Carl Peters Mkono wa damu na koloni la Tanganyika

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779

Monday, 03 October 2011 13:51
CARL Peters,
07dkkarl.jpgNa Lawrence Kilimwiko

CARL Peters, yule mjerumani tapeli mkubwa aliyewazuga machifu na kupoteza uhuru wao aliwahi kutamka kwamba, "kuwapa uhuru watu weusi ni kosa la kijinga lisilopaswa kufanywa na nchi za werevu", yaani watu weupe.
Kwake yeye, watu weusi walikuwa ni watu wa kutumiwa kwani hata Biblia ilikuwa imehalalisha hivyo. Na kuthibitisha hilo, kila alikopita Carl Peters aliacha michirizi ya damu kwa ukatili usioelezeka aliowafanyia watu kiasi cha kupachikwa jina la "Mkono wa Damu".

Lakini wakati watanzania wanaadhimisha miaka 50 ya uhuru, Carl Peters hawezi kusahaulika kwa sababu yeye ndiye muasisi wa mipaka ya koloni lililokuwa linaitwa Tanganyika. Ni Carl Peters aliyewazuga na kuwatapeli machifu wa makabila mbalimbali na kuwaweka chini ya himaya ya Ujerumani.

Ni Carl Peters huyo huyo, aliyeratibu kwa karibu sana mkutano wa Berlin, huko Ujerumani wa mwaka 1884/85, ambapo mataifa ya ulaya yaligawana bara Afrika mithili ya shamba na kuhakikisha mipaka ya Tanganyika inakuwa kama ilivyo sasa (ukiondoa tu Rwanda na Burundi).

Kwa vyote vile, simulizi za vuguvugu la uhuru wa Tanganyika, haziwezi kukamilika pasipo kueleza mchango wake katika kueneza ukoloni. Yeye ndiye aliyekuwa kinara wa kufanikisha koloni la Afrika mashariki na kupelekea kile kilichoitwa kinyang'anyiro cha makoloni Afrika.

Harakati zake za kusaka makoloni ndizo zilizopelekea kuzaliwa kwa mipaka ya nchi inayoitwa Tanganyika ikiundwa na makabila takriban 150.

Simulizi zinasema kuwa Carl Peters alikuwa ni mjerumani mvumbuzi, mwanahabari na mwana filosafa aliyezaliwa tarehe 29 Septemba mwaka 1856 katika mji wa Hanover.

Baada ya masomo ya awali katika shule ya misheni ia Ilifeld, alijiunga na chuo cha Goettingen, Tubingen, na kasha Berlin ambako alisomea historia, filosofia na sheria.

Mwaka 1879, alihitimu Chuo cha Berlin akitunukiwa digrii katika historia.Mwaka uliofuata aliachana na kazi yake ya uanasheria na kwenda London, Uingereza alikoishi na mjomba wake tajiri.

Abuni Chama cha Makaloni ya Ujerumani

Katika kipindi cha miaka mine aliyokaa Uingereza Carl Peters, alijifunza historia ya Uingereza na kuchambua sera zake kuhusu makoloni na falsafa yake. Alirejea Berlin baada ya mjomba wake kujiua mwaka 1884 na kuanzisha Chama cha
Makoloni ya Ujerumani .

Akiwa na shauku ya kuona Ujerumani akijipatia makoloni, mwishoni mwa mwaka 1884 Carl Peters alisafiri kuja Afrika Mashariki kufanya mikataba na machifu.

Licha ya kutopewa kibali na Serikali ya Ujerumani, Carl Peters alikuwa na matumaini kwamba juhudi zake hizo zingesaidia Ujerumani kupata makoloni Afrika.

Baada ya kufika Bagamoyo hapo Novemba 1884, Carl Peters na msafara wake walitumia majuma sita wakiwashawishi machifu na waarabu kusaini mikataba ya ardhi na njia za kibiashara.

