FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,052
- 40,715
Ilikuwa ni sehemu ya parking ya magari mengi sana, nilishangaa kila nikifumgua gari kwa remote , kuna gari nyingine kama mita 10 toka nilipo nayo ikawa inatoa mlio kama inafunguka, nikifunga kwa remote na yenyewe inatoa mlio kwamba inafunga sambamba na ile inayolengwa. Nikarudia hilo zoezi la kufunga na kufungua kama mara 10 ili kujiridhisha.
Sasa naomba kujua, inawezekanaje remote ya alarm system ya gari moja inakuwaje inaweza kufungua na kufunga alarm system ya gari nyingine?
Ina maana kama yule mwenye gari nyingine angekuja kufungua gari yake, na yangu pia ingefunguka, na kama si muaminifu lolote linaweza kutokea