovukwa na kuna mambo ambayo mtu hatakiwi kupewa nafasi ya pili. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikiamini kuwa somehow Kikwete atajikuta anakaa peke yake na kujikuta yuko peke (alone and lonely) na kutambua uzito alionao wa kuliongoza Taifa. Nimekuwa nikitumaini na kuombea kuwa Kikwete atatambua wajibu wake mkubwa na kuamua kufanya kile ambacho viongozi wa kweli hufanya.

  Hivyo mara kadhaa (wakati Baraza limevunjika) niliamini kuwa JK atasimama na kuuteka wakati na hivyo kuanza upya; haikutokea hivyo. HIvyo hotuba hii jinsi ilivyopambwa na kutokea kwake wakati na saa kama hii niliamini kuwa labda amejifunza kitu na sasa yuko kweli anataka kufanya kitu; nilikuwa nimekosea.

  Kikwete hawezi kuongoza; Kikwete si kiongozi ni mwanasiasa mpiga porojo; Kikwete si kiongozi ambaye Watanzania walitarajia kuwaongoza kutoka kwenye kilindi cha umasikini kuelekea kwenye mafuriko ya mafanikio. Rais Kikwete na niliandika wiki mbili zilizopita ni mtu ambaye amepewa nafasi nyingine kufunga goli ambapo amebakia yeye na golipa na mara zote amekuwa akifika golini anabakia kukaa chini na kusubiri mtu mwingine aje ampasia afunge goli wakati mashabiki wamekaa pembeni wakishangalia na kuombea afunge kwa sababu ni Kapteni wa timu na alinunuliwa kwa bei kubwa.

  Unaposhinda uchaguzi kwa zaidi ya asilimia 80 unaweza kabisa kusababisha mabadiliko makubwa ya Kitaifa na kuongoza Taifa. Unapopata support ya watu wa mjini na kijijini, maskini na matajiri unakuwa na mtaji mkubwa wa kisiasa ambapo ni wewe tu unajua ukiuwekeza vizuri utalipa. Lakini kwa kushindwa mikakati, kugwaya, kuogopa kuudhi watu n.k unabakia na mtaji huo ambao pole pole unazidi kumemenyuka.

  Kikwete ni kilele cha kukatisha tamaa na mfano dhahiri wa nini kiongozi asiwe. Kikwete anasimama leo hii kama kiongozi ambaye ameshindwa kuongoza na anabakia kuitwa kiongozi. Rais Kikwete amebakia kuwa yule mwenye "simba wa kuchora" ambaye anasimama kuunguruma kwenye picha na watoto wanabakia kucheka.

  Leo kwa hakika ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Rais Kikwete kuonesha uongozi Tanzania badala ya kupiga zogo. Kama alitaka kuelezea hali ya Muungano wetu na ya Taifa yetu alikuwa na wakati mzuri pale Aprili 26, Mei Mosi, Nane Nane n.k au kila mwanzoni mwa mwaka kama wanavyofanya Wamarekani. Lakini hili la kuiweka roho juu nchi na kwenda na magwaride na uongozi mzima wa serikali kwenye hotuba maalumu ya Rais Bungeni ni kuchezea hisia za wananchi. Ni kutuzuga kulikotukuka ambako kwa hakika kunamfanya astahili kupewa nishani iya Uzugaji uliotukuka daraja la kwanza na la pili!

  Rais anapoenda kuzungumza Bungeni iwe kwa kweli jambo muhimu, zito, na ambalo kwa hakika linastahili mahali kama hapo. Kusimamisha shughuli za Bunge ili uje upigiwe makofi na saluti wakati mijadala muhimu ya Taifa inaendelea ni kuwapotezea muda wananchi na wabunge. Hotuba yake jinsi alivyoitoa ingeweza kutolewa na Makamu wa Rais, au Waziri Mkuu au hata Salva Rweyemamu! Haikuwa hotuba inayoendana na Urais kwani kwenye suala muhimu la Muungano alitakiwa kutoa msimamo badala ya "kuwaomba" viongozi wenzake.