Moja ya mkataba unaojulikana sana ni ule aliomsainisha chifu Mangungo wa Msovero huko usagara (Kilosa) ambaye eti alikubali, "kumwachia himaya yake na watu wake na kila kitu" kwa "matumizi pekee ya mpango wa makoloni ya Ujerumani".

Carl Peters alirejea Ujerumani tayari kukamilisha mafanikio ya mipango yake Afrika. Tarehe 27 Februari 1885, kufuatia kumalizika kwa mkutano wa Berlin, Kansela wa Ujerumani Bismark alitangaza kuanzishwa kwa himaya ya Ujerumani Afrika Mashariki. Chama cha Ujerumani Afrika Mashariki kiliundwa mwezi Aprili na Carl Peters kutangazwa kuwa mwenyekiti wake.

Kwa kuanzia, kilomita 18 za ukanda wa pwani zilitambuliwa kuwa ni eneo la Sultan wa Zanzibar. Lakini mwaka 1887, Carl Peters alirejea Zanzibar na kupewa kibali cha kukusanya kodi. Hata hivyo, baada ya miaka miwili eneo hilo lilinunuliwa kutoka kwa Sultan wa Zanzibar kwa Paundi 200,000 na kwa kuchanganya na eneo la kilomita za mraba takriban 900,000 upande wa bara, eneo lote hilo likawa mali ya Ujerumani.

Kumtafuta Emin Pasha

Mwaka 1889, Carl Peters aliacha nafasi yake ya uenyekiti wa German East Africa na kujerea Afrika Mashariki.Safari hii ilikuwa ni katika kukabiliana na changamoto ya safari ya Henry Stanley (mwanabahari mwingine) ya kumtafuta Emin Pasha, mjerumani mvumbuzi na Gavana wa eneo la sasa la Sudan ambaye ilielezwa kuwa alikuwa amezingirwa ndani ya himaya yake na majeshi ya Mahd.

Carl Peters alitangaza azma yake ya kumshinda Stanley katika kinyang'anyiro cha zawadi ya kumwokoa Emin Pasha. Baada ya kufutika mfukoni kitita cha Maki za Kijerumani 225,000 Carl Peters na watu wake waliondoka Berlin mwezi Februari kuja Afrika Mashariki,

Kugombea Ardhi na Mwingereza

Baadaye ilikuja kubainika kwamba safari ya Carl Peter ilikuwa imelenga katika kupata maeneo makubwa zaidi hasa upande wa kaskazini ikibidi hadi kwenye mto Nile kaskazini mwa Sudan. Huku Stanley akifanya kazi kwa niaba yaMfalme Leopold wa Ubelgiji huko Congo, Carl Peters alikuwa akifanya hivyo hivyo kwa niaba ya Ujerumani.

Lakini mwaka moja baada ya kuondoka na akiwa amefika eneo la Wasoga katikati ya maziwa Victoria na Albert nchini Uganda , alipokea barua ya Stanley ikimwarifu kwamba Emin Pasha alikuwa tayari ameokolewa. Akaelezwa pia kwamba Uganda ilikuwa imenyakuliwa na Uingereza kama sehemu ya himaya yake.

Mkono wa Damu
Kwenye mkataba wa Heligoland wa tarehe 1 Julai 1890 ulioweka mipaka kati ya himaya za Uingereza na Ujerumani katika Afrika Mashariki, Uingereza ilichukua Zanzibar na eneo la kaskazini mwa Zanzibar ikimaanisha Kenya na Uganda wakati Ujerumani ilichukua Tanganyika bara zikiwemo Rwanda na Burundi. Zaidi ya hapo Ujerumani ilitwa eneo la mlima Kilimanjaro na kufanya mpaka wa Tanzania na Kenya uwe kama ulivyo hivi sasa.

Mwaka 1891 Carl Peters alitangazwa kama Kamishina wa eneo linaloitwa German East Afrika, makao yake yakiwa Kilimanjaro.

Hata hivyo, ilipofika mwaka 1895 taarifa zilifika Ujerumani kuhusu ukatili wa kutisha uliokuwa unafanywa na Carl Peters kwa watu weusi kiasi cha kupachikwa jina na "Mkono wa Damu".

Carl Peters alirejeshwa Ujerumani na tume ikaundwa kuchunguza madai hayo, na mwaka uliofuata alihamishiwa London. Mwaka 1897 Carl Peters alitiwa hatiani dhidi ya ukatili wake kwa watu weusi wa Tanganyika. Adhabu aliyopewa ilikuwa kufukuzwa katika utumishi wa serikali.

Akiwa London alianzisha kampuni binafsi iliyoitwa Dr. Carl Peters Exploration Company ambayo ilifadhili safari kadhaa kwenda German East Africa na British Territory karibu na mto Zambezi. Safari hizi ndizo zilizopelekea kuchapishwa kitabu chake cha The Eldorodo of the Ancients.

Baada ya kusamehewa na Mfalme Wilhelm II na kurejeshewa kiinua mgongo chake, mwaka 1890 Carl Peters alirejea Ujerumani wakati kukiwa na vugu vugu la vita ya kwanza ya dunia.

Baada ya kuchapisha vitabu kadhaa, Carl Peters alistaafu na kurejea Bad Harzburg ambako alifariki tarehe 10 Septemba 1919 akiwa na umri wa miaka 63.Baada ya vita kumalizika Carl Peters alitangazwa na mtawala wa wakati huo Adolf Hitler kuwa ni shujaa wa Ujerumani na vitabu vyake vikachapishwa upya.

Hapa Tanganyika hata hivyo," Mkono wa Damu" anakumbukwa zaidi kwa ukatili kwani kote alikopita aliacha nyuma mizoga na mazizi matupu baada ya kuchomo moto vijiji vya watu hata pale pasipo na ulazima kufanya hivyo.

Alilazimisha watu kubeba mizigo mizito katika safari zisizo na mwisho za kutafuta makoloni na unyang'anyi wa nchi za watu. Kwa kuwalaghai machifu kama vile Mangungo wa Msowero huko Morogoro, Karl Peters alifanikiwa kuiweka Tanganyika mikononi mwa wajerumani kama koloni katika mipaka inayojulikana sasa.
 
BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,516
11,823
Duuh historia nzuri ila kwa elimu ya tanzania ya sasa,elimu imeharibiwa watoto hawatajua mambo haya
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
Tatizo sasa hivi historia watoto wetu wanafundishwa ni za ajabu; hawajui Tanganyika ilianzaje; hawamjui Carl Peters ni nani? Sasa hivi tunaenzi historia isiyonifuaisha maendeleo ya utanganyika.

Sasa hivi watu woote walio na pesa wanasomesha wanao Afrika ya kusini, Malaysia, Poland sasa watajuaje kwanini Mji Mashuhuru ukaitwa Dar-es-salaam? ni kwanini Tulipigana na Nduli Idd Amin, lakini kwanini baba yao ni Mwanajeshi na anakomba pesa za Ghadaffi ???

Shame Shame Shame...
 
Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,663
504
Kwa habari za nyongeza soma wikipedia ya Kiswahili Karl Peters - Wikipedia, kamusi elezo huru.

Jina la "mkono damu" alijipatia kwa njia ya kusikitisha mno:
Akiwa mwakilishi Mjerumani Kilimanjaro Peters alikuwa na mabinti wenyeji aliowatumia kama wapenzi wake. Usiku wa tarehe 18 Oktoba 1891 Peters alimkuta binti Yagodja pamoja na Mabruk mtumishi wa kiume wakilala pamoja. Peters alikasirika mno akaita mara moja kamati ya mahakama akiwa yeye mwenyewe mwenyekiti. Mtumishi wake Mabruk alihukumiwa anyongwe. Yagodja alikimbia lakini akakamatwa Januari 1891 akapigwa viboko na kunyongwa naye.

