Captain Sully: Shujaa wa Marekani atatizmiza miaka 72 Tarehe 23/1/2022

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Ilikua ni Jan 25 mwaka 2009, ndege aina ya Airbus A320 mali ya Us Airways chini ya captain Chelsey Burnett (captain Sully) ikiwa na abiria 155 kwenye uwanja wa ndege wa laGuardia uliopo mji wa Newyork city ilikua ipo tayari kwa safari ya kuelekea Charlotte Airport huko North Carolina

Ndege ikiwa kwenye runway captain Sully akai set throttle to 100% tayari kwa ajili ya kupaa, ndege ikaondoka lakin muda mfupi baada ya ndege ku takeoff (kuondoka) ikiwa angani ikavamiwa na kundi kubwa sana la ndege (birds) wakaingia kwenye engine zote za ndege , injini zote zikaharibika, licha ya kuwa ndege ilikua bado ipo karibu na airport lakin captain Sully alishindwa kuirudisha ndege kwaajili ya kufanya Emergency landing.

Alishindwa kurudi kwasababu ndege ilikua chini ya lowest safe altitude (LSALT) namaanisha ilikua chini ya 500 feet toka usawa wa bahari, ndege ikifeli injin na ikawa ipo kwenye anga la chini inakua ipo kwenye hatari zaidi kuliko iliyopo kwenye anga la mbali, ikiwa chini huwez kufanya Emergency landing maana inakushinda kuiongoza na inatafuta sehem ya kujipigiza tu.

Ndipo ikabidi Captain sully akiwa na msaidizi wake Jeffrey skiles ilibidi waielekeze ndege kwenye mto uliopo karibu na uwanja wa ndege unaojulikana kama Hudson River ambao upo kama miles 126 toka ilipo LaGuardia airport Mungu ni mwema alifanikiwa kufanya Ditching (kutua kwa dharura kwenye maji) ndege ilitua salama kwa dharura juu ya mto huo bila kuleta madhara yeyote na watu wote 155 walitoka salama, ni miaka 13 Sasa toka tukio hilo lilipo tokea, Captain sully kwa Sasa ni shujaa naeishi ana miaka 71 na atatimiza miaka 72 siku 5 zijazo yaani tarehe 23 January.

Mtanisamehe kwa uandishi mbaya.
FB_IMG_1642539431097.jpg
 
Ndege imetua kwa dharaula watu wote wamepona.

Ingekua ni kwetu hapa tungeandika mengine ingekua msiba wa taifa.
 
Waqt kama haujafika kitatokea cha kutokea lakini Waqt ukifika unakuwa umefika.Pongezi kwa pilot na manusura wote walio okoka na kadhia hiyo
 
Kazi ya urubani inataka uwe jasiri sana,usione ndege zinaenda na kurudi,huwa wanakutana na matukio mengi sana wanapokuwa kwenye service,kwahiyo jinsi unavyozidi kuwa mvumilivu ndivyo unavyozidi kuwa bora zaidi kukabiliana nayo.Jaribu kufikiria ikishaondoka na kupaa juu,huko hakuna garage,hakuna fundi,hakuna kituo cha mafuta wala nini,ni wewe na anga tu,kila kitu kiko kwenye dashboard na kikikataa chochote pale wewe ndio uatakayeamua hatima ya abiria wako...
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom