WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
CCM 2011 NA MAKAMBI YAKE MBALI MBALI NCHINI
Hivi kati ya hizi CCM mbali mbali hivi sasa nchini, wewe ni wa kundi gani hasa hapa chini???
1. CCM- Uadilifu (Wazee wenzake na Mwalimu Nyerere ambao ni watulivu, wakomavu na masikini wa kutupwa kwa kuipenda sana nchi na wenye moyo kuitetea Tanzania).
2. CCM- Ufisadi ( Ni kundi dogo linalojiita Wanamtandao au kumbakumba wa kila dili / mchecheto wa kila senti irukayo hewani wenye utayari wa kuuza hata mtoto wake alimradi fedha ipatikane zaidi kufanyia kila aina ya uchafu unaoweza kufikiria; ni wale ambao mpaka hivi sasa wamepepetwana pembeni wasio na kitu na kubakia RA + EL).
3. CCM-Unguja (Chama cha Wazanzibara kama Vuai wa Kondoa na Hussein Mwinyi wa Kisarawe Umatumbini).
4. CCM-Yatima (Ni wale akina Sumaye, Kigoda, Mungai, banduka, Komanya, Ngulume, na wengine waliokua chini ya BWM).
5. CCM-Bongo Flava (Rizi1, Februari Ma-Ropes, Ndungai, Malisa, Nchimbi, ... hawa hawana hela ila kamsimamo wa uongo na kweli)
6. CCM-Mwandosya / Mangula (Kanda ya Juu Kusini)
7. CCM- Six/John Liquor Ma-Padlocks (Kanda ya Ziwa)
8. CCM- Two Coins Mramba / Mrema / Mbatia (moshi Vijijini)
9. CCM-Uislamu (Pwani/ Tanga / Mashariki na Pemba)
Sasa hapa mtu unapoongelea CCM ni sharti uwe makini sana sana na ijulikane kwamba unazungumzia CCM ipi hasa.
Huu mchanganuo au sijui ndio upembuzi umeniacha hoi!