Katika hasira yake Peters aliamuru hata kijiji cha binti huyo katika eneo la Rombo kichomwe moto. Wachagga wa Rombo walichukua silaha na kujitetea. Hasira ya Peters ilisababisha vita vya miezi kadhaa, vijiji vingi viliharibika na watu kufa.

Baada ya habari hizi kufika Ujerumani vyama vya upizani walimshtaki Peters bngeni wakamwita "Hänge-Peters" yaani "Peters mnyongaji".

Hata hivyo jinsi ilivyo mara nyingi katika historia: yeye aliunganisha maeneo yanayofanya leo hii Tanzania bara. Historia inaonyesha mababu wa taifa wanaoweza kusikitisha au kuaibisha.
Je ni kosa kusema: hakuna Tanzania bila Karl Peters?
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
95,530
163,260

kama hakufika Zanzibar , tafadhali ihusishe Tanganyika tu , siyo Tanzania.
 
mpalu

JF-Expert Member
Sep 15, 2010
2,520
868
Kwa kuanzia, kilomita 18 za ukanda wa pwani zilitambuliwa kuwa ni eneo la Sultan wa Zanzibar. Lakini mwaka 1887, Carl Peters alirejea Zanzibar na kupewa kibali cha kukusanya kodi. Hata hivyo, baada ya miaka miwili eneo hilo lilinunuliwa kutoka kwa Sultan wa Zanzibar kwa Paundi 200,000 na kwa kuchanganya na eneo la kilomita za mraba takriban 900,000 upande wa bara, eneo lote hilo likawa mali ya Ujerumani.
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
Kwa kuanzia, kilomita 18 za ukanda wa pwani zilitambuliwa kuwa ni eneo la Sultan wa Zanzibar. Lakini mwaka 1887, Carl Peters alirejea Zanzibar na kupewa kibali cha kukusanya kodi. Hata hivyo, baada ya miaka miwili eneo hilo lilinunuliwa kutoka kwa Sultan wa Zanzibar kwa Paundi 200,000 na kwa kuchanganya na eneo la kilomita za mraba takriban 900,000 upande wa bara, eneo lote hilo likawa mali ya Ujerumani.

Sultani wa ZNZ hakuwa anazijali hizo kilometa 18 za ukanda wa PWANI; Alikuwa hazitumii as ADMINISTRATION AREA but as area to collect some fees as well as easy to transport their TRADE from INLAND such as IVORIES, Then Slaves...

Lakini hawakuwa hawataki kuwa na HIMAYA kwenye hizo PWANI labda ENEO la MOMBASA
 
simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,271
8,976

Tunarudi pale pale, mipaka rasmi ya Tanganyika huru, Tanganyika ya Mwalimu ni ipi? Hasa mashariki.
 
Kasimba G

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
3,428
2,609
Duuh historia nzuri ila kwa elimu ya tanzania ya sasa,elimu imeharibiwa watoto hawatajua mambo haya
Ni nzuri lakini kwa nchi yetu hii hatutaki kuwa na history ya ukweli,kilakitu ni propaganda, utasikia, Uhuru wa Tanzania, Muungano wa Tanzania na Zanzibar e.t.c. Mbaya saana hii, hatujitambui kabisaaaaaa!
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
Tunarudi pale pale, mipaka rasmi ya Tanganyika huru, Tanganyika ya Mwalimu ni ipi? Hasa mashariki.

Ni ambayo MJERUMANI alitawala -- Na NDIO TANGANYIKA NYERERE aliyoichukua haikuwa na any strings attached....
 
mpalu

JF-Expert Member
Sep 15, 2010
2,520
868
Tunarudi pale pale, mipaka rasmi ya Tanganyika huru, Tanganyika ya Mwalimu ni ipi? Hasa mashariki.

