Carbon credit business | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Carbon credit business

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Malila, Oct 3, 2010.

 1. M

  Malila JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kadiri mabadiliko ya tabia nchi yanavyoongezeka ndivyo mwanadamu anavyotafuta mbinu zaidi za kujihami.

  Sasa hivi upo mpango wa kutoa malipo kwa Watz waliopanda miti kwa wingi ktk eneo moja. Kwa sasa mpango huu uko ktk mkoa wa Iringa.Kuna kampuni moja kubwa ya upandaji miti inausimamia mpango huu. Watakachofanya, wanapima kipenyo cha miti yako,umri wa miti,kisha wanakwambia miti yako italipiwa kiasi gani kila mwaka. Malipo yatakuwa yanaongezeka kila mwaka kwa kadri mti unavyopanuka.

  Bahati mbaya watakaofaidi fedha hizi ni wageni kupitia makampuni haya,sisi tunaishia kupiga soga na kulalamika. Hapa jamvini kuna mtu anatumia ID ya Edson,nina hakika anaweza kutuweka sawa ktk hili.

  Ikiwa ni kweli mpango huu utapanuka mpaka kwa watu wa chini,basi ni muhimu tuunganishe nguvu ili nasi tufaidi
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mkuu nami nimesikia hiyo habari ya carbon credit - ningependa sana kujua zaidi inavyofanya kazi.
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mpango mzima uko hivi; kama una miti uliyopanda vizuri na unaitunza,wao wanaandikisha jina lako na kiasi ulicho nacho,wanapima kipenyo cha miti yako ili kujua kiasi cha carbon kinachokuwa-consumed na miti yako ili kupata thamani kwa kila mti. Sasa wao wanakulipa kwa mwaka,kwa kule Mfindi Green resources Limited ndiyo ambao wameanza kutoa elimu hiyo kwa wanavijiji wanaozunguka misitu yao.

  Bahati mbaya wengi tumepanda miti holela,tungekuwa tumepanda miti kwa mfumo wa estate,hii hela tungekula mpaka tunaingia kaburini. Ni zaidi ya pensheni ya Nssf/Ppf. Bado nafuatilia mpaka nione mwisho wake. Mwaka huu nimepeleka jina langu wilayani nasubiri majibu.
   
 4. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  Kenyan KenGen is eyeing at least Sh300 million (US$3.7 million) before the end of 2012 as proceeds from the carbon market deal it signed with the World Bank in 2006.

  Reported from the country, "Kenyan companies are missing billions of shillings in new revenue because of lack of expertise to develop projects that help reduce carbon dioxide emissions and therefore earn from the global carbon trading market.

  The global carbon trading market, which rewards projects that help reduce emission of carbon dioxide into the atmosphere, is now worth estimated Sh12.5 trillion ($170 billion), according to industry data provider, Carbin Point, but only a very small fraction of this money, estimated at two per cent, is coming to Africa.

  "We are not getting enough projects in Kenya. People are aware, but the proposals they present are poorly done," said Tom Owino, of JP Morgan Climate Care, which helps corporate and non-profit organisations earn from the carbon market.

  Proposals that are coming from Kenyan companies are requests for money to finance the intended projects with owners hoping to raise all the project money from the organisation which will buy the emission reductions.

  This is not supposed to be the case, Mr Owino said, because the serious project proposals must have part or all of the financing requirements.

  The proposal must also be accompanied by a good business plan that can raise the appetite of banks to finance the project.

  Banks in Kenya are yet to start active financing of carbon trading projects partly because of lack of skills needed to evaluate financing risk of such projects.

  KenGen is eyeing at least Sh300 million (US$3.7 million) before the end of 2012 as proceeds from the carbon market deal it signed with the World Bank in 2006.

  The company is seeking to earn the credits from the development of Olkaria II Unit 3 Project which is expected to produce 35MW of electricity when it starts operation around May 2010.

  Jane Watiri of the Green Earth Trust, which is helping organisations design carbon market projects and guide them how to earn from those projects said there is a huge pool of investors ready to finance viable projects that make business sense.

  "From our experience, financing a carbon trading project is not a problem. The only problem is getting a project that is viable on a project proposal that makes business sense," said Ms Watiri.

  One CER costs $10 or Sh760 based on Wednesday's exchange rate. But this price changes depending on the players involved.

  National Environment Management Authority (Nema) is charged with the responsibility of being a focal point in coordinating carbon market projects, but the industry said the authority is not visible in the Kenya's carbon market circles."
   