  Kilichodhihirika ni kuwa kama tunataka kuleta mabadiliko ya kweli, kelele za hapa mtandaoni zinapoteza muda na kwa hakika hazifiki kunakotakiwa. NI kwa sababu hiyo nimeamua kutilia mkazo na nguvu zangu zote kwenye kukiendeleza kijarida cha Cheche ambacho nataka kiwe ni nguvu ya kupambana na ufisadi na hata ikibidi kutoka kila siku bure nitafanya hivyo. Nataka kuhakikisha kuwa mwananchi wa kawaida anapata access ya mawazo na fikra nzito, na hoja zenye nguvu ili ziweze kuteka fikra zake.

  Ni kwa sababu hiyo, naamua kuchukua likizo isiyo na muda ya kuachana na Kuandika na kutilia mkazo uwanja mpya wa mapambano ambao ni fikra za wananchi wa kawaida wasio na mtandao. Tumeanza kuwafikia wiki hii iliyopita na tunataka tuwafikie zaidi sasa. Kuendelea kujibishana hapa na kulumbana na kubezena na kuwashiwishana ni kupoteza muda kwa sababu naamini hakuna watu ambao wako so informed kuhusu nchi yao kuliko watu wa Tanzania. Nadhani hapa tumebakia kuhubiri kwa wanakwaya wetu na tumeendelea kuimba pambio ndani ya kanisa. Tunachofanya sasa hapa ni kuendelea kufanya maulidi kwenye madrasa! Lazima tutoke humu na kwenda kuwa mwanga na nuru kule nje.

  So, I said it, tulifanya makosa tulipomchagua Kikwete na ni wajibu wa kila Mtanzania anayeitakia nchi mema, na ambaye anataka Taifa jipya, la kisasa, la kizalendo na lilo nona kwa mafanikio kuwepo kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa Kikwete na maswahiba wake hawarudi tena Ikulu 2010 na kuvunja huu uigizaji wa uongozi unaofanywa nao. Sidhani kama kuna kitu chochote ambacho Kikwete atakifanya sasa ambacho kitanifanya nimpe nafasi nyingine ya kumuamini.
   
 13. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
 14. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu Proffessor Baregu ndiye Mwanakjj au?Maana I have read something very similar to this ambayo ilipostiwa na Mwanakjj akisema anachukua likizo!
   
 15. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2008
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mambo yote 2010...baada ya haya yooooote watanzania watamchagua tena kipenzi chao JK tena kwa "landslide victory"...watanzania ndivyo tulivyo...
   
 16. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  umeniwahi tu na mimi nilitaka kuhoji vivyo hivyo.
   
 17. H

  Haika JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  kila mwana jf ambaye hajajitaja jina mtu fulani mwenye jina lake la kweli, mimi nilishawahi kusikia mwanakijiji alipohojiwa BBC sikumbuki kama ilikuwa sauti ya Prof.
  Anyway tunathamini michango yenu (yako) sana
   
 18. n

  nat867 Member

  #18
  Aug 27, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu MJJ heshima zikufikie kwa kweli makala yako imeeleza kinagaubaga mahali tulipo.. hii pia inaendana na ile iliyopo katika gazeti la Mwanahalisi ya Ndimara kuhusu " Sakata la EPA: Kikwete avuruga utawala bora".

  mbarikiwe, kwa makala murua...

  "watanzania ehe!, mimi kikwete nimeshinda na ninawaogopa mafisadi":(
   
 19. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji funika,

  Katika meeengi yaliyosemwa ambayo sina haja ya kuyarudia napenda kuongezea moja tu.Katika kuogopa kuwa prosecute wahalifu kwa sababu eti "wanaweza kushinda kesi na hela tusipate" Kikwete anajionyesha kwamba hana imani na justice system ya Tanzania.

  Go figure, rais wa nchi hana imani na justice system sisi wakalamba ndio tutasemaje?

  On the other hand hiyo ni karata tu inatumiwa, mimi naona ushahidi kwamba hapa kuna mambo mabaya kuliko wote tunavyofikiri na pia Kikwete personally yuko implicated either directly or by proxy katika uchafu huu, ndiyo maana anagwaya.

  Otherwise he is extremely stupid, even more than I thought him to be.
   
 20. M

  Major JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2008
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  hivi huyu kikwete ni mvinyo gani aliopewa unaomlewesha tangu ameingia ikulu mpaka leo na hata kama ni heng over si huwa inaisha?sasa hii ya huyu mkwere itaisha lini? lakini pia kuna kila sababu ya kutumia kama kuna vipimo vya DNA tuangalie kama ktk huu ukoo kuna asili ya utawala maana hii siyo bure!!!!!!!
   
Loading...