Kwa kuanzia, kilomita 18 za ukanda wa pwani zilitambuliwa kuwa ni eneo la Sultan wa Zanzibar. Lakini mwaka 1887, Carl Peters alirejea Zanzibar na kupewa kibali cha kukusanya kodi. Hata hivyo, baada ya miaka miwili eneo hilo lilinunuliwa kutoka kwa Sultan wa Zanzibar kwa Paundi 200,000 na kwa kuchanganya na eneo la kilomita za mraba takriban 900,000 upande wa bara, eneo lote hilo likawa mali ya Ujerumani.
 
mpalu

JF-Expert Member
Sep 15, 2010
2,520
868
Sultani wa ZNZ hakuwa anazijali hizo kilometa 18 za ukanda wa PWANI; Alikuwa hazitumii as ADMINISTRATION AREA but as area to collect some fees as well as easy to transport their TRADE from INLAND such as IVORIES, Then Slaves...

Lakini hawakuwa hawataki kuwa na HIMAYA kwenye hizo PWANI labda ENEO la MOMBASA

kuna ubishi ule wa eneo la Tanganyika
 
simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,271
8,976
Kwa kuanzia, kilomita 18 za ukanda wa pwani zilitambuliwa kuwa ni eneo la Sultan wa Zanzibar. Lakini mwaka 1887, Carl Peters alirejea Zanzibar na kupewa kibali cha kukusanya kodi. Hata hivyo, baada ya miaka miwili eneo hilo lilinunuliwa kutoka kwa Sultan wa Zanzibar kwa Paundi 200,000 na kwa kuchanganya na eneo la kilomita za mraba takriban 900,000 upande wa bara, eneo lote hilo likawa mali ya Ujerumani.

Jibu swali mpaka wa mashariki wa iliyekuwa Jamhuri yaTanganyika uliangukia wapi?
A) Kibaha
B)Magogoni
C)km 22 ndani ya bahari Hindi kutoka ufukoni.
D) sijui.
(Mpaka wa magharibi ndio mgogoro na Malawi)
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
Jibu swali mpaka wa mashariki wa iliyekuwa Jamhuri yaTanganyika uliangukia wapi?
A) Kibaha
B)Magogoni
C)km 22 ndani ya bahari Hindi kutoka ufukoni.
D) sijui.
(Mpaka wa magharibi ndio mgogoro na Malawi)

Kabla ya Mwarabu kuwasili PWANI ya Africa ya Mashariki ilikuwa kama sasa kawaida Bahari ya HINDI hadi ARDHI ya TANGANYIKA...

** Issue ya MALAWI waligawana hilo ziwa MALAWI wakati UINGEREZA ilipokuwa ina-create alliance kati ya RHODESIA; NORTHERN RHODESIA na MALAWI hapo ndipo MWINGEREZA alipobadilisha Ramani ya ZIWA NYASA na kuonyesha ziwa lote kama mali ya MALAWI... wakati huo MWINGEREZA alipewa Tanganyika kama Protectorate hakuwa na HIMAYA nayo sana kama hizo nchi zingine nilizozitaja...
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
6,216
4,563
Sultani wa ZNZ hakuwa anazijali hizo kilometa 18 za ukanda wa PWANI; Alikuwa hazitumii as ADMINISTRATION AREA but as area to collect some fees as well as easy to transport their TRADE from INLAND such as IVORIES, Then Slaves...

Lakini hawakuwa hawataki kuwa na HIMAYA kwenye hizo PWANI labda ENEO la MOMBASA

Siasa tu mkuu, Sultan alinyang'anywa kwa shindizo eneo la Tanganyika si kwa ridhaa, Wajerumani na Waingereza wlikua wamemkalia vibaya sana. Ilimbidi tu awaachie maeneo mengine Ili apate kubakia yeye.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Top Bottom