Carl Peters Mkono wa damu na koloni la Tanganyika

Karl Peters ndiye aliyeifanya Tanganyika iwe a huge nation in east africa. Ndiye aliyetupatia mlima kilimanjaro la sivyo mlima ungekuwa kenya
 
Kwa habari za nyongeza soma wikipedia ya Kiswahili Karl Peters - Wikipedia, kamusi elezo huru.

Jina la "mkono damu" alijipatia kwa njia ya kusikitisha mno:
Akiwa mwakilishi Mjerumani Kilimanjaro Peters alikuwa na mabinti wenyeji aliowatumia kama wapenzi wake. Usiku wa tarehe 18 Oktoba 1891 Peters alimkuta binti Yagodja pamoja na Mabruk mtumishi wa kiume wakilala pamoja. Peters alikasirika mno akaita mara moja kamati ya mahakama akiwa yeye mwenyewe mwenyekiti. Mtumishi wake Mabruk alihukumiwa anyongwe. Yagodja alikimbia lakini akakamatwa Januari 1891 akapigwa viboko na kunyongwa naye.

Katika hasira yake Peters aliamuru hata kijiji cha binti huyo katika eneo la Rombo kichomwe moto. Wachagga wa Rombo walichukua silaha na kujitetea. Hasira ya Peters ilisababisha vita vya miezi kadhaa, vijiji vingi viliharibika na watu kufa.


Baada ya habari hizi kufika Ujerumani vyama vya upizani walimshtaki Peters bngeni wakamwita "Hänge-Peters" yaani "Peters mnyongaji".

Hata hivyo jinsi ilivyo mara nyingi katika historia: yeye aliunganisha maeneo yanayofanya leo hii Tanzania bara. Historia inaonyesha mababu wa taifa wanaoweza kusikitisha au kuaibisha.
Je ni kosa kusema: hakuna Tanzania bila Karl Peters?
Hizo tarehe hapo juu zimenichanganya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom