Captain George Mazula wa Air Tanzania afariki dunia

Poleni familia katika wakati huu mgumu.

May all beings attain enlightenment.
 
Nimepatwa na butwaa juu ya habari za kifo cha Capt. Mazula George. Ni habari za kusikitisha sana. Nimemfahamu George kwa zaidi ya miaka 20 na nimefanya nae kazi kwa karibu katika sekta ya anga hapo Tanzania.

Ninawapa pole wafiwa na kuwatakia wapate moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao George.

Mungu ailaze roho ya marehemu George mahala pema peponi, amina.
 
Tunashukuru Mungu kwa kuendelea kutukumbusha kuwa hapa Duniani sote ni wapitaji.
Apumzike kwa amani. Amina
 
Capt MAzula ni miongozni mwa Wazalendo halisi wa Nchi hii na atakumbukwa kwa ujasiri wake pale alipoirusha ndege ya E.A Airways na kuishusha Tanzania wakati Jumuiya ya A. Mashariki inavunjika. Tumempoteza Shujaa na Mzalendo halisi.

BWANA alitoa na BWANA ametwaa, Jina lake lihimidiwe!

Taarifa yako siyo sahihi, waliohusika kipindi kile katika tukio unalolitaja ni Rubani Makinda (naweza kurekebishwa) na siyo George Mazula.
Hata hivyo tukio ambalo linahusisha jina la Mazula ni wakati ndege ya Air Tanzania ilipotekwa ikitokea uwanja wa ndege wa Mwanza na kulazimishwa kwenda hadi Uingereza. Hata hivyo Mazula aliyehusika siyo George bali ni Deo kama ambavyo wachangiaji wengine walionitangulia walivyojaribu kuiweka sawa posting mojawapo hapo juu.
 
Ctaki kuamini kama kweli Mazula Katutoka. The best Rubani we ever Had in TZ. I was so comfortable with his flight
RIP George

Uhuru wa maoni;

...Mkaguzi, nadhani Cpt DEO MAZULA, yule aliyetekwa na kurusha Boeing 737 ATC toka mwanza mpaka stanstead, hata pale Cpt Mwamaja alipojeruhiwa mguuni na risasi utamuweka kwenye daraja gani?, ....wakati huo Cpt George ndio kwanza alikuwa anarusha Fokker, anyway, tupo kwenye maombolezo.


 
Poleni wafiwa, by the way huyu ndie alietekwa na akina Yassin Memba?

HAPANA HUYU NI

MAZULA JR SR NDIE ALIETEKWA
 
Familia ya Mazula Jnr, ndugu, jamaa na marafiki wote mnauguswa na msiba huu naomba niwape pole sana.... George, RIP Brother, umetutangulia nasi tu nyuma yako, we will miss you Bro'

Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!!!!
 
Msiba Uko Nyumbani Kwake Mikocheni Karibu Na Itv!!!
Kwa Maelezo Zaidi Piga 0784 737 206/0754 884 185
 
Ukipanda La Mwenge Shuka Itv Ingia Kwa Ndani Au Uliza Msiba Wa Mazula Utaonyeshwa
 
Jamani Mbona Bokhe Munanka Anaondoka Na Marafiki Zake Hivyo
 
Poleni sana ndugu na marafiki wa mpendwa wetu Mazula. Nimemsikia mara nyingi sana huyu kaka yetu.

Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, amen.
 
Upumzike kwa amani, Mzee Mazula.

Brian na George, hivi karibuni mlipoteza kaka, leo mnamuaga Baba yenu, poleni sana, sana.
 
Back
Top Bottom