 5. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Asante kwa elimu hiyo Malila
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Taarifa hizi(the highlited) wengi hawazijui na wanaozijua ama hawataki kuziweka wazi au ni wabinafsi. Unaweza kufika pale idara ya misitu wakawa nazo na hawana mpango wa kuwahamasisha Watz ili wazifanyie kazi. Tumebaki tunalalama,ohh majirani zetu wanataka ardhi yetu, jamani tuamkeni tufanye mambo.

  asante majimoto,bado namtafuta mkuu mmoja anisaidie kuwapata GRL,ambao ni wahusika wakuu wa shughuli hii.
   
 7. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  carbon credits business at the expenses of our lives...yani tuache kulima na kuchimba madini tujikwamue na ufukara kufa tulokua nao tunakalia kulipwa vijisenti kuwatunzia mazingira wao waliokwisha-toboa ozone layer yote ikabaki kama kokoro za kuvulia samaki za magufuli...

  Am against huu upuuzi wao hawa wazungu...waanze wao kufunga viwanda na kuacha kuzalisha hewa ukaa (carbon) then waje kwetu kutuambia ujinga huo...zaidi ya hapo ni mbuaye-mbuaye bwana..ukimwaga mboga namwaga ugali....mbaka dunia ikauke maji ya bahari na mibarafu yote iyeyuke liwe jangwaaa kuu...nakataa hiyooooo
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  yah! ni kweli mkuu malila kama ulivyosema. kwa taarifa zaid tembelea www.greenresources.no kampuni hii inauza hewa ya ukaa( carbon). kinachofanyika hapo ni hivi : wanaangali una miti kiasi gani, then ina umri gani let say miti yako ina miaka mitano unachukua urefu wa miti yako( height) then unaangali unene wa mti wako . so ukishajua haya( umri wa miti , urefu, unene) wapo wataalamu watakufanyi mahesabu then watakwambia miti yako imevuta hewa chafu kiasi gani toka angani( carbon) utapat tani kadhaa.

  soko

  nchi zilizoendela zenye viwanda wao ndo wana jukumu la kununua hewa hiyo chafu maana wao wanachafua mazingira kwa kiasi kikubwa kutokana na viwanda vyao. so kuna makampuni yanafanya kazi ya udalali yatakuja katika eneo lako na kuiona hiyo miti na kiasi cha carbon ulicho nacho then wao wataenda katika nchi husika na hiyo nchi itatoa fedha na kunua hewa hiyo chafu.watu wengi hawaelewi hapa hiyo hewa chafu maana yake ni kwamba miti inapovuta hewa hiyo inasaidia kusafisha mazingiza na kupunguza mabadiliko ya tabia nchi kama vile ongezeko la joto nk so nchi zenye viwanda ndo kinara cha uchafuzi wa mazingira kwa hiyo wao wakinunua maana yake umewasaidia kusafisha mazingira.

  mpaka uuze hewa hiyo sio kazi ndogo kwani inabidi upewe cheti na mashirita ya kimataifa kama FSC, CDM , ISO nk.

  serikali yetu mpaka leo hawajui biashara hii licha ya kuwa na misitu kibao, kuna baadhi ya wabunge walikuja hapa tukawaeleza wakabaki kutoa macho.........
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  kwa watu binafsi wao wanatakiwa kila mmoja awe na miti yake then wakae katika vikundi na grl itawasaidia katika kuuza hewa hiyo ya ukaa( carbon). aisee hii kitu ina pesa sana serikali yetu haijui tu. grl ndo the largest afforestation company in Africa ikiwa na matawi mozambique, sudan, tanzania, uganda, na sasa malawi. wao ndo masupplier wa nguzo zote za umeme( tanesco) nchi nzima, wanauza mbao uarabuni, afganistani
   
 10. M

  Malila JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mkuu asante,

  Kaka nitakutafuta,niko na vishamba kadhaa vya miti, nimeyaona matusi ya grl pale Mapanda/chogo. Tayari niko na kikundi kikubwa sana,mwaka huu tumepanda miti kama milioni moja hivi,mwaka jana kama laki sita. Mwaka huu desemba tutapanda kama milioni moja na nusu hivi.

  Mwakani nitawafuata grl kule Uchindile. Nipe nondo zaidi kwa faida ya wadau.
   
 11. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ahsante Edson, Malila na Wakuu wote jamvini:
  Tengenezeni corporation, NGO, co-poorative,

  Nadhani viongozi wetu wanachukuaga muda kidogo kufikisha mikakati mitaani,. Wabunifu wako mitaani kwenye jamii. Wala hii mambo ya Hewa mkaa wakuu wangu, haina ugumu sana. wanatishia na paraganya mambo ili wanakijiji wadhani hawawezi kusimamia hii shughuli wao wenyewe. Watu wote wa mijini wasipewe hizi kazi. Sisi ndio waharibifu na sisi hawahwa ndio tunufaike, nadhani tungewasaidia kazi watu wa vijijini. Mjini iwe admistrative only. Nafikiri (sirkali) wanamajukum mengi, Ndugu wa wakubwa, and rafiki zao ndio wanawekewa hizo dili. Ili kuokoka and kufanya mabadiliko, tunatakiwa tushirikianeni, tuwasaidie kufanya mambo mengine ya kutatua ustawi wa jamii. Kama vile kufanya sensa ya miti inayokubalika kulipiwa katika shamba la mtu, si lazima tungoje sirikali, baadhi yetu tutapa kazi, na baadhi watapata cheki, ilhali wanaendelea na kazi zao za kila siku. corporation, non profit, co-operative, etc. hii ni investment, na moja ya bahati tukiifuatilia itasaidia kupunguza umasikini.
   
 12. K

  King kingo JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu hebu fuatilia utupe habari ili hivi vishamba tunavyotafuta tupande hiyo miti
   
 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Inabidi tumwombe Edson atusaidie,maana yeye yuko jikoni. Pili tupande miti kwa estate ili hata wakala akija kuangalia anaona kitu kimesimama.
   
 14. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280

  kama umeshapanda miti yote hiyo na bado unaendelea basi fanya utaratibu wa kuni PM pindi utakapokuwa tayari ili nikuunganishe na MD moja kwa moja na pilika za kuuza carbon zianze.. kwa sasa niko Sudan (juba) na wiki ijayo narudi TZ so kama vipi tuwasiliane ili uje uonane na MD mwenyewe then mambo yaanze...
   
 15. M

  Malila JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Presha inapanda,presha inashuka;

  Niko nje ya Dar,nategemea next week kurudi dar,na nitapitiliza Mapanda/Chogo kuangalia usalama na maendeleo ya kitalu cha miche. Nikitoka huko nitakutafuta na ikibidi nitakufuata hata kama utakuwa Mafinga.

  Mpaka hapo nakushukuru sana mkuu. Namwomba Mungu nipate hiyo fursa ya kuonana na MD na Mungu anipe kibali cha kusikilizwa na mkuu huyo.
   
 16. T

  Teko JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2010
  Joined: Jul 3, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hizi ni habari njema, je ni aina gani ya miti inayotakiwa kupandwa au miti yoyote tu? na kama mtu akiwa peke yake bila kikundi hawezi kupata soko hata kama akiwa na miti mingi sana? Naomba mnijuze tafadhali nisije hamasika kupanda miti isiyohitajika.
   
 17. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #17
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Tafadhali nitumie details zaidi nikanunue shamba kule Kimbiji nipande miti! Deal nzuri sana hii. Nitumie PM please.
   
 18. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Way to go MwanaHaki!. Huu uwekezaji katika kukuza miti, kwa maoni yangu nadhani bei wanayopewa wapandaji miti itaongezeka kidogo kidogo, kulingana na uzalishaji wa hii Carbon monoxide, na kemikali nyinginezo ambazo ni mbaya kwa afya yetu sote. Kulingana na mahitaji yetu sisi wanunuzi (ambao tuna hela), biashara zitaendelea kuzalisha kwa kutumia njia zinazotudhuru kwa sababu shida yao ni mafaida. Hali inaendelea kua mbaya, myoshi chungunzima hewani. moja ya solution ndio hii ya kupanda miti. Kiwastani kuongeza kiwango cha oxigen. Sasa myoshi ni mingi sana kiasi bora wahamasishe watu kwa kuwalipa wanaojenga Eco - Systems. Navile vile kuwachaji pesa vile viwanda vinavochafua mazingira.

  Ingekua vizuri tukiacha kuzalisha hewa mkaa na kufikiria njia zingine za uzalishaji ambazo zina shinikizo dogo kwenye mazingira yetu. Na sisi tupunguze matumizi ya kukata miti ya mkaa.
   
 19. M

  Malila JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ngoja tusubiri jibu la Edson, ninachojua mimi ni kwamba miti yote hupunguza carbon dioxide angani ambalo ndilo lengo kuu la mradi,sasa wao kama wame-specify jamii ya miti kutakuwa na sababu nyingine ya msingi zaidi. Kama mambo yatakwenda vema basi baada ya week mbili tutakuwa na jibu zuri juu ya hili suala. Kuhusu mtu binafsi angalia post ya Edson hapo juu alivyojibu. Vuta subira,muda si mrefu tutapata majibu.
   
 20. M

  Malila JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280

  Kimbiji si ni ndani ya jiji la Lukuvi? hawapimi viwanja huko mkuu. Ningekushauri uwe karibu huko huko waliko akina Edson ndio ununue pembeni yao na upande miti.
   
Loading...